Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akutana na Mabalozi

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, akizungumza na Mabalozi mbalimbali wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini, walipofika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo kumpa mkono wa pole kutokana na kifo cha Kaka yake, Suleima Kikwete, kilichotokea hivi karibuni.

IMG_0045.JPG
 
Nimeangalia picha vizuri na kuangalia kicheko cha J.K na hao wanaoitwa mabalozi walivyo na furaha, hakika hawaakisi utamaduni wa misiba ya kiafrika.
 
Wanamuomba amwambie magu aachie kdgo maana ngoma ishakuwa ngumu kwa mabepari wote, biashara zao haziendi
 
Ingekua jk ndio kenda kwa japo mmojawapo ktk hao leo humu pasingetosha!! Lkn wamepigwa butwaa wamebaki kutafuta kasoro za vivazi na sura za bashasha!! Hongera JK kwa uongozi mahiri
Hongera tena? Nyie watu vipi, hata watu kuja kuhani msiba imekuwa jambo la sifa? Sasa itakuwa mnanuombea apate msiba mkubwa zaidi ili atembelewe na maraisi jirani badala ya mabalozi ili mje JF na kutamba sio?
 
Naona mabalozi wa Burundi, Zimbabwe, Rwanda na Uganda wamefurahi sana. Itakuwa anawaelezea habari za jecha
Mkuu hivi kwanini "rais wa mioyo"...hutembelewa na kupewa tunzo na mifano ya vijitaasisi?...mara "wachungaji "200 toka kongo!..mara "wanafunzi" shule za kata,mara "waganga"....hivi PM "uliyestaafu"...unakosa watu credible/genuine kukutembelea?..kuna walakini!
 
Nimeangalia picha vizuri na kuangalia kicheko cha J.K na hao wanaoitwa mabalozi walivyo na furaha, hakika hawaakisi utamaduni wa misiba ya kiafrika.
Unajua kuna umri mtimilifu mtu akifa wala huzuni huwa haipo... Kwa kuwa mtu kaishi umri wake mtimilifu... Misiba inayoleta kilio sana ni ile ya majanga kama ajali na pale mtu anapoondoka katika umri mdogo ambapo uwepo wake ulikuwa unahitajika zaidi...
 
Mabalozi watakuwa wamechoka saana.Dar hadi Msoga ni mbali na barabara siyo nzuri na polisi wa tochi kibao kuongeza pato la taifa.
 
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, akizungumza na Mabalozi mbalimbali wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao nchini, walipofika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo kumpa mkono wa pole kutokana na kifo cha Kaka yake, Suleima Kikwete, kilichotokea hivi karibuni.

View attachment 329726
Alitutangazia kwamba anenda kuishi msonga kumbe bado anaishi jijini!
 
Nimeangalia picha vizuri na kuangalia kicheko cha J.K na hao wanaoitwa mabalozi walivyo na furaha, hakika hawaakisi utamaduni wa misiba ya kiafrika.
Hii picha ingekuwa video walau ya dk 10 ungeweza ku-gauge mood vizuri. Hivi kwa hulka ya JK ulitarajia waanza kulia na picha mnato zionyeshe kuwa wana huzuni? Hivi unapohani msiba ni lazima uonyeshe huzuni badala ya faraja. Hata hivyo, unajua at particular point in time JK ame-crack joke gani ambayo inawezekana kuwaweka wageni kwenye jovial mood!
 
Nampa Pole sana

Hivi JK si aliaga taifa kabisa anaenda Msoga na Helkopta ikawa nje ya Ikulu kwa ajili ya kumuhamishia huko au ilifika Bunju ikakata kona na kurudi Osterbay?
 
Back
Top Bottom