Rais Samia wanakujaribu, chukua hatua

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,711
Rais Samia Suluhu Hassan, natumaini unapata wasaa wa kupitia pitia mitandaoni kusoma maoni ya sisi watu wako.

Ninakushi endelea na utaratibu huu kwa sababu una manufaa mengi sana kwa Taifa letu na uongozi wako.

Wananchi tunaongea yale tunayoyaona, yanayotusibu na yanayofanyika. Nina hakika wasaidizi wako wanakuletea taarifa nyingi lakini siyo zote.

Mimi ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi, lakini ninaamini kwamba kabla ya CCM kuna Tanzania kwanza. Wewe ni Rais wa Watanzania wote.

Wanaokukubali na wasiokukubali wote wanatambua kwamba wewe ndiye mkuu wa Nchi kwa sasa na hivyo matumaini yetu wote yapo kwenye busara na hekima zako kwenye maongozi ya Taifa hili.

Ninaleta kwako hoja kwa minajili ya kukushauri kuhusu namna hali inavyokwenda kwa kasi na uweze kuangalia wapi pa kuweka mambo sawa.

Kuanzia Jumatatu wiki, tarehe 17/05/2021 Shirika la Umeme Tanesco limekuwa na tatizo la mfumo wake wa LUKU.

Wateja wananunua umeme lakini ni wachache waliofanikiwa kununua, lakini wachache hao umeme unagoma kuingiza kwenye mita zao. Shirika limekaa kimya hakuna taarifa wala maelekezo kwa wateja kuhusu kadhia hiyo.

Shirika lina maafisa wake Uhusiano Jamii kila wilaya lakini hakuna aliyetoa taarifa. Leo Jumatano tarehe 19/05/2021 ndipo Tanesco wametoa taarifa kuwa kuna tatizo la mfumo wa LUKU.

Kama haitoshi wameelekeza wateja wakanunue umeme kwenye ofisi za Mikoa na Wilaya huku wakijua hawakuandaa utaratibu huo na imeleta usumbufu mkubwa kwa Watumiaji umeme.

Lakini walipaswa kutoa maelekezo ya ziada kwamba mtu akinunua umeme anauingizaje maana mita zinagoma kupokea umeme. Mimi nimenunua umeme tangu jumatatu lakini token zimegoma kuingia kwenye mita, na hata niliponunua kwa mtandao mwingine hawajanitumia token zangu hadi leo.

Wiki mbili zilizopita, tulishuhudia Bunge likisimamisha mjadala wa Bajeti kwa saa mbili ili kujadili mkwamo uliojitokeza Bandarini.

Tunashukuru ziara ya Mhe. Waziri Mkuu ilitufungua macho sisi raia wako kwamba kuna taharuki imetengenezwa makusudi ili kuonyesha kwamba serikali yako inakwama. Lakini inaonyesha wazi kuna tatizo kwenye mfumo wa TRA kwani mfumo wake unaelekea kutindikiwa hivyo kukwama mara kwa mara.

Mheshimiwa Rais, changamoto ya kukosa umeme inasababisha mambo mengi kukwama. Nitatoa mifano michache

1. Wapo wagonjwa kwenye hospitali mbalimbali ambao wengine maisha yao kwa sasa yanategemea mitambo ya kuwasaidia kuishi, hivyo kwa siku tatu hospitali zinakuwa zimeelemewa gharama za uendeshaji wa mashine zinazolenga kurefusha uhai wa mgonjwa. Na endapo zinatumia majenereta, hupelekea gharama za matibabu kuwa juu sana. Uwezekano wa kuwa tumepoteza Watanzania wengi kwa kipindi kifupi hiki.

2. Wafanyabiashara kwa asilimia 80% wanategemea umeme kwenye shughuli zao za biashara, hivyo kukosa umeme kunasababisha hasara kubwa sana kwao na hivyo serikali kukosa mapato yake halali. Kwa wale wanaotumia EFD upo uwezekano wakashindwa kuzitumia katika kipindi hiki kwa kisingizio cha umeme kuwa na tatizo la kimfumo

3. Mifumo ya usalama wa maeneo nyeti inategemea umeme, hivyo upo uwezekano kukawa na compromise ya baadhi ya masuala nyeti ya nchi kwa kisa cha Tanesco.
Rais wangu, naomba nikunong’oneze neon moja hapa. Hakuna rais wan chi hii ambaye hajawahi kupingwa, marehemu Baba wa Taifa alipingwa hata kufanyiwa majaribio kadhaa ya kumpindua. Lakini ukimuweka kwenye mizani utaona alitenda mazuri mengi kwa kipindi chake. Hivyo nakusihi usiwe na shaka kwamba hakuna watakaokupinga. Leo umeamua kusimamia serikali inayojali hali za watu na huku ukionyesha dalili zote za kuliunganisha Taifa bila kubagua itikadi, ukabila na hali. Lakini wale waliokuwa wanasimama na wewe kwenye kuinadi ilani ya CCM wameanza kukugeuka na kuendesha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kukupinga wazi wazi.

