GE2025 Rais Samia alipochangiwa fomu ya urais na wananchi Dodoma

GE2025 Rais Samia alipochangiwa fomu ya urais na wananchi Dodoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, akiwa njiani kuelekea ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu kuelekea ya Urais, Wananchi wa Chamwino wamemchangia Tsh. 200,000.

Baada ya kuchangiwa, Rais Samia amesema “Nawashukuru kwa kuja kuniunga mkono katika safari hii ninayoanza ya kwenda kukisemea Chama chetu ili tupate ridhaa ya kuongoza tena nchi yetu, leo tunakwenda kuchukua fomu nitakuja mnidhamini ili tuanze ile safari sasa.



 
Rais Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 9, 2025 amechukua fomu ya kuwania muhula wa pili wa Urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (#INEC) akiwa ameongozana na Mgombea Mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambao wanajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Screenshot_20250808-135021~2.png
 
Chukueni hii hela wekeni mafuta kwenye yale mabasi, chukua na hii laki mbili uwape watu wajidai wananisimamisha njiani wanichangie, alafu yale mabus jaza watu wajifanye wananisindikiza, na zile pikipiki zetu si zipo chukua hii posho na hela ya mafuta wape wajidai wananisindikiza pia
 
Tukumbuke tu wadau wa michezo saa 7 kamili mchana huu kutakuwa na droo ya CAF ikifanyika live na kwa mara ya kwanza kutoka Dar es Salaam kupitia Azam Sports 1 HD, burudani kwa wote. Karibuni sana kuangalia maana ndiyo furaha yetu nyingine ipo huko, baada ya ile ya nyumbani.
 
Nawaza tu, zile taasisi zilizochanga pesa kwa ajili ya kuchukulia fomu zimekwenda wapi kwa sasa, unafiki mwingine bwana
 
Hao Matonya Waliandaliwa Tu
Hapo Jioni Wanaenda Kulipwa Ofisi Ya Chama.
#drama Za Ccm.
 
Wa pili upi? Kwani wa kwanza ulikua upi? Yeye si alidandia Treni ya Magufuli?
Magufuli aliongoza miezi mitano tu ya muhula wake wa pili akaaga dunia, Samia ameongoza muhula mzima wa JPM na sasa anamalizia muhula wake wa pili.

Angekuwa kaingia ikulu miaka hii miwili au huu mmoja wa mwisho asingethubutu kugombea urais angekuwa keshamaliza muda wake.
 
Akivuta Huyu mama kuna watu watakesha usiku kucha wakibubujikwa machozi ya furaha
 
Akivuta Huyu mama kuna watu watakesha usiku kucha wakibubujikwa machozi ya furaha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom