Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 980
- 3,646
Rais Samia, amesema kwamba licha ya hali tete inayoikumba dunia kwa sasa, Tanzania inafanya vizuri kwa viwango vya kuvutia kiuchumi. Akiwahutubia wananchi wa Simiyu katika ziara yake ya kikazi, Rais Samia alieleza kwa msisitizo hali halisi ya ulimwengu na nafasi ya Tanzania ndani yake:
'Ukitegemea msaada wale wanaotoa msaada dunia yote sasa ipo juu chini. Mavita, maugomvi, mavurugu, chumi zimeshuka, huko hawafanyi vizuri kama tunavyofanya sisi.''
Katika kauli hiyo, Rais Samia aliweka bayana kuwa hata mataifa makubwa yanayojulikana kwa nguvu zao za kiuchumi hayako tena katika nafasi ya kuigwa kwa sasa
''Ulaya na Marekani sasa hivi hawafanyi vizuri kiuchumi kama tunavyofanya sisi huku, hata ndani ya kanda yetu hii ya Afrika Mashariki, Tanzania tunafanya vizuri.”