Rais Samia: Nimefanya Movie nyingine na Mwigizaji wa Kichina inaitwa "Kijiji Cha Milele" itatoka hivi karibuni

Si kaishapata kazi aache ofisi ya pale kivukoni, tumpe mwingine, tuna matatizo ya ajira nchi hii.
 
Hii lugha ya kisanii ya kufanya "movie" ilianzia kwa wasanii uchwara wa bongo, ilianza kusikika kwenye miaka ya tisini mwanzoni. Kuna dada mmoja enzi hizo aliamini kuwa ukiwa na kipaji hupaswi kupoteza muda kusoma....

Alikuja baadaye kuingia kwenye mtandao wa wasanii wa bongo kama Babalevo, Steve Nyerere na Mwijaku ingawa sasa ni RIP.

Inasikitisha sana kuona Rais wa nchi badala ya kufanya majukumu muhimu ya kitaifa tuliyomtuma anawaza kutengeneza "Movie" ... Wasanii wamekuwa watawala wakati mtawala amegeuka msanii....Du!!😭
 
Weka Assessment Report ya Royal Tour tuone kama ilizaa matunda.
Egypt wanapokea watalii zaidi ya Milioni 20 kwa mwaka ila hatujawai kumuona Rais wao anacheza movie,yeye huu upuuzi kautoa wapi!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Utalii wa Egypt haujaanza Leo ni WA kihistoria tangu kuumbwa Kwa Dunia na Wala hautegemei kenge kama WA kwenu.

Umaarufu wa Egypt ni mkubwa Dunia nzima hawahitaji kujitangaz ila Tzn ni lazima hamuna mtu anaijua.

Kwa hiyo punguza ujinga wa kufananisha visivyofanana.

Mwisho analysis zimewekwa mara nyingi tuu Kwa mfano baada ya Royal tour idadi ya Wamarekani wanaotembelea Tanzania imeongezeka.
 
Back
Top Bottom