Wale wanaharakati ambao walisimama kuikosoa Serikali hata wengine kuhatarisha maisha yao (ingawa wapo waliopotea au kupotezwa) lakini leo wanaona unafanya jambo zuri kuifungua nchi ili iweze kuendana na kasi ya dunia kuelekea uchumi wa kati.

Nikukumbushe kwamba hao wanaharakati walio wengi ni Watanzania na walisimama kukosoa mwenendo wa serikali zilizopita kwenye eneo la HAKI. Umeonyesha kwa mguu wa awali kwamba unatamani kuona matabaka ya wenye haki na wasio na haki yanavunjwa. Fahamu kwamba hili jambo halijawafurahisha wengi tena haswaa hao waliokuzunguka.

Wengi wao ndiyo waliokuwa wanasimama hadharani kupindisha na kuvunja haki za binadamu. Wapo ambao umewapa teuzi nyingine lakini ni vyema sana Rais wangu ukatafakari sana haya mambmo kwa kina sana kabla haujafanya maamuzi.

Naomba uniwie radhi kwa uandishi wangu usiokuwa na mpangilio mzuri, lakini ninalazimika kukuandikia kwa sababu hakuna njia nyingine ya kukufikia zaidi ya hii mitandao ya kijamii ambayo umesema wazi unapata wasaa wa kupitia pitia humo. Ninapendekeza yafuatayo uyaangalie kwa jicho la kipekee ili kuiweka nchi yetu kwenye ramani ya mataifa yanayozingatia utu, usawa na ustawi wa watu wake

1. Teua Tume maalumu ya Maridhiano ya Kitaifa ili kupokea maoni ya wananchi na hata kutengeneza Road Map ya muafaka wa kitaifa ili sisi kama raia wako tuweze kupeleka malalamiko yetu ya uvunjivu wa haki za binaadam kwenye tume. Wapatie Tume hiyo uwezo wa kutoa mapendekezo ya msamaha kwa wale watakaokiri kushiriki kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za raia. Tume iweze pia kuandaa hati za mashtaka kwa wale watakaobainika bila shaka kushiriki kwa kiwango kikubwa matendo yaliyohatarisha ama kutoa uhai wa raia nje ya misingi ya kisheria. Tume iweze kutoa elimu kwa Umma kuhusu maridhiano na mshikamano katika kipindi chote cha uhai wa tume

2. Wapo viongozi wetu ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukwapua mali za Umma na kwenda kuficha fedha kwenye benki za siri za nje. Nashauri uangalie namna ya kutengeneza reconciliation with immunity kwao warejeshe sehemu ya fedha hizo na ikiwezekana wawekeze hapa nchini ili watoe ajira kwa vijana wetu lakini fedha hizo wazirejeshe katika awamu au wasamehewe ikiwa itaonekana vyema

3. Bank of Tanzania uiangalie kwa upekee, sheria ya BOT iangaliwe kuiondolea ukiritimba bali iweze kusimamia ukuaji wa uchumi na kuweka securities za mabenki yote nchini bila serikali kutumia akaunti za watu kama njia ya kuwadhibiti na kuwabana. Yaani tuchukue mfumo wa Benki za Switzerland ambapo zimesaidia kutengeneza safe heaven ya wawekezaji wakubwa duniani.

4. Ruhusu vyama vya siasa viweze kufanya shughuli zao za kisiasa nchini. Ni kweli uchaguzi umeisha lakini mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine. Wakiruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa itasaidia kuimarisha demokrasia nchini.

