Hamnaga mzuri kwenu daima. Hamkumpenda kikwete eti anachekacheka, mkasema mnataka rais dikteta akaja Magufuli akaanza kuwadektetua mara mkaanza kuomboleza kwa vilio ...mkata demokrasia kaja mama kawaachia uhuru na demokrasia, mmeanza kumtukana matusi na kutaka kumpanda kichwani Sasa ngoja awanyooshe ili mjitambue.
Tatizo wapinzani hamjawahi kueleweka nini mnachohitaji . Mlimuita lowasa fisadi hatari kwamba hafai kuwa rais mara mkamtakasa akawa mgombea wenu ,mkambeba na nyalandu mkataka awe mgombea haya Sasa wote wamewakimbia wamerudi ccm ...
Sasa nyie tuwaelewe vipi ? Hamjui mnachokisimamia Wala mnachokihitaji.. inaonyesha wazi lengo lenu sio kuikomboa nchi Kama mnavyojinadi majukwaani Lengo lenu na nyie mpate ulaji basiii ...kwa jinsi hii kweli mnataka tuwape nchii aasubutuuu .... acheni tupambane na ccm tu