Rais Mwinyi: Kushuka kwa kiwango cha hali ya usalama husababisha kuporomoka kwa utalii

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
732
475
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa matukio mbali mbali yakiwemo kushuka kwa kiwango cha hali ya usalama husababisha kuporomoka kwa utalii.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo katika uzinduzi wa Kikosi cha Polisi wa Utalii na Diplomasia, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar.

Katika hotuba yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa baadhi ya nchi zimepoteza watalii baada ya kushuka kwa kiwango cha hali ya usalama pamoja na mambo mengineyo yakiwemo kutokea kwa machafuko ya kisiasa, vita vya wenyewe kwa wenyewe, miripuko ya maradhi na majanga.

Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba uanzishwaji wa Kikosi cha Polisi wa Utalii kwa madhumuni ya kulinda na kuimarisha usalama wa watalii ni hatua muhimu na inayoendana na dhamira ya kuhakikisha watalii na wageni wanaoitembelea Zanzibar wako salama na wakirejea kwao wanakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza kwa mambo mazuri.

Hivyo, alitumia fusra hiyo kwa kuwataka viongozi watakaopewa dhamana ya kuongoza Kikosi hicho wajifunze kutokana na mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Kikosi kilichofanana na hicho kilichokuwepo hapo awali.
 
Waaambie hao wavaa kobazi na nusu surual kuwa jihadi haisaidii kitu kwa maisha ya sasa ,mitume walishaondoka sisi tufanye yetu mambo ya dola ya kiisilam haitadaidia maisha ya sasa

USSR
 
Yeye Mwinyi ndo anaona kuna hatari ya kiusalama, bado uongo mwingine huo, agenda hiyo tunaifahamu kilichojificha nyuma yake, naye SSH ameishatangaza majeshi yalinde mito, na mtaajiri askari wengi tu kwa sababu za kiusalama mnazozijua, hata ugaidi wa Osama ulikuwa ni uongo ili mpeleke vita Mashariki ya kati na Asia na kusababisha mamilioni ya Innocent civilian kuuwawa kwa sababu zenu za kupambana na ugaidi.
 
Ufaransa na Brazil kuna vibaka hatari kule na watalii kila leo wanakwenda India kuna vibaka hatari na watalii wanakwenda. Zanzibar wala urojo na ubuyu na haluwa Leo wanaundiwa na jeshi la watalii na makamera kila kona.

Kuna viongozi wana akili za kitumwa kweli mwananchi ndio wakupewa ulinzi mzuri na ajira ili kodi yake iweze kuiendesha serikali. Lakini kwanza mgeni ana thamani kuliko mwenyeji afrika kuna akili hata shetani ana shangaa.

Lunatic
 
Ufaransa na Brazil kuna vibaka hatari kule na watalii kila leo wanakwenda India kuna vibaka hatari na watalii wanakwenda. Zanzibar wala urojo na ubuyu na haluwa Leo wanaundiwa na jeshi la watalii na makamera kila kona...
Vile vile huduma za zima moto ziimarishwe.
 
Waaambie hao wavaa kobazi na nusu surual kuwa jihadi haisaidii kitu kwa maisha ya sasa ,mitume walishaondoka sisi tufanye yetu mambo ya dola ya kiisilam haitadaidia maisha ya sasa

USSR
Jinga kubwa.
 
Back
Top Bottom