5. Anzisha mchakato wa kurasimisha Wizara hasa kwa kuziweka kwenye Katiba. Inawezekana kwa kila rais anayeingia kuwa na mtazamo wake namna anavyoona serikali iweje. Lakini kuwepo na mtazamo wa kitaifa ambao unatoa mwelekeo wa kisekta na ukamilifu wa Taasisi za kidemokrasia na utawala kupitia Katiba ya Nchi. Rais awe na mamlaka ya kuanzisha na kuondoa Idara ndani ya Wizara lakini Muundo wa Wizara usitegemee instruments bali mwongozo wa Katiba. Tujue idadi ya Wizara na sharia zinazohusu kila Wizara zitokane na Vifungu vya Katiba kuhusu Wizara husika. Hii itapunguza gharama za uendeshaji lakini kuwa na uwajibikaji mkubwa kwenye serikali.

Naweka mfano hapa

A. Ofisi ya Makamu wa Rais
B. Ofisi ya Waziri Mkuu
C. Wizara ya Ulinzi
D. Wizara ya Fedha na Uchumi
E. Wizara ya Afya
F. Wizara ya Ustawi wa Jamii (Sanaa, Utamaduni na Michezo_)
G. Wizara ya……….
H. ………………

Naamini Roma haikujengwa kwa usiku mmoja, lakini kuna siku waliamua kuanza kujenga na hatimaye ilikuwepo siku waliyokamilisha hatia kubwa za ujenzi. Rais wangu Samia Suluhu Hassan, sisi tuna imani nawe ingawa kuna dalili zote za kukukwamisha zinazofanywa na walio karibu yako. Wewe ni Mwanadiplomasia Namba Moja, hivyo unajua nini cha kufanya na nini cha kupuuzia.

Mwandishi ni Mwanachama Hai wa CCM
 
Kwenye maridhiano ya kitaifa umechemka.

maridhiano na nani? Au unawapigia debe wale jamaa wawili,waliokwenda kutafuta maisha Ughaibuni?

si warudi tu nyumbani maana si walimkimbia mwendezake na sasa hayupo?

Hakuna mkwamo wowote nchini,ila kakundi kanakotaka kenyewe kaangaliwe special kuliko watanzania wengine.

Rais achana na watu wenye ubinafsi,kama yule bwana anataka kuhakikishiwa usalama,ila aliposikia kuna kugombea urais alikuja mbio bila kujali usalama wake mwenyewe.

Mpaka akasahau kuvaa barakoa alipokuwa TZ,alikumbuka alipopanda ndege kurejea kwake kula maisha.

pengine ulipochemka ni kujiita wewe ni CCM, au umekosea ulimaanisha wewe ni CHADEMA umekuja kivingine.
 
Nadhani kwa kifupi tu ungemshauri Rais Samia kitu anachokifahumu; pengine kumkumbusha tu kuwa amalizie kile kiporo cha KATIBA na mambo yote yatatengemaa.
 
Mnavyosema maridhiano ya kitaifa mnamfananisha nini? Mbona huku mtaani tunaishi vizuri tu?
 
Rais Samia Suluhu Hassan, natumaini unapata wasaa wa kupitia pitia mitandaoni kusoma maoni ya sisi watu wako.

Ninakushi endelea na utaratibu huu kwa sababu una manufaa mengi sana kwa Taifa letu na uongozi wako.

Wananchi tunaongea yale tunayoyaona, yanayotusibu na yanayofanyika. Nina hakika wasaidizi wako wanakuletea taarifa nyingi lakini siyo zote.

Mimi ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi, lakini ninaamini kwamba kabla ya CCM kuna Tanzania kwanza. Wewe ni Rais wa Watanzania wote.

Wanaokukubali na wasiokukubali wote wanatambua kwamba wewe ndiye mkuu wa Nchi kwa sasa na hivyo matumaini yetu wote yapo kwenye busara na hekima zako kwenye maongozi ya Taifa hili.

Ninaleta kwako hoja kwa minajili ya kukushauri kuhusu namna hali inavyokwenda kwa kasi na uweze kuangalia wapi pa kuweka mambo sawa.

Kuanzia Jumatatu wiki, tarehe 17/05/2021 Shirika la Umeme Tanesco limekuwa na tatizo la mfumo wake wa LUKU.

Wateja wananunua umeme lakini ni wachache waliofanikiwa kununua, lakini wachache hao umeme unagoma kuingiza kwenye mita zao. Shirika limekaa kimya hakuna taarifa wala maelekezo kwa wateja kuhusu kadhia hiyo.

Shirika lina maafisa wake Uhusiano Jamii kila wilaya lakini hakuna aliyetoa taarifa. Leo Jumatano tarehe 19/05/2021 ndipo Tanesco wametoa taarifa kuwa kuna tatizo la mfumo wa LUKU.

