Rais Trump amnyooshea mfanyakazi wa kiwanda cha Ford River Rouge kidole cha kati

Rais Trump amnyooshea mfanyakazi wa kiwanda cha Ford River Rouge kidole cha kati

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Rais wa Marekani Donald Trump amenaswa na kamera akionekana kuinua kidole chake cha kati na kutamka neno lenye maana ya tusi kwa mfanyakazi mmoja wakati wa ziara yake kwenye kiwanda cha Ford River Rouge huko Dearborn, Michigan siku ya Jumanne Januari 14, 2026.

Tukio hilo limekuja baada ya mfanyakazi huyo kumpiga kelele kwa kumuita "paedophile" yaani Mtu anaye dhalilisha watoto kingono, jambo lililo mfanya Rais Trump kumpa ishara ya kidole cha kati kabla ya kuendelea na matembezi yake na kushirikiana na wafanyakazi wengine.

Msemaji wa Ikulu ya White House alitetea majibu hayo, akiita jibu la rais "linalofaa na lisilo na utata" na tayari inaripotiwa kuwa Mfanyikazi wa kiwanda hicho amesimamishwa kazi na kampuni ya Ford kusubiri uchunguzi.

 
Ngoja na mimi nisubiri siku mke wa Ayatollah akifanya tu ziara huku mtaani nitamuonesha hiyo ishara ya kidole cha kati, halafu atakaye nisogelea namkata viganja vya mikono kwa kutumia hii sime yangu.
 
Back
Top Bottom