Rais Samia azindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dodoma Julai 17, 2025

Rais Samia azindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dodoma Julai 17, 2025

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,521
Usiondoke JF

Rais Samia Suluhu Hassan leo anazindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Uzinduzi huo utafanyika wakati wa Mkutano wa Tatu wa Taifa wa Dira, na unatajwa kuwa ni tukio kubwa la kihistoria, likiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa dira ya muda mrefu ya maendeleo ya taifa.

Mchakato wa maandalizi ya Dira hiyo umehusisha ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, huku maoni ya Watanzania kutoka makundi mbalimbali yakichangia msingi wa dira hiyo.


View: https://www.youtube.com/watch?v=8LjsYo62HTk

1752740914856.png

Mwenyekuti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ni miongoni mwa wageni wanaoshiriki hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 leo Julai 17, 2025.

Dkt. Fred Msemwa - Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango

"Kazi ya kukusanya maoni imefanyika kwa ufanisi mkubwa, tulitumia njia mbalimbali katika kuhakikisha kila Mtanzania popote alipo anaweza kutoa maoni. Tulipita Kaya kwa Kaya, Nyumba kwa Nyumba ambapo tulikuwa na madodoso ili kuuliza Wananchi wenzetu juu ya maoni yao kuhusu Dira na matamanio yao ya namna wanavyotaka nchi yetu iwe itakapofika mwaka 2050"

"Kupitia utaratibu huo Mhe. Rais tuliweza kuwafikia Watanzania Milioni 1.174 ambao walitoa maoni ya ana kwa ana kupitia Kaya zao"

Rostam Aziz - Mfanyabiashara (Mwakilishi Sector binafsi)

"Sisi sector binafsi tulisikilizwa na maoni yetu yalitumika katika kuunda Dira hii"

"Kuandaa Dira ya Maendeleo ni muhimu, kuwa na mipango ya maendeleo ni muhimu, kupanga ni muhimu. Kila hatua ya maana ya maendeleo huanzia katika kupanga. Lazima tukubaliane kama nchi kuwa hatua ya maana zaidi inayotusubiri katika kupata mafanikio tunayoyatarajia katika dira hii ni utekelezaji."

"Sisi Watanzania ni hodari sana wa kupanga, lakini inapofikia utekelezaji hubweteka na kusuasua. Kama sekta binafsi, tunaomba tubadilike na safari hii tutekeleze kwa kweli."

"Ili Tanzania ipige hatua katika karne ya 21, ni lazima kuwekeza kwa makusudi kwenye rasilimali watu, hasa vijana. Hatua ya kwanza ni kuanzisha mfuko wa maendeleo ya vipaji wenye bajeti ya takribani dola milioni 100 kwa mwaka. Kupitia mpango huu, tutawatambua na kuwalea vijana 1,000 wenye uwezo mkubwa kiakili katika nyanja za kimkakati kama uhandisi, akili mnemba (AI), sayansi ya takwimu, fedha, na nyingine muhimu kwa maendeleo ya taifa."

Profesa Kitila Mkumbo - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

"Asilimia 81 ya watu 1,132,837 waliojitokeza kutoa maoni yao kwa njia ya ujumbe wa simu, tovuti na mitandao ya kijamii walikuwa vijana wa umri kati ya miaka 15–35. Dira hii, kwa kuzingatia maoni yao, imeandikwa kwa vijana ambao wataishinayo kwa muda mrefu zaidi."

"Hii inaonyesha wazi sura ya demografia ya Tanzania, ambapo asilimia 76 ya Watanzania wote wako chini ya miaka 36. Ni dira iliyoandikwa na vijana na itakayotekelezwa na vijana hao kwa muda mrefu zaidi"

"Tanzania kuwa na pato la Taifa lenye thamani ya Dola za Marekani Trilioni 1 na wastani wa pato la mtu mmoja lenye thamani ya Dola za Marekani 7,000 kwa hivyo range ya Benki ya Dunia ni kati ya 4516 mpaka 14,000 wataalamu wetu wamekaa wakachambua wakafanya modelling na Mheshimiwa Rais hizi namba hazikushuka tu"

"Tulikutana na viongozi 19 wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa, katika vikao viwili, na kupata maoni yao ya jumla. Hatimaye, wakakubaliana kwamba haya ndiyo maono yetu Watanzania, na wakakubaliana kwamba Ilani zetu za vyama katika uchaguzi wa mwaka huu (Oktoba 2025) zizingatie na kuakisi maudhui ya Dira 2050."

"Malengo mahususi ya Dira ni: (i) Tanzania kufikia hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Uchumi wa kati ngazi ya juu ni uchumi ambao pato la taifa kwa mtu mmoja linathamani ya dola za Marekani kati ya 4,516 na 14,005."

"Lengo la pili mahususi ni maisha bora na ustawi kwa wote."

Jakaya Mrisho Kikwete - Rais mstaafu wa Awamu ya Nne

"Dira 2025 inaakisi mahitaji, matarajio, matamanio na maono ya Watanzania walio wengi"

"Mhe. Rais, nilitoa maoni kadhaa, lakini kubwa la msingi kwangu mimi nilieleza furaha yangu kuona shabaha ya msingi ya Dira 2050 itakuwa kuitoa Tanzania kutoka nchi ya uchumi wa kati ngazi ya kwanza/chini na kufikia uchumi wa kati ngazi ya juu ifikapo 2050."

Dkt. Hussein Ali Mwinyi - Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

"Dira hii mpya itatuongoza katika kufahamu wapi Tanzania inatarajia kufika katika miaka 25 ijayo katika kuimarisha ustawi wa wananchi wake."

"Dira ya Maendeleo ni nyenzo muhimu inayotumiwa na taifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo kwa muda unaokusudiwa. Dira lazima izingatie matakwa na iwashirikishe wananchi kikamilifu."

Dkt. Samia Suluhu Hassan - Rais wa JMT

"Kama mnakumbuka Dk Philip Mpango (Makamu wa Rais) alisema kwa anavyojisikia angeomba kupumzika lakini nilikuwa namwambia hupumziki, usimamizi wa Dira na Mpango wa Maendeleo ni jukumu lake, atapumzika kiaina lakini yupo kazini."

"Nchi hii pamoja na utajiri wa rasilimali zake, bado ina watu wengi masikini. Kwa hivyo, changamoto yetu kubwa kama viongozi ni kubuni na kutekeleza mipango na mikakati madhubuti ya kutumia utajiri wa nchi yetu katika kufaidisha maisha halisi ya Watanzania."

"Ndani ya kipindi cha miongo 6 ya Uhuru wa Nchi yetu, dhoruba nyingi zimelitikisa bara la Afrika na kudhoofisha nchi nyingi ila Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobalki Imara, tumeweza kudumisha utamaduni wa Kidemokrasia wakupokezana madaraka na uongozi kwa njia ya Amani, mimi ni Rais wa 6 nikitanguliwa na Marais Watano na Rais wa awamiu ya 4 tukonaye pamoja"

"Mtakubaliana nami kwamba kuna hali ya kudorora kwa ari ya kujadili masuala ya maendeleo katika jamii yetu, hususan miongoni mwa vijana ambao ndiyo tegemeo letu katika kujenga kesho iliyo bora. Hii siyo sawa hata kidogo. Katika miaka 25 ijayo lazima turudishe mijadala ya maendeleo katika nchi yetu ijadiliwe na vijana na wajipange vyema katika utekelezaji wake kama ilivyokuwa misingi yetu kabla."

"Maudhui ya Dira 2050 yametokana na maoni na matakwa ya Watanzania wenyewe. Tumefikiri wenyewe, tumeandika wenyewe, tumepanga wenyewe, na tutatekeleza wenyewe kwa kushirikiana na wale tutakaoona wanatusaidia."
 
Hilo ni wazo zuri kijamii na linaonesha dira ya matumaini kwa watoto wa familia masikini. Hata hivyo, utekelezaji wa elimu bure hadi chuo kikuu unahitaji mipango madhubuti ya kifedha, rasilimali watu, miundombinu, na dhamira ya kweli ya kisera.

Swali muhimu kwa wananchi ni: Je, CCM itaweza kutekeleza hilo kwa vitendo au ni ahadi nyingine ya kisiasa? Historia ya utekelezaji wa ahadi kama hizi inaweza kusaidia kutathmini uhalisia wake.
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo atazindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Uzinduzi huo utafanyika wakati wa Mkutano wa Tatu wa Taifa wa Dira, na unatajwa kuwa ni tukio kubwa la kihistoria, likiwa ni mara ya pili kwa Tanzania kuandaa dira ya muda mrefu ya maendeleo ya taifa.

Mchakato wa maandalizi ya Dira hiyo umehusisha ushirikiano wa kitaifa na kimataifa, huku maoni ya Watanzania kutoka makundi mbalimbali yakichangia msingi wa dira hiyo.

 
Sijui ni uelewa wangu au vipi ila naona huu ni mwendelezo wa kuwalisha wananchi maneno matamu bila mikakati sahihi

Nilitegemea mipango na dira za maendeleo zingejikita kwenye Target na what should be done to achieve target.

As tunaweza sema

Kwenye Umeme

Target: Kuzalisha megawati laki 2 za umeme kufikia 2050

Mambo ya kufanywa:
1. Kuanzisha mradi wa Umeme wa Nyuklia kuzalisha Megawati elfu 50

2. Kuanzisha Mradi wa Umeme wa Jua wa Megawati elfu 50

3. Kuanzisha Mradi wa Umeme wa Geothermal megawati elfu 10

4. Kuboresha mradi wa Umeme kupitia Gesi Megawati elfu 20

5. Vyanzo vingine- Megawati elfu 50

Then kwenye bajeti za Taifa za kila mwaka mipango kwenye Umeme inajikita hapo.


Kwa sasa naona ni kama mwendelezo wa kuwalisha wananchi maneno matamu tena matupu tu.

Sijaona chochote cha maana hapo.
 
Usiondoke JF

Ni muhimu ukaelewa Tulikotoka , Tulipo na Tunakokwenda

Ahsanteni sana 🙏
DIRA YOYOTE ISIYOTOKA KWA WANANCHI NI KUPOTEZA MUDA NA RASILIMALI,RAISI SAMIA UMEAMBIWA KWAMBA SIKILIZA WATANZANIA WANATAKA NINI,MAWAZO YA MTU NA MUME WAKE ,AU MTU NA RAFIKI ZAKE NA TENA MAWAZO YA WAHUNI NA WENYE KIBURI,HAYAWEZI KUWA DIRA YA TAIFA:ZAIDI NI KIBURI, UHUNI NA UZANDIKI USIOKUBALIKA.
 
Back
Top Bottom