Kama haitoshi wameelekeza wateja wakanunue umeme kwenye ofisi za Mikoa na Wilaya huku wakijua hawakuandaa utaratibu huo na imeleta usumbufu mkubwa kwa Watumiaji umeme.

Lakini walipaswa kutoa maelekezo ya ziada kwamba mtu akinunua umeme anauingizaje maana mita zinagoma kupokea umeme. Mimi nimenunua umeme tangu jumatatu lakini token zimegoma kuingia kwenye mita, na hata niliponunua kwa mtandao mwingine hawajanitumia token zangu hadi leo.

Wiki mbili zilizopita, tulishuhudia Bunge likisimamisha mjadala wa Bajeti kwa saa mbili ili kujadili mkwamo uliojitokeza Bandarini.

Tunashukuru ziara ya Mhe. Waziri Mkuu ilitufungua macho sisi raia wako kwamba kuna taharuki imetengenezwa makusudi ili kuonyesha kwamba serikali yako inakwama. Lakini inaonyesha wazi kuna tatizo kwenye mfumo wa TRA kwani mfumo wake unaelekea kutindikiwa hivyo kukwama mara kwa mara.

Mheshimiwa Rais, changamoto ya kukosa umeme inasababisha mambo mengi kukwama. Nitatoa mifano michache

1. Wapo wagonjwa kwenye hospitali mbalimbali ambao wengine maisha yao kwa sasa yanategemea mitambo ya kuwasaidia kuishi, hivyo kwa siku tatu hospitali zinakuwa zimeelemewa gharama za uendeshaji wa mashine zinazolenga kurefusha uhai wa mgonjwa. Na endapo zinatumia majenereta, hupelekea gharama za matibabu kuwa juu sana. Uwezekano wa kuwa tumepoteza Watanzania wengi kwa kipindi kifupi hiki.

2. Wafanyabiashara kwa asilimia 80% wanategemea umeme kwenye shughuli zao za biashara, hivyo kukosa umeme kunasababisha hasara kubwa sana kwao na hivyo serikali kukosa mapato yake halali. Kwa wale wanaotumia EFD upo uwezekano wakashindwa kuzitumia katika kipindi hiki kwa kisingizio cha umeme kuwa na tatizo la kimfumo

3. Mifumo ya usalama wa maeneo nyeti inategemea umeme, hivyo upo uwezekano kukawa na compromise ya baadhi ya masuala nyeti ya nchi kwa kisa cha Tanesco.
Rais wangu, naomba nikunong’oneze neon moja hapa. Hakuna rais wan chi hii ambaye hajawahi kupingwa, marehemu Baba wa Taifa alipingwa hata kufanyiwa majaribio kadhaa ya kumpindua. Lakini ukimuweka kwenye mizani utaona alitenda mazuri mengi kwa kipindi chake. Hivyo nakusihi usiwe na shaka kwamba hakuna watakaokupinga. Leo umeamua kusimamia serikali inayojali hali za watu na huku ukionyesha dalili zote za kuliunganisha Taifa bila kubagua itikadi, ukabila na hali. Lakini wale waliokuwa wanasimama na wewe kwenye kuinadi ilani ya CCM wameanza kukugeuka na kuendesha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kukupinga wazi wazi.

Wale wanaharakati ambao walisimama kuikosoa Serikali hata wengine kuhatarisha maisha yao (ingawa wapo waliopotea au kupotezwa) lakini leo wanaona unafanya jambo zuri kuifungua nchi ili iweze kuendana na kasi ya dunia kuelekea uchumi wa kati.

Nikukumbushe kwamba hao wanaharakati walio wengi ni Watanzania na walisimama kukosoa mwenendo wa serikali zilizopita kwenye eneo la HAKI. Umeonyesha kwa mguu wa awali kwamba unatamani kuona matabaka ya wenye haki na wasio na haki yanavunjwa. Fahamu kwamba hili jambo halijawafurahisha wengi tena haswaa hao waliokuzunguka.

Wengi wao ndiyo waliokuwa wanasimama hadharani kupindisha na kuvunja haki za binadamu. Wapo ambao umewapa teuzi nyingine lakini ni vyema sana Rais wangu ukatafakari sana haya mambmo kwa kina sana kabla haujafanya maamuzi.

