Rais Obama awakataza uhamiaji kurudisha 'young illegal immigrants'!...Wabeba maboksi wenzangu mpo?

Mkuu Zomba hiyo ni kweli kabisa nina ndugu kakimbilia USA miaka 15 iliyopita karejea nyumba mwaka jana Dec na jeans akidhani ni kitu cha maana sana.Mbaya zaidi kakuta Ndugu,jamaa na marafiki wengi wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Mwaka jana nilitembelea huko, nimeongea na baadhi ya Watanzania, niliowakuta kwenye hali nzuri ni wale ambao nawajuwa walienda kusoma na wakasoma kiukweli, lakini wale walioingia kutafuta maisha na wakawacha kusoma, nimewakuta hali ni mbaya sana, kuna mmoja au wawili nikawauliza kwanini hamrudi? mmoja akasema "aah kaka, nirudi hivi si aibu, baada ya miaka 15 sina hata nyumba nyumbani, bora nifie hukuhuku tu". Mwingine akanambia anataka kuvuka border aende akajaribu Canada maana hapo sasa kashindwa, huyu yupo US kwa miaka 8.

Kusema kweli wengi wanasikitisha. Kuna mmoja nilimkuta New York, huyu alikuwa wa kike na ana maisha mazuri kwa kwango cha wengine, nae hana kazi. Nikaambiwa kinachomsaidia ni kuwa aligunduliwa ana UKIMWI na ukiwa na hilo gonjwa huko Serikali inahakikisha hulisambazi kwa hiyo wanakuhudumia kwa kila kitu kuliko wale disables.
 
Hana jipya huyu haya ujumbe wa nyumba kumi kumi hastahili achilia mbali kuwa rais wa nchi. Wewe unaona hivyo lakini nchi inazidi kudidimia kimaendeleo na uko ushahidi wa kutosha kuhusu hili. Elimu yetu ni hoyo na kila kitu chetu nchini ni hovyo hakuna hata kimoja ambacho Watanzania tunaweza kujivunia kwa sasa.

Ni mmoja wao nini wa wanaoshindwa kurudi TZ kwa kuwa huna pakufikia na itabidi ufikie kwa shemeji?
 
Waliokuwepo kabla yake walifanya nini zaidi yake? mimi naona yeye ndiye anafanya kila kitu zaidi yao. Nyerere miaka 24 aliikuza elimu? Kikwete anaiua 83/17 na ndio chuki zenu kwake.

Hakuna kimoja utakachonionesha ambacho Kikwete hajakifanya zaidi ya yeyote aliyekuwepo kabla yake, si Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Mkoloni wao pamoja.

Hebu tuwekee aliyoyafanya msanii Kikwete tangu alipoingia madarakani mwaka 2005 ambayo Watanzania wanastahili kujivunia.
 
Hebu tuwekee aliyoyafanya msanii Kikwete tangu alipoingia madarakani mwaka 2005 ambayo Watanzania wanastahili kujivunia.

Wewe weka yaliyofanywa kabla yake mimi ntakuonesha kafanya nini.
 
Ni Kweli Viongozi Wakijua huku hutuambia maneno ya uongo na hata maswali hawataki kuulizwa wanakimbia Maswali tena mnaambia musimuulize Maswali kiongozi Wenu yeye hakuja kuulizwa Maswali atakachowaambieni pigeni tu makofi mushangilie uongo mtupu Siasa ya Tanzania ni ya wizi na uongo mtupu Sera za chama tawala zimeipitwa na wakati bora tungojee chama kingin tuone Sera zake zitalata Maendeleo? ninakukubalia unavyosema mkuu@BAK

Mkuu MziziMkavu waruhusu kuulizwa maswali waadhirike? Wakati mwingine wanakuja na za kuleta eti ratiba yetu iko very tight hivyo hatuna muda wa kujibu maswali...Daaaa!
 
Last edited by a moderator:
Wewe weka yaliyofanywa kabla yake mimi ntakuonesha kafanya nini.

Asingeitwa msanii kama alifanya mambo ambayo Watanzania wanastahili kujivunia. Asingechachamaliwa na Wabunge kufukuza Mawaziri wake kama Wabunge wa Magamba wangemuona ni Kiongozi anayetenda kazi zake.
 
Hao Watanzania wanaozamia huko ni Watumwa mambo leo. Nimewakuta wengi sana US na UK, wengi wao wana maisha ya taabu kuliko hapa nyumbani. Kinachowashinda kurudi mara nyingi huwa ni uoga wakuwa "failures" wameshindwa kimaisha Tanzania wakaona huko ndio watafanikiwa, kufika huko nako wameshindwa, kwani walifikiri maisha bora yanaletwa bila kufanya kazi.

Nnakuhakikishia anaefanikiwa Tanzania hata akienda huko pia atafanikiwa lakini anaeshindwa Tanzania hata aende wapi hatoweza. Tanzania kuna fursa nyingi sana kwa anaejituma.

Nani ana maisha ya tabu Marekani au UK kuliko mtu wa bongo? Au wewe unazungumzia bongo ya vigogo? Kama bongo ya vigogo sawa lakini bongo ya watu baki huwezi kulinganisha.
 
