Rais Samia alifanya kosa la kiufundi

Rais Samia alifanya kosa la kiufundi

Katiba yetu inasema wazi kuwa Rais atakoma kuwa Rais mara anapofariki. Dakika ile anapofariki tu, Urais wake umeishia pale. Hafi, akiwa umeubakiza Urais nyuma kiasi cha kuweza kukasimisha kwa mtu mwingine.

Rais akifa, Katiba yetu inasema kuwa aliyekuwa Makamu wake, ataapishwa kuwa Rais. Atakuwa Rais kumalizia kipindi kilichobakia kufika muda wa uchaguzi unaofuata. Katiba haisemi kuwa Makamu wa Rais ataapishwa kumalizia kipindi cha Urais wa Marehemu kwa sababu Marehemu akishakufa, hana Urais wake aliouacha.

Kama Urais wa marehemu umekoma, basi na Serikali yake, kimantiki imekoma. Ili uunde Serikali mpya, ni lazima uanze kwa kumpendekeza Waziri Mkuu, na kisha kwa kushirikiana na Waziri mkuu, Rais auende Baraza la Mawaziri. Rais Samia hakufanya hivyo. Kama alitaka kuendelea na Majaliwa kama Waziri Mkuu, alistahili kumteua tena, kisha ashirikiane naye kuunda Baraza la Mawaziri.

Kwa kutokufanya hivyo, ndiyo maana watu wengine wanasema kuwa hii ni Serikali ya Magufuli, na Samia anamalizia awamu ya Magufuli, yaani anamalizia Urais wa Magufuli. Jambo ambalo siyo kweli, Rais akishakufa Urais wake umekomea pale, Serikali yake imeishia pale.

Rais Samia kwa kutomteua Waziri Mkuu na kuteua Baraza la Mawaziri akishirikiana na Waziri Mkuu, kumefanya baadhi ya mawaziri vichwamaji kuamini kwamba wanatumikia serikali ya Magufuli, na Magufuli ndiye aliyewateua (japo ni Samia aliyewateua tena kwa tittle zile zile na wengi kwa nafasi zilezile). Hawa royalty yao ipo kwa marehemu, japo hayupo, kuliko kwa Rais Samia, na hawa ndiyo mchana wanamsifia Samia, usiku wanasema Samia hana uwezo.

Ushauri
Rais Samia, kama anataka kufanikiwa, ni lazima ateue serikali yake ya awamu ya 6.

Katiba ipo wazi, Rais akifariki, Makamu wake anakuwa Rais. Ni Rais kamili, hamalizii uongozi wa marehemu, ambao kimsingi unakuwa haupo, anakuwa Rais kamili kama Rais aliyechaguliwa kwa kura.

Katiba inaeleza namna ya kumpata Rais baada ya aliyekuwepo kufariki, lakini haisemi kuwa atakaimu nafasi ya marehemu au atapungukiwa mamlaka au kulazimika kufuata chochote cha mtangulizi wake, isipokuwa katiba.

Kuna watu hawataki kuamini kuwa Rais aliyekuwepo, sasa hayupo, na alipofariki hakuacha mamlaka yoyote nyuma. Amefariki, na mamlaka yake yameishia pale. Hawaamini kuwa Samia yule akiwa makamu wa Rais, ambaye walimwona hana uzito wowote kwa sababu walikuwa wanaripoti moja kwa moja kwa Magufuli, sasa ndiye mkuu wa nchi na ndiye mkuu wao aliye na uwezo wa kumteua yeyote amtakaye na kumwondoa mteuliwa yeyote.

Hawa wanafanya jitihada nyingi usiku na mchana, kuthibitisha kuwa Rais Samia hana uwezo. Wakimshauri, wanamshauri wakiwa na hila. Bila shaka, na kwa uwezekano mkubwa, baadhi yao ndio walimshauri Rais aidhinishe kukamatwa kwa Mbowe na kumbambikizia kesi ya ugaidi Mbowe na makomandoo, wakijua hilo litamchafua sana na kupoteza uungwaji mkono mkubwa ulioanza kuonekana kutoka vyama vya upinzani.

Rais Samia, sasa anatakiwa kufikiria kwa umakini sana anaposhauriwa. Lengo la hawa washauri wenye hila ni kutafuta kila namna ya kumtenganisha na wananchi. Kwa hili la Mbowe, wamefanikiwa sana. Maana mamilioni waliokuwa wakimwunga mkono Rais Samia, kulala la kuamka wakaanza kumlaani sana.
Rais SSH ametumia busara na hekima kubwa kuliko akili yako inavyokuongoza. Mazingira aliyochukulia Serikali hayakuwa rafiki kama unavyoona kwenye vyombo vya habari.

Kulikuwa resistance Samia asiwe Rais kutoka kwa genge lililokuwa na nguvu wakati wa Magufuli. Isingekuwa kwa busara na hekima za Chief of Defence Forces sasa hivi Rais angekuwa Ndugai au Bashiru Ally au Chamuriho.

Mama yuko very calculative, muacheni aupige mwingi kwa staili yake
 
Rais akifariki serikali haifi. Baraza la Mawazi4i na Mawaziri wote bado wanaendelea na uwaziri wao kama kawaida. Makamu wake anapandishwa kuwa Rais na anaikuta serikali halali ikiendelea na majukumu. Hicho ndicho alichokiona Rais Samia.

Anaweza kuamua kuivunja rasmi kwa kulivunja baraza la mawaziri ili aanze upya akipenda.

Endapo ataona vinginevyo anaweza kuendelea na mabadiliko madogo madogo ya hapa na pale mpaka awamu yake itakapomalizika kwa mujibu wa katiba.
 
Back
Top Bottom