Naomba uniwie radhi kwa uandishi wangu usiokuwa na mpangilio mzuri, lakini ninalazimika kukuandikia kwa sababu hakuna njia nyingine ya kukufikia zaidi ya hii mitandao ya kijamii ambayo umesema wazi unapata wasaa wa kupitia pitia humo. Ninapendekeza yafuatayo uyaangalie kwa jicho la kipekee ili kuiweka nchi yetu kwenye ramani ya mataifa yanayozingatia utu, usawa na ustawi wa watu wake

1. Teua Tume maalumu ya Maridhiano ya Kitaifa ili kupokea maoni ya wananchi na hata kutengeneza Road Map ya muafaka wa kitaifa ili sisi kama raia wako tuweze kupeleka malalamiko yetu ya uvunjivu wa haki za binaadam kwenye tume. Wapatie Tume hiyo uwezo wa kutoa mapendekezo ya msamaha kwa wale watakaokiri kushiriki kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za raia. Tume iweze pia kuandaa hati za mashtaka kwa wale watakaobainika bila shaka kushiriki kwa kiwango kikubwa matendo yaliyohatarisha ama kutoa uhai wa raia nje ya misingi ya kisheria. Tume iweze kutoa elimu kwa Umma kuhusu maridhiano na mshikamano katika kipindi chote cha uhai wa tume

2. Wapo viongozi wetu ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine kukwapua mali za Umma na kwenda kuficha fedha kwenye benki za siri za nje. Nashauri uangalie namna ya kutengeneza reconciliation with immunity kwao warejeshe sehemu ya fedha hizo na ikiwezekana wawekeze hapa nchini ili watoe ajira kwa vijana wetu lakini fedha hizo wazirejeshe katika awamu au wasamehewe ikiwa itaonekana vyema

3. Bank of Tanzania uiangalie kwa upekee, sheria ya BOT iangaliwe kuiondolea ukiritimba bali iweze kusimamia ukuaji wa uchumi na kuweka securities za mabenki yote nchini bila serikali kutumia akaunti za watu kama njia ya kuwadhibiti na kuwabana. Yaani tuchukue mfumo wa Benki za Switzerland ambapo zimesaidia kutengeneza safe heaven ya wawekezaji wakubwa duniani.

4. Ruhusu vyama vya siasa viweze kufanya shughuli zao za kisiasa nchini. Ni kweli uchaguzi umeisha lakini mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine. Wakiruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa itasaidia kuimarisha demokrasia nchini.

5. Anzisha mchakato wa kurasimisha Wizara hasa kwa kuziweka kwenye Katiba. Inawezekana kwa kila rais anayeingia kuwa na mtazamo wake namna anavyoona serikali iweje. Lakini kuwepo na mtazamo wa kitaifa ambao unatoa mwelekeo wa kisekta na ukamilifu wa Taasisi za kidemokrasia na utawala kupitia Katiba ya Nchi. Rais awe na mamlaka ya kuanzisha na kuondoa Idara ndani ya Wizara lakini Muundo wa Wizara usitegemee instruments bali mwongozo wa Katiba. Tujue idadi ya Wizara na sharia zinazohusu kila Wizara zitokane na Vifungu vya Katiba kuhusu Wizara husika. Hii itapunguza gharama za uendeshaji lakini kuwa na uwajibikaji mkubwa kwenye serikali.

Naweka mfano hapa

A. Ofisi ya Makamu wa Rais
B. Ofisi ya Waziri Mkuu
C. Wizara ya Ulinzi
D. Wizara ya Fedha na Uchumi
E. Wizara ya Afya
F. Wizara ya Ustawi wa Jamii (Sanaa, Utamaduni na Michezo_)
G. Wizara ya……….
H. ………………

Naamini Roma haikujengwa kwa usiku mmoja, lakini kuna siku waliamua kuanza kujenga na hatimaye ilikuwepo siku waliyokamilisha hatia kubwa za ujenzi. Rais wangu Samia Suluhu Hassan, sisi tuna imani nawe ingawa kuna dalili zote za kukukwamisha zinazofanywa na walio karibu yako. Wewe ni Mwanadiplomasia Namba Moja, hivyo unajua nini cha kufanya na nini cha kupuuzia.

Mwandishi ni Mwanachama Hai wa CCM
Mfumo CCM ndio tatizo la nchi hii.
 
Mkuu uliandika kwa msisitizo zaidi:

#1. "Mwandishi ni Mwanachama Hai wa CCM."

#2. "Mimi ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi, ..."

Kama ni hivi wa ACT-wazalendo naye akihitaji kuandika lake si itakuwa shughuli?

😂😂😂😂😂!

Hiiiiii bagosha!
 
Back
Top Bottom