Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi, fedha za Wastaafu wa EAC zilitumikaje?

Scarlet

Senior Member
Mar 28, 2014
116
44
Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi, fedha za Wastaafu wa EAC zilitumikaje baada ya serikali yako kukabidhiwa iwalipe? Naam, hilo ndilo swali lililoumiza vichwa vya wengi na linalohitaji majibu mkiwa bado mko hai...miaka 40 ni mingi hivyo funguka Mzee Rukhsa!

Sehemu ya kwanza...

Naanza kwa kutoa historia fupi ya iliyojulikana kama Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community iliyoundwa mwaka 1967 na kuvunjika miaka kumi baadaye 1977.

Ushirikiano kati ya nchi tatu katika ukanda wa Afrika Mashariki, wakati huo zikijulikana kama Tanganyika, Kenya na Uganda, ulianza mapema mwanzoni mwa karne ya ishirini.

Ushirikiano wa kwanza kabisa ulifanyika mwaka 1917 kati ya Kenya na Uganda ukihusisha mambo ya forodha (Customs) na miaka kumi baadaye, 1927, Tanganyika nayo ikajiunga katika umoja huu.

Mwaka 1948, ushirikiano wa kitaifa kati ya Kenya (Colony), Uganda (Protectorate) na Tanganyika (Territory) uliridhiwa rasmi na hivyo kuunda umoja wa forodha, ushuru wa pamoja wa nje, fedha, na posta pamoja na huduma ya kawaida katika usafiri na mawasiliano, utafiti, na elimu.

Baada ya nchi hizi tatu kupata huru, ziliamua kuunda Mamlaka ya Huduma za Pamoja Afrika ya Mashariki iliyojulikana kama EACSO (East African Common Services Organisation).

Mamlaka haya yalihusu fedha (East African Shilling), forodha (Customs Union), huduma za reli (East African Railways), ndege (East African Airways), bandari (E.A. Harbours) simu (E.A Posts and Telecommunications) na elimu ya juu (E.A. University).

Mkataba huu ulilenga pia mahakama ya pamoja, sera ya kiuchumi ya soko la pamoja. Haya yote yalitakiwa kuwa chini ya Bunge la Afrika Mashariki.

Hata hivyo matatizo yaliyojitokeza yalilazimisha kusitishwa kwa matumizi ya fedha ya pamoja na hivyo mwaka 1965 kila nchi ikawa na fedha zake.

Sehemu ya pili...

Mwaka 1967 makubaliano mapya yaliyoendana na wakati ilibidi yafanyike na matokeo yakawa ni kuanzishwa kwa utengamano mpya kati ya hizi nchi tatu za Afrika Mashariki, EAC (East African Community)

Jumuiya hiyo iliundwa na nchi wanachama na ilikuwa na Bunge lake la kutunga sheria na iliendeshwa kwa sheria kama Serikali na mafao ya wafanyakazi wake yalilindwa na kifungu namba 82 cha uliokuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya mwaka 1967.

EAC pia iliendeshwa kwa mfumo wa jumuiya za kimataifa na ilikuwa na service commission yake, pensions fund yake na saving scheme yake. Makato ya pension yalitunzwa Uingereza kwa agents wa EAC waliojulikakna kama "crown agents".

Sehemu ya tatu...

Mkataba wa EAC ulisema kuwa, ikitokea jumuiya ikavunjika, mgawanyo wa mali na madeni ufanywe na baada ya hapo wastaafu walipwe fedha zao mara moja. Pia walioainisha namna ya kuwalipa hizo fedha kulingana na thamani halisi ya dola na riba ya asilimia 7%.

Kwa kulinda thamani hiyo nayo isije ikaangushwa na farigisi (mfumuko wa bei) wataalamu wa uthamanishaji wa fedha za pensheni na Provident Fund Actuarists nchini Uingereza, waliweka asilimia saba ya riba limbikizi la dola hizo kwa kila mwaka, ambao deni au mafao hayo yatakuwa yamecheleweshwa kulipwa kikamilifu.

Kutokana na hali hiyo, iliweka katika article 1 "n" ya mkataba huo kile kinachoitwa weighted average ya sh. 8.31542 za nchi wanachama kuwa sawa sawa na dola moja ya Marekani kuwa ndio msingi wa kulipia madeni na mafao.

