Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,260
- 39,495
Ninashawishika sasa kuamini kwamba lawama tunazomtwisha Rais ni kumuonea.
Rais anatokea kwenye jamii, anayoyafanya ndiyo desturi za jamii hiyo. Mnapoona tunapata rais ambaye anakandamiza demokrasia na uhuru wa habari ni kwa sababu jamii hiyo ndivyo ilivyo.
Watu wanapotea, wanachinjwa, wanabambikiziwa kesi ni aina ya uongozi uliomea Afrika kwa kiwango kikubwa.
Jiulize wewe uliye ndani ya familia, unadumisha demokrasia na uhuru wa maoni? Je, unaposema jambo lako linajadilika au ndo maamuzi ya mwisho?
Je, unapopita mtaani ukasikia kelele za mwiziii mwiziii kisha akakamatwa umewahi kuona watu wanamhoji mwizi na kumpeleka polisi au hukumu inapitishwa bila kuhoji na anauawa?
Ukikuta mtu amemtongoza mwenza wako, nini kinakuja akilini mwako kwanza kabla ya yote?
Hivyo nawaasa kama jamii, mkitaka rais na viongozi bora wa kesho, anza sasa kutengeneza watoto wenu wawe reasonable and balanced kwenye maamuzi yao ya kila siku.
Mnapomsuta Rais ni kujisuta wenyewe kwani garbarge in garbarge out ndo mtindo tunaoendelea nao.