Rais Samia huu mkakati wako au wasaidizi wako dhidi ya Kanisa Katoliki (TEC) unatuangusha sana tunaokutetea na kutukanwa Mitandaoni

Rais Samia huu mkakati wako au wasaidizi wako dhidi ya Kanisa Katoliki (TEC) unatuangusha sana tunaokutetea na kutukanwa Mitandaoni

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,006
Reaction score
126,388
Mama (Rais Samia) unataka nikushauri vipi na mara ngapi kuhusu Kanisa Katoliki ambalo Mimi GENTAMYCINE pia ni Muumini tukuka wa hilo Dhehebu na wala sina mpango wa Kuacha kuwa Mkatoliki? Rais Samia hivi unajua kuwa kupambana na Kanisa Katoliki kunahitaji Akili Kubwa ambazo kwa bahati mbaya sana hawa so called Strategists na Spin Doctors wako hawana na kamwe hawatakuwa nayo?

Rais Samia (Mama) hivi unajua kuwa Mizizi ya Kanisa Katoliki ilianza kusimikwa Tanzania hii tokea enzi na enzi na kwamba kwa Wewe sasa kuhangaika nao / kupambana nao ndiyo unajiharibia zaidi na huenda hata ukawa unajihatarishia ustawi wako wewe mwenyewe?

Mama (Rais Samia) kuna tatizo gani kwa Wewe kiungwana na kiustaarabu tu ukawaita Viongozi wa TEC Ikulu na Kuzungumza nao huku ukiwapa Sikio lako kama Kiongozi wa nchi na uwasikilize? Rais Samia wengine akina GENTAMYCINE tuliamua KUJILIPUA kwa kujitolea Kukutetea kwa Dhambi ulizoponzwa na Washauri wako wabaya tukidhani utatumia huo muda Kujitafakari, Kujitathmini na Kujirekebisha na Maslahi ya Tanzania yetu.

Rais Samia (Mama) kwa utafiti wangu mdogo tu na usio rasmi nimegundua kuwa tokea uanze Kupambana na Wakatoliki (TEC) ndiyo unaharibu zaidi badala ya Kujenga. Hivi Rais Samia unajua kuwa hata hawa Waislamu wenzako Wasomi wengi nchini Tanzania (akiwemo Mshauri wako Rais Mstaafu Kikwete) wamepata Elimu nzuri ya Kikatoliki kupitia Shule / Taasisi zao?

Hivi Rais Samia (Mama) unajua kuwa 99% ya hawa Watu wako (Strategists na Spin Doctors) wanaopambana Kijinga (Kingumbaru) na Kipumbavu (Kipopoma) na Kanisa Katoliki, Wakatoliki Tanzania na hasa TEC wanafanya hivyo ili tu wale hizo Fedha zako ila ukweli wa Mioyoni mwao wanajua hawawezi Wakatoliki / TEC?

Na Rais Samia (Mama) sijui kwanini umeshindwa pia kutambua kuwa hata tu 65% ya Watumishi wako Serikalini hadi katika Idara zako Nyeti za Kitaasisi ni Wakatoliki hivyo haya Mapambano yako nao pia ni kama vile unalazimisha Uadui kutoka ndani Kwako kitu ambacho GENTAMYCINE nakiona ni HATARI Kwako na kwa Nchi pia.

Rais Samia (Mama) hii kampeni yako dhidi ya TEC na Wakatoliki Tanzania (ambayo umeponzwa kwa Kushauriwa vibaya) na Wanaokuzunguka nikuhakikishie kwa 100% kuwa haitofanikiwa sana sana ndiyo unawalazimisha sasa Wakatoliki watumie Akili zao Kubwa walizobarikiwa kupunguza Ufanisi wako wa Kiuongozi.

Rais Samia (Mama) kwa sasa Mwanao GENTAMYCINE nakushauri rudisha Imani ya Watanzania Kwako na Serikali yako, Tubu pale ambapo ama Umekosea au Umewakosea Watanzania, Imarisha ule Umoja wetu, badilisha Washauri wako, Sali sana kwa Mwenyezi Mungu (Allah) akusaidie Kutuongoza vyema Watanzania na kamwe usitafute Suluhisho la kudumu kwa tatizo Kubwa na Gumu kwa kutumia njia nyepesi yenye Washauri wako wasioitakia mema Tanzania.

Nimesikitika sana na mno Rais kwa jinsi unavyoendeleza Ligi usiyoiweza na hutoiweza na Wakatoliki / TEC Tanzania.
 
Ni dhahiri jumapili hukwenda kugawa mafuta na kuchotea watu udongo, na hizi ndio akili zako nzuri kabisaa ulizokuwa unajidai nazo pale mitaa ya Nsumba ukiwa chuo mtakatifu Agustino ,uache sasa kula mikate ya upako bado hujachelewa unaweza kupona ukijiwahi.

NB: Karibu hapa Solya hapa nauza mafuta ya alizeti
 
Umemuadress Mama kwenye paragraphs zote wakati heading inaonesha huna uhakika ni mkakati wa nani.
GENTAMYCINE sijawahi kamwe kueleweka na sitoeleweka daima na Wapumbavu wa mfano wako hapa JamiiForums.
 
Back
Top Bottom