888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 445
- 553
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Kwa heshima na taadhima, nakuandikia kwa sauti ya wananchi si kwa ghadhabu, si kwa jazba, bali kwa uchovu wa matumaini na kilio cha mabadiliko yanayocheleweshwa.
Tulikukaribisha kwa matumaini makubwa. Ulikuja na sauti ya upole, ukatutangazia “kazi iendelee”, ukahimiza majadiliano na maridhiano. Ulipokea taifa lililokuwa limevunjika kiroho, watu wake wakiwa wamegawanyika kwa hofu, lakini pia kwa matumaini kwamba labda mama angeleta huruma.
Lakini miaka inavyosonga mbele, wananchi wengi wanajiuliza:
Naiona Tanzania ikiendeshwa kwa propaganda zaidi ya sera. Tumeona viongozi wa dini wakinyamazishwa, waandishi wakitishwa, wananchi wakipotea. Tumeona chama tawala kikirudi kwenye hulka ya ubabe, wakati taifa linahitaji fikra mpya.
Mama, historia itakuhukumu si kwa muda uliokaa madarakani, bali kwa alama uliyoacha. Na kama hali hii itaendelea, basi tutaweka kumbukumbu kuwa tulikuwa na nafasi ya mabadiliko—lakini ikapotea kwa sababu ya hofu ya kuachia.
Nashauri Kwa Upendo na Uzalendo:
Mama, kama dhamira ya kuleta mabadiliko ya kweli haipo tena, kama kushikilia madaraka kumechukua nafasi ya kusikia sauti ya wananchi, basi huenda muda umefika wa wewe kuachia madaraka kwa heshima, kwa hiari, na kwa historia.
Kwa kufanya hivyo:
Utakuwa Rais wa kwanza kuonyesha kuwa madaraka si urithi, ni dhamana.
Utalinda jina lako kuliko kuwa sehemu ya kuandika historia ya kulia.
Utatuachia nafasi ya kuanza upya kama taifa linalojifunza na kujirekebisha.
Uongozi wa heshima si ule wa kubaki madarakani hadi ushindwe, ni ule wa kusikia sauti kabla ya kelele.
Kwa heshima,
Kwa upendo,
Kwa sauti ya kizazi kinachoamka.
✍🏾

- Yale matumaini ya katiba mpya yako wapi?
- Kwa nini mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hayawekwi wazi wala kupewa uzito wa kitaifa?
- Kwa nini vyombo vya dola vinaendelea kukandamiza sauti za wananchi, makanisani, mitaani, hata bungeni?
- Na kwanini serikali yako inajibu hoja kwa kejeli badala ya kujenga hoja mbadala?