Rais Samia hataki kodi za dhuluma; Lipeni kodi na tozo

Rais Samia hataki kodi za dhuluma; Lipeni kodi na tozo

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
9,424
Reaction score
23,816
Mama yetu mpendwa samia(Chui Jike) alipoingia madarakani alisema hataki makodi ya dhuluma kama ya mwendazake.

Bwana yule mwendazake, alichota na kuvuna kodi kutoka kwa majizi bila huruma.

Mabeberu yalilipa kodi stahiki kwa kutumia mkono wa chuma huku wanyonge wakila bata kwa kulipia elfu ishirini tu ya kitambulisho kwa mwaka.

Hiyo haikuwa demokrasia. Ni udikteta mbaya kwa sababu majizi yanatakiwa kubembelezwa yasije kututoroka ati.

Kwa msingi huo, mama hataki kodi za kushurutisha kama mwendazake. Lipeni tozo za miamala ya simu na benki. Hatutaki janja janja.

Na vifurushi vya mitandao pia mlipie gharama iliyowekwa na mamlaka. Tunakuza maendeleo.

Tunakupa mshahara tunakata kodi za serikali, ukienda kuutoa tunakata pia tozo zetu. Hapo vipi? Huo ndio uchumi wa kweli.

Samia oyeee! Lipeni kodi na tozo.
 
Nimeona kuwa miamala ya mpesa imewekewa kiwango cha juu kusudi ukitaka kutuma pesa nyingi basi ulipe tozo mara nyingi pia.

Kwa mfano mwaka jana niliwahi kumpelekea mama shiling milioni nne kwa kutumia mpesa lakini leo nilipotaka kupeleka milioni nne nikaambia kuwa kiwango cha mwisho ni milioni tatu, kwa hiyo nikatuma milioni tatu hizo, na kuongezea milioni moja, na kusababisha tozo mara mbili..

Tutanyooka.
 
umetupasha tena kwa kuongea kinyume chake.tulipe tozo au kama vipi Burundi patuhusu mbwa wakubwa sie.
Tozo ni kwa maendeleo yako wewe, mimi na jamii nzima kwaiyo lazima tulipe tozo ili tuondokane na utegemezi
 
Mama yetu mpendwa samia(Chui Jike) alipoingia madarakani alisema hataki makodi ya dhuluma kama ya mwendazake.

Bwana yule mwendazake, alichota na kuvuna kodi kutoka kwa majizi bila huruma.

Mabeberu yalilipa kodi stahiki kwa kutumia mkono wa chuma huku wanyonge wakila bata kwa kulipia elfu ishirini tu ya kitambulisho kwa mwaka.

Hiyo haikuwa demokrasia. Ni udikteta mbaya kwa sababu majizi yanatakiwa kubembelezwa yasije kututoroka ati.

Kwa msingi huo, mama hataki kodi za kushurutisha kama mwendazake. Lipeni tozo za miamala ya simu na benki. Hatutaki janja janja.

Na vifurushi vya mitandao pia mlipie gharama iliyowekwa na mamlaka. Tunakuza maendeleo.

Tunakupa mshahara tunakata kodi za serikali, ukienda kuutoa tunakata pia tozo zetu. Hapo vipi? Huo ndio uchumi.

Samia oyeee! Lipeni kodi na tozo.
Tozo kwa maendeleo ya jamii lazima tutoe tu
 
Watupe elimu ya Kodi yaani mlipaji na mkusanyaji lakini kama mtu anakaa Ikulu na ushungi anapanga Tu huo ni ujambazi
 
Back
Top Bottom