VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Wazungu wana msemo wao: "courtesy begins at home". Yaani, kama una la kufanya, anzia nyumbani. Kama ni kusafisha na kuonesha kuwa unakerwa au kufurahishwa na jambo fulani, pakuanzia pawe nyumbani. Hakuna haja ya kugawa mema kwingineko halafu uparuke nyumbani. Nyumbani kwanza. CCM kwanza, kwingine baadaye.
Rais na Mwenyekiti wangu, Dr. Bashiru Ally na timu yake wameshakukabidhi Ripoti juu ya Mali za chama chetu cha Mapinduzi (CCM). Si siri tena kuwa kwenye Ripoti hiyo kumeanikwa ubadhirifu na ufisadi mkubwa. Kuna 'mchwa' wa kutosha na kutisha. Wameanikwa watu, taasisi na makampuni yanayotafuna mali za CCM.
Ripoti ya timu ya Dr. Bashiru Ally imeanika hali halisi chamani. Imeanika hali halisi nchini. Kutamalaki kwa rushwa, ubadhirifu na ufisadi. Kutamalaki kwa wanaofaidi keki ya chama na taifa kwa ujumla huku wengine wakishindia embe mbichi na maji. Kutamalaki kwa wezi na wanaoiona Tanzania kama nchi yako binafsi. Kutamalaki kwa wanaojichora kama kila kitu.
Muda sasa umefika. Muda sasa umewadia. Wa kushughulikiwa. Wa kuambiwa kwa maneno na matendo kuwa wao si lolote wala chochote chamani na serikalini. Kuambiwa kwa sauti kali na matendo yenye maumivu kwao kuwa wao si wamiliki wa chama wala serikali. Waambiwe kuwa wao si wajanja kuliko sisi sote wengine. Kwa matendo.
Rais na Mwenyekiti wangu, najua uliingia madarakani kwa sera ya kupambana na kutokomeza rushwa, ubadhirifu na ufisadi. Kutokomeza 'majizi'. Fanya hivyo sasa. Washughulikie hao wetu kwanza. Onesha mfano kwa hao. Wakabidhi kwa vyombo vya usalama; wapelelezwe; washtakiwe na wafungwe. Kuwaadhibu kichama tu haitoshi. Wizi ni jinai. Si jambo la kisiasa.
It is now or never!
Makongoro Nyerere hakuomba vyeo anavyomiminiwa sasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa Buyungu, Kigoma)