Rais Trump kutangaza hali ya dharura

Rais Trump kutangaza hali ya dharura

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Rais Donald Trump wa Marekani anatarajiwa kusaini muswada wa vyama viwili kuhusu bajeti ya usalama wa mpaka ili kuzuia idara za serikali kufungwa kwa mara nyingine tena, lakini pia atatangaza hali ya dharura ya kitaifa ili kujipatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka ambao ameahidi kwa muda mrefu. Muswada huo utaiwezesha serikali ya Marekani iendelee kufanya kazi katika mwaka huu wa fedha lakini hautatoa dola za kimarekani bilioni 5.7 alizohitaji rais Trump kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka na Mexico. Mabaraza mawili ya bunge la Marekani yataupigia kura muswada huo baadaye. Tangazo la hali ya dharura ya kitaifa, ambalo linaweza kumruhusu rais kukwepa Bunge na kutumia jeshi kujenga ukuta huo, linatarajiwa kuzusha kesi ya upinzani dhidi ya madaraka ya rais.

Swahili.cri
 
trump ni boya kama tundu lisu aseee. namshauri tundu lisu akaombe kazi kwa trump ya kusimamia ujenzi wa ukuta
 
Wewe ndo boya na mpuuzi unadhani aliyoyapitia Lissu hayawezi kukupata wewe,akili ndogo tu wewe.
 
Huku wanajeshi wanakuwa deployed tu bila utaratibu wowote mara korosho au sijui Bureau de Change mara wajenge ukuta Mererani

Tuna safari ndefu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom