Rais Mtuele: Obama, Mbowe Vs Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Mtuele: Obama, Mbowe Vs Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Jan 21, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Siku 100 za Kikwete: Tumeona umuhimu wa Rais Mteule

  na
  David Kafulila Jr.

  Hadi sasa mengi tayari yameshasemwa kuhusiana na siku 100 za Kikwete, mazuri na mabaya karibu yote yameanikwa hadharani. Ninadhani kwa mazuri kuanikwa hadharani, kutatusaidia tuzidi kusonga mbele zaidi katika hayo kwa upande mmoja. Na kwa kwa mabaya yaliyojitokeza kutatuwezesha kutafakari upya juu ya uelekeo muafaka wa kukabiliana nayo badala ya kuzidi kwenda kasi huku tukiwa katika njia iendayo shimoni.

  Nimeamua kutumia neno “sisi kama Watanzania” badala ya yeye (Rais) kama ambavyo Watanzania wengi tulivyozoea , kwa sababu jambo ni kweli kuwa, mafanikio ya siku 100 za Rais aliyepo madarakani hutegemea vilevile mchango wa kila raia, ni jumla ya jitihada (intergrated efforts) na si jitihada za taasisi moja au mtu mmoja.

  Naamini huo ndio ulikuwa mtazamo wa Baba wa taifa letu, Mwalimu Nyerere alipenda sana kurudiarudia kauli iliyowahi kutolewa na Rais wa Marekani katika miaka ya sitini, John F. Kennedy ambaye punde baada ya kuchaguliwa aliwataka wamerekani wasiulize Amerika itawafanyia nini? Bali kila Mmarekani ajiulize ataifanyia nini Amerika?

  Ndio maana nahisi ni vema tukajiuliza sisi wananchi tumefanya nini ndani ya siku 100 tangu Kikwete aingie madarakani, badala ya kuuliza upande mmoja wa serikali kuwa umefanya nini? Kwanza sisi halafu serikali. Na kwa kawaida utendaji wa serikali hutegemea mtazamo wa wananchi! Kwanini? Haiwezekani watu wenye mtazamo sahihi kuongozwa na serikali isiyo kubaliana nayo! “Wananchi wasioweza kuiwajibisha serikali yao wakati wowote, wanachangia ubaya wa serikali iliyopo madarakani.”

  Uongozi ni kuonyesha njia, Kikwete kama Rais anawajibu wa kutuonyesha njia, kwahiyo suala la msingi linakuwa ni kwa namna gani Rais amefanikiwa kutuonyesha njia? Je huko tuendako tumejiridhisha kuwa ndiko tunakotakata kwenda au tunaburuzwa?

  Kwahiyo kila upande una wajibu wake na kila upande unayo hoja ya kujibu pindi tunapokwama. Rais atajibu kwa kutuonyesha njia mbaya, waandishi watajibu kwa kututaarifu vibaya, kutupa taarifa za uongo au zilizojaa upendeleo, wachambuzi watajibu kwa kushindwa kutoa hukumu sahihi, kushindwa kuzungumzia masuala ya msingi kwa hofu ya kimaslahi au aibu ya urafiki! Kila mmoja atajibu, walimu watajibu, waganga wa jadi na wakizungu wote watajibu! Na kwa mtindo huo kila mtu atajikuta amejibu.

  Labda baada ya kutoa maoni hayo ya jumla kwa siku 100 za Watanzania tangu awamu ya nne ianze, naomba nirejee kwenye hoja mahsusi niliyoikusudia .

  Kutokana na imani kuwa tayari mengi yamesemwa, na kujadiliwa, nimeoana nitilie mkazo hoja iliyotolewa na Mheshimiwa Freeman Mbowe hasa baada ya kuona kuwa ni hoja mpya na kwa bahati mbaya wengi kwa namna moja au nyingine wameonekana ama kutoijadili au kutoitilia maanani. Katika tamko lake la “siku 100 za Kikwete”. Pamoja na mambo mengine ya msingi, Mheshimiwa Freeman Mbowe aligusia haja ya kuwa na kipindi cha mpito (transition-period) ambapo Rais aliyeshinda atakuwa Rais mteule (haanzi majukumu ya moja kwa moja), kama mbinu ya kumuwezesha kuwa na muda wa kutosha katika kuunda serikali ikiwa ni pamoja na kupitia taarifa mbalimbali za muhimu na masuala mengine nyeti yanayo husu taasisi ya urais ambayo ni kimsingi ni muhimu ayaelewe kabla hajaanza kazi.

  Ni ukweli usiopingika kuwa, kumekuwepo kipindi kifupi mno cha makabidhiano ya Ikulu. Makabidhiano yamekuwa ni ya pupa mno kiasi kwamba laiti Mheshimiwa Kikwete angelikuwa ni mtu ambaye hakuwahi kuwa katika baraza la mawaziri tena kwa muda mrefu, suala hili lingemsumbua sana, angeshindwa kabisa kujipanga vyema ili kuelewa aanzia wapi? Aishie wapi? Na kwa nini? Katika muda mfupi wa namna hii!

  Haiwezekani Rais kuanza kutekeleza majukumu yake punde baada ya kukabidhiwa nchi kupitia gwaride. Taasisi ya urais ni taasisi nyeti, pana na ngumu sana kuindesha hasa katika nchi kama yetu ambayo serikali haina katiba inayojitosheleza. Mifumo na miundo mingi inapangwa na Rais aliyeingia madarakani.

  Kwa mfano, Ni jukumu la Rais kujua ateue mawaziri wangapi? manaibu wa ngapi? Kulingana na agenda zake! Nchi haina agenda! Ni kila Rais na agenda zake. Akimaliza kuweka mfumo huo anaanze kujiuliza nimteue nani katika wizara gani na kwanini? Ndio maana hata Mheshimiwa Rais alipokuwa akilitangaza baraza lake la mawaziri alikiri kuwa kuna baadhi anawaelewa historia yao kiutendaji na wengine hawaelewi kabisa.

  Ndio maana wakati Rais Kikwete alipokuwa akitangaza baraza la mawaziri, katika kile kilichoonekana kama ufinyu wa muda, alisema majina rasmi ya baraza la mawaziri sanjari na wizara zao sijayaandaa rasmi, bado nimeyaandika kwa mkono na nimefuta futa. Sasa hebu tujiulize? Kama Mheshimiwa Rais aliyekuwemo kwenye baraza la mawaziri kwa zaidi ya muongo mmoja alibanwa kiasi hicho, Je ikitokea siku tukampata Rais ambaye atakuwa hakuwahi kuwa waziri, wala hana uzoefu mkubwa na maswala ya ikulu itakuwaje?

  Kwa kweli hatuna budi kuliangalia upya suala hili bila kujali limetolewa na nani au upande gani kwani nchi hii ni yetu sote, na sote tunawajibu wa kuchangia, na unapo kuwepo utawala mzuri tunakuwa na haki ya kusikilizwa. Bila kijali itikadi za dini, siasa, n.k.

  Kauli ya Mheshimiwa Rais kuwa wengine hawaelewi vizuri inamaanisha kuwa haukuwepo muda wa kutosha kuweza kuwafuatilia na kuwaelewa vizuri ili awakabidhi madaraka watu anaowaamini kuwa wanauwezo badala ya kubahatisha. Ni hatari sana kubahatisha katika uteuzi wa nafasi nyeti kama uwaziri! Kuwa na mawaziri wa kubahatisha ni sawa na kuchezea kamari maisha ya Watanzania.

  Hii ndio sababu niliwahi kumpinga jamaa yangu aliyetaka kumrushia lawama Mheshimiwa Rais kutokana na skendo ya umafia wa kisiasa, ambapo vigogo kadhaa wa CCM mkoa wa Kigoma wakishirikiana na naibu waziri wa kazi, Bwana Nsazugwanko siku chache tangu alipokuwa ameteuliwa na Mheshimiwa Kikwete kuwa naibu waziri. Nilimkumbusha rafiki yangu kuwa, “inawezekana Nsazugwanko ni miongoni mwa mawaziri ambao aliwateua bila kuwafahamu vizuri”.

  Lakini hiyo ndio hasara ya kutokuwa na kipindi cha mpito, kwani katika hali kama hiyo Rais anaweza kujikuta ameteua hata wahuni kuwa mawaziri ndio! Kwani siku hizi ubunge si unanuliwa? Nakwani hakuna wahuni wenye pesa? Kama wapo, ikitokea Rais anafanya bahati nasibu kama hii hakuna uwezekano wa watu wa namna hiyo kuukwaa uwaziri? Binafsi nafikiri uwezekano huo upo ndio maana nahisi kuwa kuna haja ya kumpa Rais mteule muda wa kutosha ili kupanga baraza lake la mawaziri sambamba na mambo mengine.

  Nchini Marekani kwa mfano, Baada ya Rais kuapishwa hupewa muda wa miezi kadhaa ili kukabidhiwa ofisi sambamba na kupewa muda wa kuunda baraza la mawaziri kwa utulivu. Labda wengine wanaweza kuhisi kuwa labda Marekani inafanya hivyo kwa kuwa ni taifa lililoendelea na hivyo hatuwezi kuiga toka kwao!

  Ukweli ni kwamba suala hili halihitaji kuendelea kiuchumi bali maendeleo ya uwezo wa kimaamuzi ya msingi. Na hili halipo Marekani au Ulaya pekee. Hata Afrika masuala yanakwenda hivyo. Sote tumeshuhudia namna mwanamama wa shoka, Ellen-Johnson-Sirleaf, Rais wa Liberia alivyopewa miezi kadhaa kwa ajili ya kujiandaa kuanza shughuli za utendaji kama Rais.

  Ndiomaana nahisi kuwa ipo haja ya kuunga mkono utaratibu huo hata kama umetolewa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA ambaye ni mpinzani kwa kuwa una maslahi kwa taifa na wala si kwa chama chochote.
   
 2. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asha, unalosema ni sahihi kabisa. Na kuzingatia muda mrefu wa kampeni za uchaguzi, kuanzia chaguzi kura za ndani ya chama na uchaguzi mkuu, ni wazi kuwa Rais anakuwa amechoka sana baada ya uchaguzi.

  Utaratibu wa Rais wa Marekani kula kiapo umewekwa katika katiba yao. Na kwa ziada, Katiba yao inatamka jinsi Rais atakavyoapa. Naamini kuna sababu za kutosha kabisa kuwafanya waamue kuwa na utaratibu kama huo.

  Hata mimi nimewahi kujiuliza kwanini Katiba yetu inamtaka Rais ale kiapo na kuchukua mamlaka ya u-Rais mara tu anapotangazwa kushinda uchaguzi? Sikupata jibu la maana. Ila naamini kuwa kuna haja na sisi kuwa na utaratibu wa Rais anaemaliza muda wake kuachia madaraka siku ya mwisho wa Mwaka, ama siku nyingineo yoyote (kwa tarehe) itakayoonekana kufaa. Na hapo ndipo Rais mteule ale kiapo na kuchukua madaraka (kama wafanyavyo waMarekani).

  Pamoja na kwamba Rais mteule anatakiwa kuwa amejiandaa kuongoza taifa muda utakapofika, ikiwa ni pamoja na kujua namna serikali anayotaka kuiongoza itakavyokuwa, ila muda huo utampa fursa ya kujipanga vyema zaidi kutokana na matokeo ya uchaguzi (maana Mawaziri ni lazima wawe Wabunge, kwa mujibu wa Katiba yetu).
   
Loading...