Rais Samia endelea kufagia masamjo

juctn Mt

Member
Jan 12, 2019
38
37
Well, Tarehe 29/11/2023 Ni Siku Nyingine Tena ambayo kamati ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM itakwenda kuketi Kama ilivyo Ada, Ni Kwenda kutimiza Majukumu yake.

Wakati Kama huu 'Masamjo' huwa wanawaza sana! Masamjo waliojitengenezea Territory na Imani kuwa" wanamtakia Mema Sana Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM" lakini Hapo Hapo wakiwa wanajiweka Mbali na Mwenyekiti katika Kumjibia Hoja za Msingi za Wananchi Kama vile issue za "Umeme" na "DP World n.k

Na Kuna kina Sisi hapa ambao tukikumbusha Mambo ya Msingi kwa lengo la Kumsaidia Mh Rais na Taifa Basi Masamjo huibuka haraka na kutubatiza Majina Kama "Wenye Njaa" n.k,hata Kutuchongea huko Juu kwa Maneno Mengi ya Uongo Kwamba Sisi Ni Wasaliti, tunamchafua Mama n.k!, ",Hawa Hawa wanaotuchongea ndio wanaotumika Kuweka "Barriers" Kati ya "Mama" na "Wachapakazi" na kwa Maana Kadri Mama anavyoendelea kupitisha Fagio la Wazembe na kuchukua Wachapakazi Basi na ndivyo hivyo Kizazi Cha Masamjo Wababishaji kinavyozidi kupoteza Uhakika wa Nafasi zao, Tazama Teuzi Kama ya Makonda katika Majukumu ya Chama ilivyowachanganya Masamjo! Je Mwenyekiti ndio ameishia Hapo au ataendelea Kuboresha Safu...."Masamjo" Tumbo Joto!, Hivi Ni Samjo Gani Mwenye Amani kwenye Nafasi yake hiyo asiyoitendea Haki huku wale Viongozi imara na Makini kama Ole Sabaya wakiwa Huru na bado vijana wenye uwezo wa kulitumikia Taifa hili?

Huu ndio Wakati ambao "Masamjo" ndani ya Chama bado wanakodoa kodoa! hawaelewi Ni kwa Nini Mtu Kama Makonda amewekwa pale, na Ni Nani na Nani" Viongozi Aina ya Makonda" watafuata, ni Technical Substitution yenye Afya kwa Wengi lakini isiyo Afya kwa "Wachache Wasamjo" ndani na Nje ya CCM.

Taifa Lina Changamoto Nyingi Sana,kwa Mfano issue ya Umeme n.k, na Katika Uwiano huo huo ndipo unapokutana na Baadhi ya Viongozi Mizigo na Masamjo walioshindwa Kumsaidia Mh Rais, Mh Rais endelea Kuwapangusa, kwa Maana Malengo Mema yatatimiaje Kama Wapo Watu Wachache ambao Mh Rais umewaamini wakusaidie lakini badala yake wamebaki na Alama "A" katika Kubadili Aina za kaunda suti na kusimama kwenye Podium huku wakiwa na Alama "F" katika kuyatekeleza Yale Majukumu Uliyowapa kwa ajili ya Nchi...Mh Rais endelea Kufagia, Ni Vema kuanga Safu ya Wachapakazi.

Mh Rais na Mwenyekiti wangu pale unapoona umeteua Mtu halafu wengi "wanashangilia" halafu "Wachache wanabwata! Basi kazia hapo Hapo kwa kuteua Aina hiyo kwa wingi kwa Maana hao ndio Wasaidizi wa Kweli, na Daima Watu Walio Makini na Wakweli hupigwa Vita!

Naamini kuwa Mh Rais unapoendelea Kufagia Masamjo na kuwa-replace na Wachapakazi Basi jina lako litabaki katika kumbukumbu Chanya na Historia Njema ya Taifa hili, Mh Rais Wewe sio Adui wa Wananchi kwa kuwa hata wewe pia ungetamani Siku Moja unapoondoka Madarakani Jina lako likumbukwe kwa Mazuri.

Kwa kuhitimisha “Mama Vuta kina Happy, Ole Sabaya, Polepole na sampuli ambazo pengine sumu ilisagwa kwao lakini Mwenyezi MUNGU Muaminifu amekuonyesha kuwa ni kheri Sana wale wanaokosea wakitenda kwa dhati kuliko wale wanaonyamaza kimya ili wasikosee huku wakitaka waonekane “wasafi” kwa ajenda zao.

Pio Pius.
 
Back
Top Bottom