Jesusie
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 1,525
- 784
Dar es Salaam, Tanzania – Bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka Sh. bilioni 294 mwaka 2021 hadi kufikia Sh. trilioni 1.242 mwaka 2025, ongezeko la Sh. bilioni 948 sawa na ongezeko la 322%. Ongezeko hili linaonyesha juhudi za Serikali kuimarisha sekta ya kilimo na kuhakikisha wakulima wanapata rasilimali za kutosha.
Aidha, upatikanaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 678,017 mwaka 2021 hadi tani 1,213,780 mwaka 2024, huku Serikali ikitoa ruzuku ya Sh. bilioni 708.6, hatua inayolenga kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija katika kilimo.