Rais Trump akerwa na hatua ya maseneta wa Democratic kukutana na Zarif

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Rais Donald Trump wa Marekani amekasirishwa mno na kitendo cha maseneta wa chama cha Democrat kukutana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kudai kuwa mikutano ya wanasiasa wa chama hicho na Zarif, ndio sababu inayoifanya Tehran isikubali mazungumzo na Washington.

Trump ambaye anakosolewa vikali kutokana na siasa zake mbovu kuihusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba kitendo cha baadhi ya wanasiasa wa Democrat kukutana na Zarif, ndio sababu inayoifanya Tehran kukataa kufikia mapatano mapya na Marekani. Akizungumzia vikao vya 'Chris Murphy' Seneta wa Democrat na 'John Kerry', Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani pamoja na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Twitter kwamba: "Kerry na Murphy wamekiuka sheria ya Logan." Sheria ya Logan inazuia mazungumzo yasiyoruhusiwa ya shakhsia wasio wa kiserikali wa Marekani na serikali nyingine za kigeni.

Idadi kadhaa ya wanachama wa Democrat wakiongozwa na Chris Murphy' Seneta wa jimbo la Connecticut walikutana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kando ya mkutano wa Usalama wa mjini Munich, Ujerumani. Kufuatia suala hilo Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema kuwa kikao hicho kinahesabiwa kuwa sehemu ya udiplomasia wa kijamii. Aliongeza kuwa daima Zarif amekuwa akisisitiza kuwa baadhi ya wawakilishi wa bunge la Kongresi ya Marekani wanaoomba vikao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, huwa anawakubalia na kukutana nao ambapo huwa anawabainishia uhalisia wa mambo kuhusu misimamo ya Iran na hali ya mambo ya Asia Magharibi.

4bv5e56a27cd931kigt_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni wanafiki tu, Democrats hawawezi kushinda uchaguzi mwaka huu.

Iran warudi kwenye meza ya mazungumzo waongee na serikali ya Marekani waachane na hao akina Kerry wanaopiga siasa tu.
 
Haya mataifa ya Venezuela, Iran north korea na Russia sana sana yanaumiza tu wananchi wao

Mchina amerise kijanja sana bila mikwaruzano na US kakumbuka shuka kumekucha,hayo malumbano hayataisaidia Tehran sana wataishia kwenye hali mbaya ya kiuchumi

Mmarekani unaenda nae kwa akili na sio hadharani wanavofanya Tehran,any way Team ayatollah najua mtakuja mnaharisha ila tambua kadiri siku zinavoenda wananachi wa Iran wanaumia wakt Washington wakila bata

Wanaumia ila hawategemei Misaada Kama Taifa Lako

Wewe Ambae Mnategemea Misaada Nataifa Lako Bado Mnasumbuliwa Nanjaa Maradhi Namagonjwa Kibao Ushawahi Kusikia Hivyo Vitu Vikiitikisa TEHRAN

Unalakujifunza Kutoka TEHRAN Wewe Nataifa Lako

Pole Sanaaaa.....

Kama Unahisi IRAN Watarudi Upya Kwenye Meza Yamazungumzo Ambayo Inatakiwa Ije Namakubaliano Mapya Inatakiwa Uwaulize US Kwanini walijitoa Kwamakubaliano Ya Awali Na Halafu Uwaulize Kwanini wairan Wawaamini yakwamba hawawezi wakajitoa katika makubaliano mapya wanayoyataka !?

IRAN Hawatakaa warudi katika mazungumzo sababu tayari mazungumzo yalishamaliza namkataba ulishasainiwa na hata UN wanautambua

Kama unahisi IRAN Atarudi Katika Meza Yamazungumzo Na US Unaota Ndoto Mbaya Sanaa Waache Waendeleze Vikwazo Wakihisi Kila Mtu Anawaona Wao MIUNGU WATU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mataifa ya Venezuela, Iran north korea na Russia sana sana yanaumiza tu wananchi wao

Mchina amerise kijanja sana bila mikwaruzano na US kakumbuka shuka kumekucha,hayo malumbano hayataisaidia Tehran sana wataishia kwenye hali mbaya ya kiuchumi

Mmarekani unaenda nae kwa akili na sio hadharani wanavofanya Tehran,any way Team ayatollah najua mtakuja mnaharisha ila tambua kadiri siku zinavoenda wananachi wa Iran wanaumia wakt Washington wakila bata

