Rais Samia amedhihirisha utendaji wake wa kazi ni awamu ya pili na tatu, combined

GOAT25

Member
Nov 29, 2021
23
16
Ndugu zangu nawasalimu kwa jina la JMT

Kazi iendelee!

Kwa jinsi awamu ya sita toka imeingia madarakani takribani miezi nane sasa.

Rais SSH amedhihirisha utendaji wake wa kazi ni awamu ya pili, na tatu, combined.

RUKHSA (awamu ya pili)

Rais SSH amekuwa akisisitiza Mara nyingi kuifungua nchi hasa katika suala la biashara nchini na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi ni Jana tu ameruhusu sukari ya UG kupewa kibali kuuzwa TZ ili kumsaidia mwananchi anunue sukari kwa bei rahisi.

Achilia mbali biashara kati ya KENYA na TZ kuimarika. Rais Mstaafu Mwinyi alipochukua madaraka alikuwa na agenda ya rukhsa ambayo Rais SSH anatekeleza.

UWAZI NA UKWELI, DIPLOMASIA, UWEKEZAJI (awamu ya tatu)

Mambo hayo ndio yalikuwa Sera kuu ya awamu ya tatu ya Hayati BMW.

Tumeona hayo yakitekelezwa na Rais SSH

kwenye diplomasia, na uwekezaji, mazingira ya uwekezaji yameboreshwa kutoka kupata kibali mwezi mmoja Hadi siku 1.

Kwenye uwazi na ukweli wote ni mashahidi jinsi uwazi wa mkopo wa 1.3tr wa IMF ulivyowekwa bayana na matumizi yake

Hakika tuna matumaini mazuri mengi yatakuja kutoka kwa Rais SSH

Mungu ibariki TZ

Signed out
GOAT 25
 
Hapo angechanganya na wa JK, ya angalau kuruhusu demokrasia ya vyama vingi ifanye kazi yake, ingekuwa bora sana!!lakini sio mbaya sana kulinganisha na tanuru tulilokuwa nalo (awamu ya meko)
 
Hapo angechanganya na wa JK, ya angalau kuruhusu demokrasia ya vyama vingi ifanye kazi yake, ingekuwa bora sana!!lakini sio mbaya sana kulinganisha na tanuru tulilokuwa nalo(awamu ya meko)
Akitupatia Katiba mpya...atakuwa na Sera za awamu ya nne..naamini atatupatia Katiba tumpe muda Kama alivyoomba.
 
.Mimi nasubiri tu Mama akiri dhambi hizi....

Risasi kwa TL
MDUDE
MAWAZO
Saa 8
KUNUNUA akina WaItaRa....
Aquiline AQUELINA
AZORY
Etc...

Zipo nyingi. Akiri tu na Roho yangu itulie.TUANZE UPYA.
 
Una hakika gani hizo hela zinaenda kwenye kujenga mashule na zahanati na mabweni sijui!
Ada za kazi gani wazazi walipe?
Tozo zina kazi gani kama tunalipishwa ada na michango?
Serikali yake kutoka hadharani na kutupa matumizi ya mkopo huo ni Uwazi mkubwa...
Kuhusu tozo zilishatolewa ufafanuzi boss
 
Akitupatia Katiba mpya...atakuwa na Sera za awamu ya nne..naamini atatupatia Katiba tumpe muda Kama alivyoomba.
Ni kweli mkuu, kwani tumemaliza awamu ngumu sana!!imebidi MUNGU, atuonee huruma tu waja wake, kwani tulikuwa tumeingizwa kwenye mtumbwi wa kibwengo, yaani mnaona bora hata kuongozwa na mkoloni !!na hata baadhi ya kauli zake unaona kabisa kuwa hata yeye kuna ujinga ulikuwa unafanyika haukubali, mfano ule wa kuchoma vifaranga, ule ulikuwa ni ukatili sana!!lakini mwenazake fc waliona ni shujaa!!SIASA ZA MIAKA YA YA 50, ndio jamaa alikuwa anazitumia miaka hii lazima uta fail tu mjini!!
 
Rais SSH amekuwa akisisitiza Mara nyingi kuifungua nchi hasa katika suala la biashara nchini na kuimarisha diplomasia ya kiuchumi
Tumekuwa tunawauliza kila mara hili swa "Ni nani aliifunga nchi na kuharibu diplomasia?" lakini hamtaki kutupa jibu sahihi
 
Kila kitu Ruksa, Tunarudi hatua hamsini Nyuma, Huoni Mataifa makubwa yaliyoendelea yanavyoulinda uchumi wake wa ndani kwa ushibiti wa uingiaji bidhaa holela
 
Kila kitu Ruksa, Tunarudi hatua hamsini Nyuma, Huoni Mataifa makubwa yaliyoendelea yanavyoulinda uchumi wake wa ndani kwa ushibiti wa uingiaji bidhaa holela
Kama hatuna uzalishaji wa kutosha ...kuagiza nje sio dhambi..ni kumsaidia mwananchi apate bidhaa kwa Bei rafiki...na kuwe na ushindani wa kibiashara..haimaanish kuua viwanda vya ndani...Mbona sisi tunataka kuuza bidhaa nje.
Ni kubalance tu.
 
🐒🐒🐒
imgvfdage12.png
 
Back
Top Bottom