Rais Samia kuhutubia dunia kupitia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
🔥 NI LEO! RAIS SAMIA KUHUTUBIA DUNIA KUPITIA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA 🔥.


Mabibi na Mabwana, leo Alhamisi Septemba 23, 2021 kuanzia saa 3 usiku majira ya Afrika Mashariki, Mwanamke wa shoka Rais Samia Suluhu Hassan atahutubia dunia kupitia Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) Jijini New York, Marekani. Rais Samia atahutubia Baraza hilo lenye Wakuu wa nchi, Serikali na Wakubwa wote wa dunia baada ya kupita miaka 6 bila Mkuu wa nchi ya Tanzania kuhudhuria Baraza hilo muhimu sana kwa uchumi, uwekezaji, biashara na maendeleo ya Taifa letu.

Kitendo tu cha Rais Samia ambaye ametajwa na Jarida la Avance Media la nchini Ghana kuwa moja ya Wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika na dunia kwa ujumla kushiriki Mkutano huo kunamuwezesha kukutana na Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa wa dunia, Wakuu wa taasisi kubwa za kifedha ulimwenguni kama Benki ya Dunia (WB), Shirika la Biashara duniani (WTO) na wengine wengi na moja kwa moja kuwezesha kushusha uwekezaji mkubwa wa biashara na utalii nchini ambao utatoa ajira kwa Watanzania na kuimarisha uchumi wetu maradufu. Nani Kama Mama Samia?

â–  Marais wa Tanzania waliowahi kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Leo Alhamisi September 23 kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. #UNGA

IMG-20210923-WA0009.jpg
 
Tutamsikiliza maana naamini TBC na channel za ndani watajitahidi wairushe live
 
TBC Redio na Televisheni watuonyeshee live Madame President akihutubia ili tumuone na tufahamu atakachoongea. Taifa linasubiri kwa hamu.
 
Anahutubia au anasoma ?

Wataalamu wanao muandikia cha kusoma kwenye hotuba yake wasisahau kuweka aya ya kujibu dongo la Biden. Akumbushwe ajue jinsi wakati mwengine USA na washirika wake wanavyotumia mifumo ya demokrasia vyama vingi kama kisingizio cha kuingulia soverenity ya mataifa mengi kinyume na maazimio ya UNO. Kwa vile mlengwa ni Biden waseme kabisa Democracy is not like some Pepsicola.
 
Back
Top Bottom