Pamoja na juhudi na malengo mazuri Jumuiya haikuweza kustahimili matatizo ya kiuendeshaji yaliyosababishwa na utofauti kimtizamo, kisiasa na kiuchumi baina ya hizi nchi na hivyo mwaka 1977 Jumiya ikavunjika.

Sehemu ya nne...


Baada ya kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilitakiwa waliokuwa wafanya kazi wake walipwe haki zao baada ya kuitumikia Jumuiya kwa miaka mingi.

Zoezi hili halikuweza kufanyika mara moja kwani ilibidi kwanza mgawanyo wa mali na madeni ya jumuiya ufanyike ikisimamiwa na msuluhishi aliyekubalika kwa pande zote, Dr. Victor Umbritch.

Pamoja na kuvunjika ipo secretariat ilibaki Arusha ikiendelea kukokotoa stahili ya kila mstaafu kulingana na ngazi aliyofikia pamoja na mshahara, muda aliotumikia jumuiya, pensheni na madai yoyote yale husika kama malimbikizo ya likizo.

Mwaka 1985 msuluhishi alimaliza kazi yake na kukabidhi ripoti yake kwa sekretariat husika. Miaka miwili baadaye, 1987, Serikali ya Jamhuri ya Tanzania ilikabidhiwa fedha za pensheni za hao wastaafu wa EAC zaidi ya pauni milioni 9 za Uingereza iweze kuwafikishia walengwa ambao kimsingi walikuwa ni wale wa General Fund Services.

Ushahidi huu hapa...

jumuiya2a-jpg.453496

Wakati huo pauni moja ya Uingereza (British Sterling pound), ilikuwa sawa na Tshs 20/= tu, kwa nini serikali ilishindwa kuzilipa? Mh. Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi, hizi pesa zilitumikaje? Je huu ulikuwa ndio mwanzo kabisa wa ufisadi nchini uliofanywa na serikali kwa kuamua kuwadhulumu (kuwaibia) wananchi wake?



Badala ya kufanya hivo, serikali ya Mwinyi kwa sababu ambazo hadi leo bado ni kitendawili ikaamua hizo fedha zitumike kwa malengo ambayo nayo hadi leo hayajawekwa hadharani na juhudi za wastaafu kuhoji zilizimwa kwa ukatili na bila maelezo.

Sehemu ya tano.

Kwa niaba ya Wastaafu waliotangulia mbele ya haki, wastaafu ambao pamoja na kuwa vikongwe bado wako hai, wajane na warithi wa Wastaafu, naomba majibu kwa swali hilo kutoka kwa Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi na viongozi wengine wa serikali wakati huo.

Kwa bahati nzuri wengi wao pamoja na kustaafu bado wako hai na wenyewe wakiendelea kulipwa mafao yao bila matatizo yoyote.

Viongozi wote wakuu waliohusika wakati wa matumizi ya fedha hizo bado wako hai…Rais Mstaafu Ali Hasan Mwinyi bado yupo, aliyekuwa Waziri Mkuu John Samwel Malecela yupo na aliyekuwa Waziri wa fedha Cleopa David Msuya bado yupo.


Nakaribisha mjadala na baadhi ya viambatanisho vitafuata…

Update 1


Tunaaza kwa kuangalia historia na misingi ya madai ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC.. Rejea hii "position paper" ikielezea zaidi...

jumuiya1-jpg.453484


jumuiya2-jpg.453483


jumuiya3-jpg.453482


jumuiya4-jpg.453489


jumuiya5-jpg.453481
 
Haya Makaburi haya ....!


Endeleeni kuyafukua

Ila msitegemee kukutana na harufu inayofanana hata robo na pafyum

Kaburi wake uvundo!!
 
Mkuu tunakusubiria, ila ninavyofahamu hapa kati watu walilipwa, kuna mzee mmoja namfahamu alilipwa.
 
Mkuu tunakusubiria, ila ninavyofahamu hapa kati watu walilipwa, kuna mzee mmoja namfahamu alilipwa.
onyx, ni kweli watu walilipwa lakini unajua malipo waliyopewa yalikuwa ni asilimia ngapi ya kiasi walichostahili? Hebu fikiria mtu aliyestahili kulipwa USD 8000 mwaka 1977 analipwa Tshs. 10,000,000 mwaka 2001, miaka 34 baadaye!

