Rais Samia ni komandoo aliyeiva

Ni ukweli wa kichawa zaidi.
Ni ukweli juu ya kazi kubwa na ya kutukuka aliyoifanya ndani ya muda mfupi mh Rais wetu shupavu na madhubuti,mzalendo wa kweli,Jasiri,Hodari ,sauti ya Afrika, mtetezi wa Afrika na waafrika wote mh Rais mama Samia suluhu Hassani.
 
Komando wa mchongo asiye na mafunzo kwenye uwanja wa Vita . Vasco da gama
 
Chawa wa mama
Mimi Ni msema kweli, sihitaji na Wala sipendi kuuficha ukweli,kiongozi akifanya vyema Ni lazima watanzania Tuwe na utamaduni wa kupongeza na kumtia moyo na faraja mhusika. Tusipende kuwakatisha Tamaa viongozi aina ya Rais Samia walio jitoa na kujitolea maisha Yao Kama sadaka kwa ajili ya kuwasaidia na kuwatumikia watanzania kwa moyo wa upendo, unyenyekevu na uzalendo wa usiopimika katika kuona kila mmoja wetu Ni mwenye Tabasamu,furaha na matumaini katika moyo na paji lake la uso wake
 
Kwa hiyo naye ni kama wale wanaofanya maonesho siku za sikuu za kitaifa siyo?
 
Acheni uchawa watoto wa kiume, biblia yenyewe imesema mwanaume ale kwa jasho, sawa Lucas?
Ndio hata Mimi nakula kwa jasho langu,nakula baada ya kufanya kazi kwa kutumia mikono yangu pasipo kumnyonya mtu kwa Aina yoyote Ile,nawajibika juu ya kupata chakula changu.huo Ni wajibu wangu ninao utimiza kwa uaminifu na kujituma kwa bidii,juhudi na maarifa
 
Machawa wajengewe uwezo

 
Kila siku unavyoleta ngonjera umeridhika na huduma Zinazotolewa na serikali?
 
Serikali watu hawa wachache akina Lucas wekeni utaratibu wa kuwaunga mkono muwatie moyo
 
Kila siku unavyoleta ngonjera umeridhika na huduma Zinazotolewa na serikali?
Ndio nimeridhika na huduma zinazotolewa na serikali yangu , nimeona pia juhudi zake katika kukabiliana na changamoto na kero zinazokuwa zinajitokeza,Ikumbukwe kuwa changamoto huwa hazikosekani hivyo kinachoangaliwa Ni namna gani na vipi serikali inavyochukua hatua katika kuzitatua. Serikali ya Rais Samia imeonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa Sana katika kukabiliana na changamoto na kusogeza huduma karibu ya mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…