Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 735
- 476
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa matukio mbali mbali yakiwemo kushuka kwa kiwango cha hali ya usalama husababisha kuporomoka kwa utalii.
Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Kikosi cha Polisi wa Utalii na Diplomasia, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Katika hotuba yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa baadhi ya nchi zimepoteza watalii baada ya kushuka kwa kiwango cha hali ya usalama pamoja na mambo mengineyo yakiwemo kutokea kwa machafuko ya kisiasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe, miripuko ya maradhi na majanga.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba uanzishwaji wa Kikosi cha Polisi wa Utalii kwa madhumuni ya kulinda na kuimarisha usalama wa watalii ni hatua muhimu na inayoendana na dhamira ya kuhakikisha watalii na wageni wanaoitembelea Zanzibar wako salama na wakirejea kwao wanakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza kwa mambo mazuri.
Hivyo, alitumia fusra hiyo kwa kuwataka viongozi watakaopewa dhamana ya kuongoza Kikosi hicho wajifunze kutokana na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Kikosi kilichofanana na hicho kilichokuwepo hapo awali.