Hapo umeongea vya maana kidogo. Mtu lazima ujue pale unaposhindwa halafu utafute njia zingine. Ni kama pale unapofanya mtihani. Kama kuna swali gumu limekushinda huwezi tuu kung'ang'ania kulijibu mpaka muda unakwisha. Liruke tuu hilo swali halafu jibu mengine. Kuna watu wengi majuu wameshindwa lakini bado wanang'ang'ania. Nasema tumia formula hii kujua kama maisha ya majuu yamekushinda. Kama upo US unafanya kazi huendi shule halafu mshahara wako wa ni chini ya dola USD 85,000 kwa mwaka, wewe umeshindwa. Tafuta plan B au rudi bongo. Using'ang'anie tuu Marekani. Maisha ni mafupi sana. Ukilala ukiamka utajikuta ujana umekupita wewe bado unayakimbiza maisha ya Marekani. Msikae tuu kuishi ma ghetto, watoto wenu wanaenda shule za wajinga wajinga maana US shule za watoto zinaenda na unakoishi. Ukiishi mashenzini na shule za watoto wako zitakuwa ni zile zile za wachovu. Tena sasa hivi uchumi wa Marekani uko dhoofu, ni muda mzuri sana wa wewe kufunga virago. Tena hakuna atakayekulaumu au kukucheka. Maana wengi wanataabika siyo wewe tuu.
Hadithi za vijiweni zitakwisha lini? Hivi unaijua thamani ya dola? USD 85,000 unaijua au umepata wepesi wa kuaindika? Daktari aliyemaliza majaribio na kuanza kazi hatengezi USD 85,000 mkiwa kwenye hivyo vijiwe vya kahawa uliza kwanza; hivi kwa akili inakujia ukishindwa na maisha Marekani ya bongo utayaweza? Msipoteze muda kuandika vitu msivyovijua Marekani maisha tambarare asiyefanya kazi jua fika hataki kufanya kazi.
Chama
Gongo la Mboto DSM