Rais: Siyo lazima lakini fanya haya sasa

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,501
34,562
Trump aliwapiga mkwara wasaidizi wake waache kumuandikia maripoti mareeefu bali wawe precise and briefy.... Naandika kwa ufupi tu, sitaacha kukushauri hata kama nitaonekana mpuuzi kwa waliokuzunguka.

  1. Punguza the so called utumbuaji majipu bali tengeneza mfumo wa kisheria ambao utakuwa unatumbua atomatic. Tutakushukuru na kukumbuka muda wote wa uhai wa Taifa letu ukifanya hivyo
  2. Punguza ama acha kufanya harakati za kiuongozi bali be either Commander In Chief or Comforter in Chief uwapo majukwaani.
  3. Waziri wako akitoa tamko la hovyo nawe usijibu kupitia tamko maana ni sawa na mtu kupigana na mkewe ili kumfunza adab. Zuia utekelezaji wa tamko hilo and taarifa itolewe baadaye
  4. Kuwa makini na wasaidizi wanaokuletea taarifa. hakikisha unawafanyia vetting ya kutosha na chuja sana taarifa kabla ya kuact
  5. Each one Teach one. WALAMI wanaitumia sana hii falsafa sasa hivi ndo maana unaona kama wapo kimya vile
  6. Wawekezaji wakifunga biashara hakikisha tuna plan mbadala la sivyo unemployment level itapanda sana.
Wait and Hope ni msingi mkubwa kwa mwenye hekima yeyote.
 
Nani alikwambia anapokea huo ushauri aliouita udaku wa kwenye mitandao?
Au wewe ulimsindikiza kuchukua fomu ya kugombea urais?( ingawa anasema alikuwa peke yake sijui wewe umetokea wapi!)
 
Acha shobo ushaambiwa hapangiwi kitu na mtu...shobo za nini? yeye ndo anajua kila kitu...
 
Nani alikwambia anapokea huo udaku aliouita wa kwenye mitandao?
Au wewe ulimsindikiza kuchukua fomu ya kugombea urais?( ingawa anasema alikuwa peke yake sijui wewe umetokea wapi!)
Literary aliongea vile kwa sababu maalumu.
Lakini urais wake nilifanya sana kampeni kuhakikisha anashinda na nilifanya kwa moyo mweupe....

Sibebi maneno kama bendera. Situmii udhaifu wake kumtenga bali ntamsaidia hadi dakika ya mwisho ingawa inasemwa hashauriki.

Timiza wajibu
 
Sorry.Ngoja tujifunze kidogo alama : wapi yapaswa kutumika. : hii huwekwa na kufuatiwa maneno ya mtu ili msomaji directly anajua kuwa fulani kasema hivi.
Ukiandika RAIS:.......... Sisi wasomaji tutajua kuwa umeweka maneno ya rais na si yako.
 
Acha shobo ushaambiwa hapangiwi kitu na mtu...shobo za nini? yeye ndo anajua kila kitu...
Ina maana hata ratiba zake za kazi anajipangia mwenyewe?

Siasa hizi hazina tija sana.

Kikubwa tumhukumu kwa kushindwa kuleta maendeleo yenye tija kama alivyoahidi. Ukiacha kumshauri ni haki yako ila ujue yeye ndo mwenye funguo za nchi kwa sasa lazima asilemewe akashindwa kuhold still.

Bashite ni tatizo na kama ameamua kumlinda ni utashi wake ingawa siku zote kwa jirani kuna mjukuu aitwaye majuto
 
Ukweli ni kwamba hawezi kuleta maendeleo yoyote yale sababu hana mpango wowote ule wa maendeleo, ameshasema yeye hapangiwi kitu, hana vision wala mission yoyote ile..
 
Ukweli ni kwamba hawezi kuleta maendeleo yoyote yale sababu hana mpango wowote ule wa maendeleo, ameshasema yeye hapangiwi kitu, hana vision wala mission yoyote ile..
Ilani ipo na anatakiwa kuitekeleza
 
Yeye alishasema hapangiwi... so tumuache hivyo hivyo... mpaka hapo atakapoona maji yamefika shingoni
 
Ilani ipo na anatakiwa kuitekeleza
Acha ubishi usio na tija katika hio ilani kafanya kitu yani? zaidi ya kutaka sifa aonekane kila kitu amafanya yeye? mafanikio ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja maendeleo ni ya watu wote kufanya kazi pamoja sasa mtu anapotaka yeye ndo aonekane anafanya kila kitu wakati kitu hicho chaweza fanywa na mtu wa chini yake lazima ushangae, kwanza ujue mpaka dakika hii anafanya vitu nje ya ilani sidhani kwamba ilani ni kukandamiza upinzani, kutotaka mtu amkosoe, kutengeneza uwanja wa ndege wa kimataifa sehemu ambayo mtu hawezi kwenda, kununua ndege zisizo na tija huyu mtu hana plan yoyote ile...
 
Nani alikwambia anapokea huo ushauri aliouita udaku wa kwenye mitandao?
Au wewe ulimsindikiza kuchukua fomu ya kugombea urais?( ingawa anasema alikuwa peke yake sijui wewe umetokea wapi!)
hhahaahahaaahh, ngushi jamani hahahhahaha
 
..........mafanikio ya nchi hayawezi kuletwa na mtu mmoja maendeleo ni ya watu wote kufanya kazi pamoja sasa mtu anapotaka yeye ndo aonekane anafanya kila kitu wakati kitu hicho chaweza fanywa na mtu wa chini yake lazima ushangae, kwanza ujue mpaka dakika hii anafanya vitu nje ya ilani sidhani kwamba ilani ni kukandamiza upinzani, kutotaka mtu amkosoe, kutengeneza uwanja wa ndege wa kimataifa sehemu ambayo mtu hawezi kwenda, kununua ndege zisizo na tija huyu mtu hana plan yoyote ile...
Nimekuelewa mkuu...
Nini kifanyike? hafanyi kwa ajili yake anatakiwa kuleta tija...
 
Nimekuelewa mkuu...
Nini kifanyike? hafanyi kwa ajili yake anatakiwa kuleta tija...
Mkuu jamaa anafanya vitu kwa ajili yake..vitu nilivyovitaja ukivigeuza utapata nini kifanyike mkuu, kwanza hawezi sikiliza kitu nahisi jamaa alikualia kwenye maisha magumu sana...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom