Rais Samia apewe haki yake katika haya

Mbona hilo tone la maji mungu wenu wa Chato hakuliongeza kwa miaka yote 5 akiwa Ikulu?
Alizuia saana mfumko wa bei ndo maana life lilibalance, lakni huyu bei juuu inayomeza hadi kanyongeza. Anavyowinda misaada huyu lockdown ingetuhusu ila Mungu fundi akamlinda kwanza jpm atuvushe.
 
Mmeanza sifa za kijinga? Sifia wa maana uko kwenye ulaji. Sisi maisha yetu ni magumu hatuoni chochote cha kusifia.
Maisha yako hayawezi kuwa mazuri kwa kukaa tu kupuyanga JF bila kujishirikisha na shughuli yeyote ya uchumi. Hata Mbowe au Lissu akiwa Rais hatakugawia hela za kuboresha maisha bali ataleta sera na mipango ya uchumi tu, ambayo wewe utatakiwa kushiriki ili uzalishe mali ndipo upate fedha.
 
Alizuia saana mfumko wa bei ndo maana life lilibalance, lakni huyu bei juuu inayomeza hadi kanyongeza. Anavyowinda misaada huyu lockdown ingetuhusu ila Mungu fundi akamlinda kwanza jpm atuvushe.
Hivi unajuwa kuwa DIKTETA Magufuli kwa miaka 5 ndiye Rais aliyekopa madeni kwenye taasisi za fedha za ndani na nje kuliko Rais yeyote toka nchi ipate uhuru? Alikuta tunadaiwa Tsh 32 Trillion na wakati anakufa deni lilipanda hadi Tsh 59 Trillion? Yaani alikooa Tsh 29 Trillion wakati J Kikwette alikopa Tsh 10 Trillion kwa miaka 10.

Ila wajinga akili zenu zimepigwa ganzi, mnashanga Samia anapokiri kuwa anakopa, wakati yule alikuwa anawadanganya kuwa ni hela za ndani!!
 

Mkuu na mimi nataka nipewe cheo nile kwa ulaini kama hao wengine wanaopendelewa. Hapa nilipo nafanya shughuli isiyolioa maana wateja hakuna. Labda mniunganishe kwenye asali kama nyie mnaosifia, na mimi nianze kusifia kama nyie.
 
Mkuu acha kupotosha hamna mshahara uliongezeka,hicho kiwango cha 23.3% kilichotangazwa ni mpango utekelezaji wake bado-so,kitu ambacho watu hawajapokea huwezi sema kimisha ongezwa.

Pili,hivyo viwango vya posho ni politics kama zilivyo politics zingine,maana viwango hivyo havijaambatana na ongezeko la bajeti.So ukitumia badget iliyopitishwa hi hi maana yake siku tu ndio zitapungua-hilo ni changa La macho.
 
😂😂 32 to 59 then alikopa 29? Hesabu za wap hizi? Mbona sa hvi ni 70+ means maza kwa mwaka mmoja alishafikisha 11 trilion!! Ratio kali sana hii.
 
Kwa hio watu wote 60m waajiriwe serikalini?
Au unatakaje boss?!
Ila kwa mbaaali nakuona una dalili za kuwa mchawi. Waache waliobahatika kuwepo serikalini wafaidi uwepo wa mama na we endelea kulima tumbaku mama atapandisha bei msimu huu.

For real umeandika hayo
Jisikitikie
Jitahidi uwe GT haswa humu
 
Mmeanza sifa za kijinga? Sifia wa maana uko kwenye ulaji. Sisi maisha yetu ni magumu hatuoni chochote cha kusifia.
Kama maisha yako magumu unataka kila mtu yawe magumu? maisha yako kuwa magumu kuna muda ni ujinga wako, usitafute kichaka cha kutoa visingizio.
 
Kama maisha yako magumu unataka kila mtu yawe magumu? maisha yako kuwa magumu kuna muda ni ujinga wako, usitafute kichaka cha kutoa visingizio.

Ni kweli, ni ujinga wangu wa kutokusifia kama wewe.
 
Huyu raisi wakatiba Huyu ameziba masikio kabisa hataki kusikia changamoto tunazopitia huku mtaani ona sasa wanamsifia na huku ... daah hii ndo Africa kiongozi akipata cheo tayari wanamfanya Mungu wanamuamini kiasi kwamba hakosei na ndo wanaotuaribia nchi
 
Changamoto zako pambana nazo mwenyewe. Siyo umekaa sebuleni kwa shemeji yako unatarajia utatuliwe na Rais kwa kulalamika humu JF. Acheni uzembe vijana
 
Hao ni wabongo katika ubora wao huwa hawana jema hata siku moja, kwao kila siku ni ya kulialia tu.
 
Anazijua changamoto kuliko unavyozijua wewe. Yupo kikazi zaidi hana zile siasa za kusimama na kuwasikiliza watu ili apate mileage za muda mfupi.

Anafungua fursa pana ni jukumu langu na la kwako kuzichangamkia na kufaidika nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…