MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Tanzania imeendelea kutambulika katika uso wa Afrika na Duniani kote!
Tutakumbuka kuwa Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi aliteuliwa kuwa Kiongozi wa Waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwenye Uchaguzi Mkuu wa Uganda ambao umemaliza majuzi. Na ninaamini kama isingekuwa umri wake, kwa sasa angekuwa kwenye majukwaa ya kimataifa kama msuluhishi wa migogoro ya kisiasa kama alivyokuwa anafanya katika mgogoro wa Zanzibar.
Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuangaza huku na kule, wamemuona Mzee Mkapa anafaa sana kuwa msuluhishi wa kisiasa nchini Burundi.
Ikumbukwe pia viongozi wakuu wa Afrika waliangaza Afrika yote na kumuona Mzee Kikwete. Februari mosi, mwaka huu walitutangazia kuwa Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete, ameteuliwa na Umoja wa Afrika (AU) kuwa mwakilishi wake katika kusuluhisha mgogoro wa Libya.
Hata kwenye mgogoro wa Kenya, Mzee Mkapa na Kikwete walifanya kazi ya ziada mpaka Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wakatia saini makubaliano ya kugawana madaraka na hivyo kumaliza mzozo wa kisiasa uliozuka baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais mwezi Desemba mwaka 2007.
Hii ni heshima kwa taifa na pia ni kigezo katika feedback/taswira kuhusu mtazamo wa mataifa mengine kuhusu uwezo wa Tanzania na viongozi wake katika majukwaa ya usuluhishi wa kisiasa.
Alichokianzisha Mwl. Nyerere katika majukwaa ya siasa za kimataifa, Marais waliofuata wanakiendeleza...