Rais Samia anacheza Drafti, wenzake wanacheza Chess

Rais Samia anacheza Drafti, wenzake wanacheza Chess

Randy orton

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2019
Posts
1,338
Reaction score
3,575
Kuna watu wako nyuma ya Mama kazi yao ni kumdanganya tu.

Kwa bahati mbaya inaonekana Mama anadeal na anachokiona sio 2025.

Watu hao wamemshauri amepandisha makodi kwenye kila kitu kinachomgusa maskini wa mwisho na mwenye kipato cha kati. Kwa bahati mbaya tena sera za mama ni rafiki kwa matajiri na kilio kwa maskini ambao ndio wapiga kura.

Mama ameshapoteza mvuto kwa watu wengi wa nchi ya Pakistan kwa sababu sera zake nyingi zinaongeza mzigo wa maisha kwa walala hoi na wenye vipato vya kati.

Kwa kawaida tunategemea angekuwa na huruma na watu maskini ukizingatia yeye ni mama pia, umaskini unaongeza mzigo kwa wamama mbalimbali ni kama Mama yupo kwenye parallel universe tofauti na wanachi wake.

Nilichogundua kuna watu wako huko kwenye mfumo wanacheza Chess , hesabu zao ni za mbali sana , ilishindikana kutupilia mbali katiba ya Pakistan , wameamua kucheza Chess ili mtu wao aje post 2025. Mama na team yake wanaendelea kucheza drafti, wanachoambiwa wanafanya bila kujua hesabu zao ni za drafti ili hali wataalam wanacheza Chess
 
Mi ninavyoona hana mpango wa kugombea tena lile gazeti lao haikua bahati mbaya ... kina january na timu yake wanamchora tu anavyojipaka matope
 
Atakuwa ameambiwa kwa kuwa huna mpango wa kugombea tena ... huu ndio wakati wa mavuno ... 2025 wanamtoa wanamleta atakae ondoa hizo tozo but it will be too late
 
Nope! Have to disagree with you Mkuu... yy Anajua anachokifanya na anahusika kikamilifu....they are replacing this country's tax bracket ,jua tu kuna watu wanapata ahueni sasa...
 
Kuna watu wako nyuma ya Mama kazi yao ni kumdanganya tu.

Kwa bahati mbaya inaonekana Mama anadeal na anachokiona sio 2025...
Kwa Hali ilivyo Wakifika salama 2025 nahamia bujumbura burundi Laana ya kuiba uchaguzi haitawaacha salama
 
Back
Top Bottom