Na Emmanuel J. Shilatu
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wanawake wote, heri ya siku ya Mwanamke! Tunaadhimisha siku ya Mwanamke tukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (SSH), Mwanamke kiongozi wa kipekee Tanzania.
Unapozungumzia Rais Samia unamzungumzia Mwanamke mvumilivu sana ambaye kama ilivyo kwa Wanawake wengine kupiga hatua wanakumbana na changamoto nyingi na kubwa lakini Rais Samia aliweza kuzivumilia na hatimaye leo ni kiongozi mkubwa nchini Tanzania.
Unapozungumzia Rais Samia unamzungumzia Mwanamke hodari na shupavu katika kuleta maendeleo ya kweli nchini na leo hii tunaona mageuzi makubwa yakifanyika kwenye nyanja zote za kimaisha iwe kisiasa, kiuchumi, kijamii nk. Mfano hai ni ujenzi wa Madarasa 15,000 nchi nzima kwa muda mfupi tangu awe Rais wa Tanzania.
Rais Samia amedhihirisha si kelele za Watu, maumbile yake Mwanamke, ama vikwazo vyovyote vile vinaweza kumrudisha nyuma ama kushindwa kuwaletea maendeleo Watanzania na Taifa la Tanzania. Hakika Rais Samia ni Mwanamke jasiri na mchapa kazi.
Ni kawaida kwa Wanawake kutokupendana na kuwa na tabia ya kurudishana nyuma kimaendeleo lakini hali hiyo ni tofauti kabisa kwa Rais Samia ambaye nyakati zote ameonekana Mtu wa kuwainua sana Wanawake nchini akihakikisha malengo ya 50/50 anayafikia kwenye uongozi wake.
Sio tu kitaifa bali hata kimataifa wanamtambua Rais Samia Suluhu Hassan kama kiongozi Mwanadiplomasia, mtiifu, mpenda mahusiano, msuluhishi, mpenda maendeleo mwenye kuamini katika ushirikiano wa kweli baina ya Tanzania na nchi nyinginezo Dunia.
Rais Samia anaposema twende Pamoja anamaanisha kivitendo, kwa matokeo ya haraka.
Hakika Rais Samia Suluhu Hassan ni super Woman! Heri ya siku ya Wanawake Duniani 2022.
Shilatu, E.J