Rais Samia ni komandoo aliyeiva

Na wewe umekuwa na hulka za kubweka ili kufurahisha bwana anaekumiliki. Kusifu, kupamba viongozi ndicho ulichobakiza kwako.

Toa kasoro pia, kosoa ili kubainisha mapungufu yarekebishwe kukuza ubora wa maisha ya wananchi. Lakini wewe ni mapambio kwa watawala mwisho unaweka na namba ya simu ili ulipwe fadhila za upambe.

Hapa ndipo CCM ilipotufikisha kwa kuzalisha wasifiaji machawa na majibwa, mtabweka ili msikiwe lakini hakuna hoja za ujenzi wa taifa
 
Sasa namba ya simu ya nini chawa wewe?
 
Kama Kuna mahali umeona kasoro ni uamuzi wako kukosoa kwa staha na hoja zenye uthibitisho ,lakini Mimi nampongeza kwa kuwa naona mengi na mazuri yanayofanywa na kutekelezwa na serikali ya mh Rais mama Samia katika juhudi zake za dhati katika kuinua maisha ya watanzania na kuleta maisha Bora kwa kila mtanzania.

Hata katika changamoto ninaona nna mh Rais anavyopambana katika kuzitatua na kuzimaliza ili kuleta nuru katika maisha ya watanzania,ninaona ushapu wa mh Rais na serikali yake katika kushughulika na kero za watu,ndio maana kwa moyo mkunjufu,upendo na uzalendo mkubwa Sana kwa Taifa langu ninampongeza kwa dhati ya moyo wangu mh Rais kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu.
 
Huna lolote wewe ni jibwa unabweka kumfurahisha bosi
 
Wahenga walisema TUMBO MPONZA TAko
 
Hata Rais Samia akisoma hili bandiko lazima acheke moyoni kimya kimya huku akimtafakari huyu kijana.
 
Hoja zako hazina nia mbaya kwa Rais wetu tatizo ni kwamba unatumia mhemko wa kihisia zaidi kuliko akili, kwa nia na malengo binafsi uyajuayo wewe.
 
Machawa bwana hata mbuzi meee akiwa raisi leo yatasifia mpaka mate yawakauke. Sasa eti Sa100 ni komandoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…