Rais Trum apost video akigawa kichapo mtu aliyekuwa na nembo ya CNN kichwani kwake

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video katika mtandao wa Twitter ikimuonyesha akimpiga mtu aliye na nembo kichwani ya shirika la habari la CNN.

Video hiyo iliyofanyiwa ukarabati ni ile inayomuonyesha Trump wakati alihudhuria michezo ya mieleka ya WWE mwaka 2007, ambapo 'alimshambulia' mmiliki wa michezo hiyo Vince McMahon.
Video hiyo inaonekana kuchapishwa katika mtandao wenye kumpendelea Trump mapema wiki hii.

CNN baadaye ilimlaumu Rais kwa kuibua ghasia dhidi ya vyombo vya habari
Lakini mshauri wa masuala ya usalama nchini Marekani Thomas Bosset, ambaye awali alihojiwa na kituo cha ABC alisema video hiyo haionekani kuwa tisho.

Mara kwa mara Rais Trump amekuwa kwenye mzozo na kituo cha CNN anachokiita 'taarifa bandia'




Chanzo: BBC
 
Duh...

Hapo Trump anawapa waandishi warning kistyle. ...

Watch out. ...
 
Pata picha angekuwa ni Uncle Magu hapo kila mtu angetokwa na povu.
Tofauti wao na sie ni kwamba wao wanaamini "maneno maneno ameumbiwa mwanadamu hivyo hata mtu umseme mtu vipi wala kiongozi haumii ila tu usi-support ugaidi yaani kwa kusema kwa maneno wala nini utashughulikiwa kikamilifu"
 
Back
Top Bottom