Rais Samia Suluhu akumbuka mchango wa mzee Waikela katika harakati za kudai uhuru

Malick Ayoub

Member
May 25, 2022
10
4
MWENYEKITI WA CCM NDUGU SAMIA SULUHU HASSAN AKUMBUKA MCHANGO WA MZEE WAIKELA KATIKA HARAKATI ZA KUDAI UHURU

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka ameungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mmoja miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za uhuru wa Tanganyika Mzee Rehani Bilal Waikela aliyefariki dunia Jumapili 07 Julai 2022 jijini Dar Es Saalam.

Akizungumza katika ibada ya sala ya maiti iliyofanyika msikiti wa Kichangani Magomeni amesema Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtaja Mzee Waikela kuwa mzalendo, jasiri mwenye uthubutu na mtu aliyejitolea kwa hali na mali katika kupigania Uhuru wa Tanganyika.

”Tumempoteza miongoni mwa waliokuwa mstari wa mbele katika kufanikisha uhuru wa Tangayika kwa sababu alikuwa jasiri, mzalendo mwenye uthubutu na utayari wa kujitolea nguvu na rasilimali zake wakati wa mapambano ya kutafuta uhuru, mchango wake ni mkubwa ambao chama na serikali tunauthamini na tutaukumbuka” Ndugu Samia Suluhu Hassan

Shaka aliwasilisha salam za pole za Chama Cha Mapinduzi kwa familia ndugu, jamaa, marafiki na kuwaomba kuwa wavumilivu na wenye subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Mzee Rehani Bilali Mwaikela amezikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam ambapo mbali na wanafamilia, ndugu na jamaa walihudhuria pia viongozi mbalimbali wa kisiasa pamoja na wanazuoni mashuhuri.

Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea
IMG-20220707-WA0153.jpg
IMG-20220707-WA0152.jpg
IMG-20220707-WA0148.jpg
IMG-20220707-WA0151.jpg
 
Back
Top Bottom