Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,527
- 34,366
Hujaona mantiki yake au hujaelewa maudhui yake!!sijaona mantiki ya bandiko lako.
Kuna dhana imekomazwa kwenye akili za Watanzania na kugeuka kuwa ni utamaduni wetu kwamba Rais tunaemchagua akishaapishwa anageuka kuwa Bosi wa kila mtanzania jambo ambalo si sahihi.
Kwa mujibu wa Katiba yetu Rais anakuwa ni mtumishi namba moja wa nchi hii anayechaguliwa ili kuisimamia serikali (Siyo wananchi) kwa lengo la kuleta maendeleo kwa taifa kwa ujumla!
Rais anaweza kuogopwa na wale walioajiriwa kwenye serikali na taasisi zake pamoja na taasisi zingine za Umma, lakini haiyumkini Rais akaogopwa na Raia waliomchagua ambao kimsingi ndiyo mabosi wake. Na ndiyo maana wananchi wa kawaida hawahitajiki kusema hela wanazozipata wamezitumiaje wakati serikali inapaswa kutoa taarifa fedha wanazozipata kwa njia mbali mbali wanazitumiaje kwa kuwa wao pamoja na Rais ni watumishi wa Umma na wala siyo Umma ni watumishi wa waliio serikalini Rais akiwemo!
Hii inawezekana tu, katika nchi zile ambazo kuna Demokrasia ya kweli.
"A government afraid of its citizens is a Democracy. Citizens afraid of government is tyranny!" Thomas Jefferson
Hii inawezekana tu, pale kwenye uwajibikaji wa kweli upo. Nchi nyingi za kiafrika zinafanya kinyume kidogo na ulichokiosema katika uzi wako, kuna tofauti kubwa kati wa msimami na mtawala!
sijaona mantiki ya bandiko lako.
Mi nashangaa kila sekunde anasema mimi ndo Rais, mimi ndo Rais... Sijui ana mtishia nani!!
Si kila mwananchi ni serikali ingawa serikali inatarajiwa itokane (Si lazima iwe hivyo) na wananchi. Neno "bosi" ambalo tumelitohoa toka kwenye lugha ya Kiingereza kwenye Mkutadha wa hoja hii limetumika kuonesha nani anamsimamia nani!!Hiyo ni dhanna potofu.
Kama unadhani mwananchi siyo serikali basi uelewe kuwa serikali bila wananchi hakuna.
Kwanza ni nini maana ya "bosi", kuna kila uwezekano hauelewi maana ya "bosi" ni nini jinsi ulivyoandika.