Rais Samia Suluhu na kauli ya 'Mimi na Magufuli ni kitu kimoja'

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Amani iwe nanyi.

Kuna kauli mbalimbali ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu Hassan zilizopelekea watanzania kuwa wamoja zaidi na kuifanya nchi kutulia mara baada ya msiba mzito wa kuondokewa na rais Magufuli.

Binafsi ninazo kauli mbili ,kama na wewe unazo weka hapa

1. Mimi na Magufuli ni kitu kimoja.
Ikumbukwe mara baada ya kufariki rais Magufuli liliibuka kundi likiongozwa na Tundu Lissu na Lema likawa linashangilia kifo hicho, hali hiyo ilienea hadi kwa baadhi ya wabunge kama Nape na Makamba, badala ya kujadili bajeti wakawa wanajadili nani ni zaidi kati ya Magufuli na Samia.!

Hali hiyo iliwakera sana wazalendo wa nchi yetu na rasmi likaibuka kundi jingine lililobatizwa jina la walinda legacy ya Magufuli, moja ya watu wa kundi hili waliojitokeza hadharani kukemea ni mbunge Lusinde ,pia Lazaro Nyalandu aliyekuwa kada wa CHADEMA alikemea hadharani na kutangaza kuachana na Chadema kwa kitendo chao cha kumtukana alipohudhuria msiba Chato.

Katikati ya mvurugano huo aliibuka rais Samia na kuwachana live Wabunge na Chadema kwa ujumla kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja na serikali yake ya awamu ya sita haijatokana na uchaguzi mbali imetokana yeye Samia kuaminiwa na hayati Magufuli na kufanywa kuwa makamu wa Rais.

Kauli hii ya Samia ililifanya kundi la walinda Legacy kuibuka kidedea dhidi ya kundi la washangilia kifo hivyo nchi kutulia.

2. Wala rushwa ,wazembe majambazi na mafisadi kuendelea kubanwa.
Rais Samia alitangaza hadharani kwamba katika masuala ya rushwa atasimama imara na akamtumbua mkurugenzi wa bandari na kuagiza Takukuru wafanye uchunguzi BOT na wizara ya fedha.

Pia kuwajibisha wote waliojaribu kuchezea mifumo ya Tanesco ,TRA na bandari.

Hatua hizi zilifanya nchi kutulia kwa sababu watanzania wengi waliona rasilimali zao bado ziko salama kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano chini ya hayati Magufuli.
 
Hiviii Mama anakosea Wapi? Wale wale Wanaomsifia Anaupiga Mwingi....Ndo wale Wale wanaotaka Maandamano Japo Ameshaomba apewe Muda ajenge Nchi Kwa kuwa Issue Ya KATIBA Ya 'Wananchi' inazungumzika...!

Tujiulize Watu Waliufyata Kabisa Kwa takribani Miaka 6.Sasa Ghafla Mama kaja Wanamsifu , mara Wanamtisha eti Maandamano...! Sisi wa chini mashinani mnatuchosa.

Sasa Semeni moja TUMSIFIE AU TUMNANGE.
 
Aisee Kumbe Mbowe na kundi lake walikuwa watu hatari kiasi hiki!

yaani ni zaidi ya Majambazi, yaaani wanapanga njama za kuuuwa watu! duh! aisee hawa watu hawafai kabisaaa!! sio binaadamu.
 
Back
Top Bottom