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu,unafikra za kimaskini Sana,
 
Mzungu pori kutoka kwenye kanchi kanako nuka umasikini eti ana washauli viongozi wa Iran na urusi jinsi ya kuendesha mataifa yao .
Watu wa nchi yako wana Maisha gani mazuri kuwazidi raia wa Iran au Urusi?
Uchumi wa jiji moja tu la Tehran ni sawa na uchumi wa nchi zote za afrika mashariki.
Pia unaitaji uchumi wa Nigeria na S. Afrika ndio upate uchumi wa jiji moja la Moscow.
Kwa hali hiyo unapata wapi ujasili wa kiandika uliyo yaandika?
 
Wanaumia ila hawategemei Misaada Kama Taifa Lako

Wewe Ambae Mnategemea Misaada Nataifa Lako Bado Mnasumbuliwa Nanjaa Maradhi Namagonjwa Kibao Ushawahi Kusikia Hivyo Vitu Vikiitikisa TEHRAN

Unalakujifunza Kutoka TEHRAN Wewe Nataifa Lako

Pole Sanaaaa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta Uzi hapa unaoelezea uswisi ikitoa msaada wa vifaa vya matibabu Tehran baada ya ruhusa ya mmarekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kaka iran ni ishu nyingine historia yao inawalinda hao ni waajemi alafu hao wafarisayo katika Biblia wanaakili kinyama miji yote mikubwa ya ukanda wa ghuba wafanya biashara mashhuri ni wairan ndo maana Israel inafyata mkia kwa Muiran kwasababu wanawajua hao watu hawajawahi kushindwa vita tangia enzi za mtume Nuhu kaka soma historia hicho nikizazi kingine wanasiri nyingi za dunia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta Uzi hapa unaoelezea uswisi ikitoa msaada wa vifaa vya matibabu Tehran baada ya ruhusa ya mmarekani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukileta Uzi Unaosema IRAN Kapewa Misaada Kutoka Uswizi Naachana Na Jf Kuanzia Mda Utakao Toa Huo Ushahidi

IRAN Hajapewa Msaada Bali Kapewa Go Ahead Yakununua Bidhaa Ambazo Awalu Alikua Haruhusiwi Sababu Yavikwazon

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaumia ila hawategemei Misaada Kama Taifa Lako

Wewe Ambae Mnategemea Misaada Nataifa Lako Bado Mnasumbuliwa Nanjaa Maradhi Namagonjwa Kibao Ushawahi Kusikia Hivyo Vitu Vikiitikisa TEHRAN

Unalakujifunza Kutoka TEHRAN Wewe Nataifa Lako

Pole Sanaaaa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Misaada inawahusu kama kawa
Radio Free Europe/Radio Liberty, rferl.org, free, press freedom, news, features, blogs › us-briain...
U.S. Criticizes EU For Sending Aid To Iran, Says Money Will Be Misused

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbna sijaona hio habar mkuuIla hapo waliposema money will be mis-used walimaanisha nn !?

Hakuna msaada alopewa IRAN Nipe Hio Habari Ilokamilika Wacha Kuruka Ruka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii pia
 
Haya mataifa ya Venezuela, Iran north korea na Russia sana sana yanaumiza tu wananchi wao

Mchina amerise kijanja sana bila mikwaruzano na US kakumbuka shuka kumekucha,hayo malumbano hayataisaidia Tehran sana wataishia kwenye hali mbaya ya kiuchumi

Mmarekani unaenda nae kwa akili na sio hadharani wanavofanya Tehran,any way Team ayatollah najua mtakuja mnaharisha ila tambua kadiri siku zinavoenda wananachi wa Iran wanaumia wakt Washington wakila bata

Sent using Jamii Forums mobile app
Trump anataka dili za Obama kule Iran apewe yeye, dili za Mafuta za Bush kule Venezuela azikombe yeye ndo maana anahangaika na vikwazo
 
Link namba moja kunapesa iran ilitakiwa ipewe pesa kama fidia yavikwazo waloekewa baada ya US kujitoa kwa JCPOA

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii pia
Link Namba Mbili Nikwamba Hakuna Pesa IRAN Walopewa Hao Jamaa walikua wanaimba taarab 2 hawana lolote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom