Rais Samia: Haikuwa na maana kuchoma vifaranga wa kuku mpakani

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,052
24,442
Katika kongamano la biashara lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambalo limehusisha viongozi wawili wakubwa ambao ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Tanzania Samia Hassan Suluhu.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amesema kwamba hakukuwa na haja ya kuchoma vifaranga waliokamatwa nchini Tanzania kutoka nchi jirani.

Amesema pia kuna kipindi ilitokea pia Sukari kutoka nchi ya Uganda iligomewa na wafanya biashara kutoka Tanzania, hivyo amemueleza Rais Museven kwamba hivi sasa Sukari kutoka Uganda itanunuliwa na wafanyabiashara wa Tanzania!

Amehimiza pia kwamba vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili viondolewe!

Hayo yamesemwa wakati Kongamano hilo likifungwa.
 
Daah! wale vifaranga walivyochomwa tukaambiwa eti wanamagonjwa, kumbe ilikuwa roho mbaya ya Bwana yule. Taratiiibu ukweli wa yaliyofichwa unaanza kuwekwa wazi! Soon hata wale wasiojulikana wanaojulikana maza atawasema siku moja mchana kweupe!
Tuombe itokee hvyo!!
 
Mimi huwa naona Museveni na Marais wa CCM ni marafiki sana, Kuna vitu wanashabiriana. Sitashangaa assert moja wapo ya Tz ikikamatwa Kama uwanja wa ndege uganda ulivyoshikiriwa na wachina!
 
Mimi huwa naona Museveni na Marais wa CCM ni marafiki sana, Kuna vitu wanashabiriana. Sitashangaa assert moja wapo ya Tz ikikamatwa Kama uwanja wa ndege uganda ulivyoshikiriwa na wachina!
Haa bandari ya Dar ili kufidia mkopo wa ujenzi wa Bagamoyo
 
Mimi huwa naona Museveni na Marais wa CCM ni marafiki sana, Kuna vitu wanashabiriana. Sitashangaa assert moja wapo ya Tz ikikamatwa Kama uwanja wa ndege uganda ulivyoshikiriwa na wachina!
Museven anakadi ya CCM. Aliichukua kipindi babaake anawaongoza wadanganyika
 
Utalindaje wazalishaji wa ndani, bei za bidhaa nchi jirani ziko chini na mipaka ya nchi ipo wazi kila pembe kupitisha magendo, Tunaenda kuua viwanda vya ndani

Kwani baada ya kuchoma wale vifaranga ni viwanda vingapi vya ndani vimeanzishwa?
Na kabla ya kuvichoma ni viwanda vingapi vilikuwa vimeuliwa, maana vifaranga walikuwa wakiingizwa!
 
Utalindaje wazalishaji wa ndani, bei za bidhaa nchi jirani ziko chini na mipaka ya nchi ipo wazi kila pembe kupitisha magendo, Tunaenda kuua viwanda vya ndani
Mkuu, kama bei ziko hivi, bora vife tu! Sukari toka 1500 hadi 3000 in 6 years, viwanda visaidie wananchi, kama vinaumiza na hawataki kuruhusu importation ili waendelee kupiga faida. Importation italeta competition, viwanda vyetu nao wa export.
 
Back
Top Bottom