Rais Samia aagiza tozo za mafuta kupunguzwa

Rais Samia aagiza tozo za mafuta kupunguzwa

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,517
Reaction score
6,074
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameelekeza kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na Taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta hapa nchini zenye thamani ya Sh102 bilioni kwa mwaka, kwa lengo la kupunguza bei za mafuta na kuwapa unafuu wananchi.

Rais Samia ametoa agizo hilo leo Jumanne Oktoba 5 , 2021 wakati akipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Nishati, January Makamba kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Wizara hiyo kupitia mwenendo wa biashara ya mafuta na bei zake hapa nchini.

Taarifa iliyotolea na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imeeleza kuwa utekelezaji wa maagizo hayo unaenda sambamba na marekebisho ya kanuni mbalimbali zinazohusiana na tozo na kuchapishwa katika gazeti la Serikali leo Oktoba 05, 2021.

Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia amechukua hatua ili kukabiliana na upandaji wa bei za mafuta katika soko la dunia, ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikipanda kwa kiwango kikubwa na kuathiri watumiaji wa bidhaa hiyo hapa nchini.

“Taasisi zinazoguswa na maelekezo haya ni, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (tozo ya miundombinu), Mamala ya Mapato Tanzania (tozo ya kuchakata taarifa), Shirika la Viwango Tanzania (tozo ya kupima ubora wa mafuta kwenye meli na gharama ya uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta),”

Taasisi nyingine Wakala wa Vipimo Tanzania (tozo ya uhakiki wa ujazo wa mafuta melini), Wakala wa Usimamizi wa Meli (tozo ya forodha) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (ushuru wa huduma kwenye Halmashauri nne zenye maghala ya kupokea mafuta kwa jumla). Halmashauri hizo ni Kigamboni na Temeke za Jijini Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Aidha, Rais Samia pia ameagiza ufanyike mchakato wa haraka wa kupeleka marekebisho ya Sheria Bungeni zinazohitaji marekebisho ya haraka leo.
 
Tusubiri utekelezaji na matokeo yake, tutarudi kuchangia.
 
Labda itasaidia kupunguza ongezeko la bei za vitu (mfumuko wa bei)
 
Sidhani kama itapunguza bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa. Faida kubwa itabaki kwa kampuni na wauzaji wa mafuta.
 
Ni siasa tu hizo, kwani wakati wanapandisha hawakujua nini.
 
Kwani ni nani aliyeidhinisha hizo tozo?

Utasikia Mataga wanavyo piga makofi na kusema Raisi msikivu,kana kwamba hizo tozo ziliwekwa na Chadema.
 
Asante Mh Rais SSH kwa maamuzi yako haya. Mafuta yanagusa uchumi kwa namna ya kipekee. Ahueni ya bei ya mafuta itagusa maisha ya wengi. #tag JMT kazi Iendelee.
 
Sidhani kama itapunguza bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa. Faida kubwa itabaki kwa kampuni na wauzaji wa mafuta.
Kwa hiyo wauzaji wa mafuta wasipate faida mkuu, au una maana gani kusema hivyo?

Tozo na kodi kwenye mafuta ni nyingi, huyo muuzaji anapata kawaida tu, sidhani kama ni faida kubwa kiasi hicho, serikali ndio inachukua tozo na kodi zisizohesabika.
 
Wapate lakini si kwa kumkandamiza mtumiaji wa mwisho.
 
Kwa hiyo wauzaji wa mafuta wasipate faida mkuu, au una maana gani kusema hivyo?

Tozo na kodi kwenye mafuta ni nyingi, huyo muuzaji anapata kawaida tu, sidhani kama ni faida kubwa kiasi hicho, serikali ndio inachukua tozo na kodi zisizohesabika.
Huyu Rais wetu anapata taabu Sana...mijitu inaongeza tozo itakavyo...halafu Rais analazimika kuingilia Kati..
 
Back
Top Bottom