Having "bebad" magunia ya mazao Kogelo, Obama is no stranger to maisha ya "mswahili". Hapa ni zaidi ya Latino /Cuba vote.
 
Nani ana maisha ya tabu Marekani au UK kuliko mtu wa bongo? Au wewe unazungumzia bongo ya vigogo? Kama bongo ya vigogo sawa lakini bongo ya watu baki huwezi kulinganisha.

Kuwa mbali tu na kwenu kwa miaka 20 huna hata banda la kuku kwenu, wakati unapewa kula ya handout hiyo ni shida kubwa sana kama huelewi.
 
Nani ana maisha ya tabu Marekani au UK kuliko mtu wa bongo? Au wewe unazungumzia bongo ya vigogo? Kama bongo ya vigogo sawa lakini bongo ya watu baki huwezi kulinganisha.

Mkuu...Nakwambia mie ninayo....12yrs ago mie na wenzangu 3 tulikwenda US uko for a simple tour at the same time kuangalia kama uwezekano wa kukaa uko upo...kwa bahati nzuri ilishindikana kwangu na wengine walipata.

Nikarudi tanzania na kukomaa na maisha na shule zetu hizi...kwa sasa wenzangu hawana hata banda nyumbani japo kuwa walinunua shamba la hekali 5 kila mmoja na kupata umili na eneo hilo kwa sasa limekuwa makazi lakini wameshindwa hata kumili tofali moja kila napo wauliza wanasema wana save watajenga. Imekuwa ni 6yrs now. Wakija likizo wako very limited na time ya kukaa nyumbani kuliko utumwani. Jamani kwa exposure kidogo mliyo pata mnaweza kufanya mengi nyumbani..Naamini kama umepata degree au diploma ya jambo flan ambalo lini apply tanzania na unajua kuitumikia elimu yako karibu nyumbani na utaweza kutoka kimaisha.

Angalia blog ya mjengwa graduate mmoja alikosa kazi for years akaamua kufunga kuku sasa anamili nyumba japo haijaisha huyu in next 2yrs atakuwa na gari.

Karibuni Nyumbani wakuu...Ntakuwa uko for vocation next week....nafurahi kuja kama mtalii na sio kutafuta maisha.
kmdh,Ogah,BAK
 
Mkuu Zomba hiyo ni kweli kabisa nina ndugu kakimbilia USA miaka 15 iliyopita karejea nyumba mwaka jana Dec na jeans akidhani ni kitu cha maana sana.Mbaya zaidi kakuta Ndugu,jamaa na marafiki wengi wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Mkuu Ngongo.
Ukienda UK mpaka wanatia huruma kuna mji mmoja unaitwa Milton Keynes, utadhani upo Kariakoo...kuna kuna vijana wa Dar, Mwanza, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Zanzibar..
 
Last edited by a moderator:
Kuwa mbali tu na kwenu kwa miaka 20 huna hata banda la kuku kwenu, wakati unapewa kula ya handout hiyo ni shida kubwa sana kama huelewi.

Wenzako tukirudi tunafikia Kempinski au Sea Cliff wewe unaongelea banda la kuku? Halafu handout mbona mpaka bongo wanategemea? Kuna USAID, na ma NGOs kibao bongo. Hizo nazo si handout au?
 
Wenzako tukirudi tunafikia Kempinski au Sea Cliff wewe unaongelea banda la kuku? Halafu handout mbona mpaka bongo wanategemea? Kuna USAID, na ma NGOs kibao bongo. Hizo nazo si handout au?

Muone mshamba huyu, unarudi kwenu unafikia hoteli?
 
Mkuu...Nakwambia mie ninayo....12yrs ago mie na wenzangu 3 tulikwenda US uko for a simple tour at the same time kuangalia kama uwezekano wa kukaa uko upo...kwa bahati nzuri ilishindikana kwangu na wengine walipata.

Nikarudi tanzania na kukomaa na maisha na shule zetu hizi...kwa sasa wenzangu hawana hata banda nyumbani japo kuwa walinunua shamba la hekali 5 kila mmoja na kupata umili na eneo hilo kwa sasa limekuwa makazi lakini wameshindwa hata kumili tofali moja kila napo wauliza wanasema wana save watajenga. Imekuwa ni 6yrs now. Wakija likizo wako very limited na time ya kukaa nyumbani kuliko utumwani. Jamani kwa exposure kidogo mliyo pata mnaweza kufanya mengi nyumbani..Naamini kama umepata degree au diploma ya jambo flan ambalo lini apply tanzania na unajua kuitumikia elimu yako karibu nyumbani na utaweza kutoka kimaisha.

Angalia blog ya mjengwa graduate mmoja alikosa kazi for years akaamua kufunga kuku sasa anamili nyumba japo haijaisha huyu in next 2yrs atakuwa na gari.

Karibuni Nyumbani wakuu...Ntakuwa uko for vocation next week....nafurahi kuja kama mtalii na sio kutafuta maisha.
kmdh,Ogah,BAK

Sasa unataka wajenge bongo wakati wao wanakaa Marekani si ni kupoteza hela huko? Kwani wameshaamua kurudi nyumbani? Wakiamua kurudi wanaweza kujenga au hata kununua nyumba iliyosha jengwa.
 
Back
Top Bottom