Rais Samia alishauri kuhusu ujenzi huu wa barabara; kwanini TANROADS na TARURA hamumsikilizi?

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,550
1,987
Mama alitoa ushauri kwenu nyinyi Wasimamizi na watengenezaji wa barabara TANROAD/TARURA, ili kuokoa fedha na kuacha kurudia rudia utengenezaji wa barabara za VUMBI kila msimu wa mvua unapoisha ! Basi mzijengee kwa SIMENTI.

Mtindo huu ulipingwa na WALAJI lakini kwa mujibu wa MAMA njia hiyo imekoa fedha na imekuwa Tiba na kufanya vizuri ZANZIBAR.

OMBI, wananchi wa LUGWADU mkoani PWANI wilaya ya MKURANGA tunapakana na TEMEKE pamoja na KIGAMBONI barabara inatutesa MNO.

TUFIKIRIENI na siye kama tunavyowafikiria nyie!! Huku nako kuna WANANCHI wanaopenda maendeleo ya miundombinu ya KUDUMU hizo rasharasha za kuleta vifusi, kuchonga barabara na mitaro ni vitendo VINAVYOUDHI .
 
Weka picha ya barabara tuifanyie tasmini ya matengenezo kijana.
 
Kanda ya ziwa pia, kuna mikoa barabara zake zinachongwa kwa miaka mingi, wakati hiyo hela ingeweza kuweka lami

Rais Samia, naomba ufuatilie hili swala, linaigharimu serikali yako.
 
Back
Top Bottom