Rais Samia, anza na Dkt. Abassi ameonesha dharau na kiburi kwako

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Watanzania wamesikia kauli yako ya kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa vifunguliwe ila vifuate sheria

Kama Mkuu wa Nchi na Kama Mama umeona utoe huo msamaha tuanze upya lakini ukasisitiza vifuate Sheria.

Lakini huko kwenye vyombo vya habari kuna ajira nyingi zilipotea na kusimama, amri yako inatoa fursa na ahueni kwenye suala hilo kwani kuna ambao waliathirika kiuchumi kwa kufungiwa huko na kuishi maisha ya tabu

Ila Mama yetu, Katibu Mkuu anayehusika na tasnia ya Habari ameamua kuonesha Kiburi na Jeuri na pia kukosea heshima kwako kama Mkuu wa Nchi kwa kupindisha agizo lako kuwa hukusema vyombo vya habari( hadi magazeti) lakini pia anataka kuonesha kuwa hauwezi kujieleza vizuri ndio maana anasema haukusema na magazeti, alitaka utamke kwa mtiririko kila chombo cha habari ili yeye PhD holder akuelewe.

Yeye ni nani awe na dharau na kiburi namna hii kwa Mkuu wetu wa nchi? Au ni moja ya watu waliokuwa hawataki wewe uwe hapo kwa mawazo yao kuwa hautoweza?

Mama yetu tunajua wewe ni mpole na uliyejaa hekima na busara kutokana kuwa Mama, mzazi, umri na hata asili ya maeneo unayotoka lakini hili lisichukuliwe ni udhaifu( kama ulivyosema kwenye hotuba yako). Inaonekana Dr Abbas anachukulia ni udhaifu na ndio maana ana kiburi cha kupingana na maelekezo yako.

Ni vyema Mama umfanye awe mfano kwa wengine kuwa upole wako na busara sio udhaifu ili wengine wajifunze. Wangoni wanasema "Make a statement"

Cha ajabu pamoja na watu kumkumbusha bado mpaka sasa anaonesha jeuri na kiburi,huyu anakudharau mbele ya macho ya watanzania.

Mama najua una huruma, utu, hekima, upendo kama huwezi kumuweka benchi basi angalia nafasi za maDAS huko mipakani zilizowazi umpangie majukumu mengine

Mama huyu kijana AMEKUZINGUA na wewe MZINGUE
 
Acha uchochezi usiokuwa na tija, unazani kufunguliwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kama kufungua mlango wa choo chako unapobanwa na haja!?
 
Dr. Abass ni mwanasheria mpuuzi sana.
Ivi huyu ni mwanasheria gani anashindwa kuelewa maana ya vyombo vya Jabari kwa ujumla wake?
Kweli anamdharau mama maana yeye alikuwa kwenye ule mpango halali wa kuongeza muda kwa yule fedhuli mwendazake
 
Acha uchochezi usiokuwa na tija, unazani kufunguliwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kama kufungua mlango wa choo chako unapobanwa na haja!?
Mama ameshasema vifunguliwe yeye alitakiwa kusema kama mtendaji Mkuu watalifanyia kazi sio kiburi
 
Acha uchochezi usiokuwa na tija, unazani kufunguliwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ni kama kufungua mlango wa choo chako unapobanwa na haja!?
mkuu hujamuelewa huyo jamaa unayemjibu, hoja yake imejikita kwenye kauli ya jana ya Abbas sio kusema eti hayo magazeti yafunguliwe haraka, jamaa analalamika kwanini Abbas atoe kauli kama ile ambayo inaonesha kudharau mamlaka yani anataka rais amuagize mara mbili
 
Dr. Abass ni mwanasheria mpuuzi sana.
Ivi huyu ni mwanasheria gani anashindwa kuelewa maana ya vyombo vya Jabari kwa ujumla wake?
Kweli anamdharau mama maana yeye alikuwa kwenye ule mpango halali wa kuongeza muda kwa yule fedhuli mwendazake
Na alikuwa mnufaika kwa sababu alikuwa na vyeo viwili.
 
Mama ameshasema vifunguliwe yeye alitakiwa kusema kama mtendaji Mkuu watalifanyia kazi sio kiburi
sahihi kabisa, yani jamaa ana Access na rais anashindwa kumuuliza kama hajaelewa vizuri anakuja kuropoka kwamba rais hajaongelea magazeti, kwani vyombo vya habari si na magazeti yamo
 
sahihi kabisa, yani jamaa ana Access na rais anashindwa kumuuliza kama hajaelewa vizuri anakuja kuropoka kwamba rais hajaongelea magazeti, kwani vyombo vya habari si na magazeti yamo
Angetamka Chuma enzi zile asingeleta hizi habari
 
Back
Top Bottom