Mwaka 1977 dola moja ilikuwa sawa na shilingi 7 tu lakini mwaka 2001 dola moja ilikuwa sawa na shilingi 1,200! Hii ina maana kwamba mtu huyo alistahili kulipwa shilingi 96,000,000! na ilikuwa ni dhuluma iliyosimamiwa na serikali.

Ni wakati wa Rais Mwinyi ndio ufisadi kama unavyojulikana leo ulipopandwa, ukakua na kukomaa na tunachovuna kwa sasa ni matunda yake. Fikiria serikali inakabidhiwa pesa za wazee wastaafu iwafikishie, serikali ya Mwinyi inazikwapua na kuzipangia matumizi mengine.

Mwaka 1991 baadhi ya wastaaafu wa EAC walipomlilia aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais, John Samwel Malecela majibu yake yaliyojaa vitisho na kejeli yalikuwa na maneno yafuatayo...

I would like to make it explicitly clear that thw Government will not any claim from the Ex-EAC employees and any such thought to that effect should be forgotten. I hope you will not disturb me with any such baseless issues again.

Hii barua iliyokuwa na kumbukumbu PMC/C.350/1 ilinakiliwa kwa Mawaziri watatu...Waziri wa Fedha, Waziri wa Utumishi na Waziri wa Kazi. Baada ya hapa jeshi la polisi liliamriwa kuhakikisha wastaafu hawafanyi mkutano wowote mjini Dar es Salaam kudai haki zao.
 
Haya Makaburi haya ....!


Endeleeni kuyafukua

Ila msitegemee kukutana na harufu inayofanana hata robo na pafyum

Kaburi wake uvundo!!
Msherwa, kilichowashangaza hawa wastaafu ni chuki ya wafanya kazi wa serikali dhidi yao. Wengi wa hawa wafanya kazi hasa wa Hazina wakiongozwa na chuki binafsi dhidi ya Wastaafu kwa kile walichoelezea kwamba pesa walizokuwa wanadai ni nyingi mno. Viongozi wa serikali kwa upande wao walikuwa wanafanya juu chini wakitafuta mwanya wa kuzitafuna hizo hela za hao wazee wastaafu. Shuhudia baadhi ya magazeti yalivyoripoti hizo hujuma miaka hiyo.

jumuiya10-jpg.453555


jumuiya8-jpg.453560


jumuiya9-jpg.453563
 
Ungemtaja na Magu alikuwepo, otherwise hakuna wachangiaji.
Rais Mstaafu Mwinyi alimaliza kipindi chake cha pili bila kuwalipa hao wastaafu pesa zao na badala yake mbinu zikafanywa kuonesha kwamba utumishi katika jumuiya haukuwa tofati na utumishi serikalini. Utata ukaibuliwa kwamba pamoja na jumuiya kuvunjika, ajira ya hao wafanya kazi iliendelezwa kwa kuajiriwa serikalini na hii mbinu ilifanywa kwa makusudi wasiwalipe wastaafu.

Serikali iliamua kutoheshimu hii ripoti...
jumuiya12-jpg.453572


Rais mstaafu Mh. Benjamin Wiliiam Mkapa aliingia madarakani mwaka 1995 kwa ahadi ya kuwalipa wastaafu hao. Ajabu ni kwamba Hazina nayo ikaunda kitengo maalum eti kukokotoa stahili za Wastaafu kabla ya kuwalipa. Wastaafu walipinga hatua hiyo kwa sababu secretariat ya EAC huko Arusha ilishafanya hivyo na kukabidhi ripoti kwa kabidhi wasii Mkuu wa serikali lakini hawakusikilizwa.

Matokeo yake kitengo hiki kilianza kwa kuitisha na kutaifisha mafaili yote ya Wastaafu kutoka Arusha na kuamua kupuuza mapendekezo yaliyomo. Wafanya kazi wa kitengi hiki walifanya kazi hii kwa malipo ya ziada ambapo baadhi yao walilipwa hela nyingi kuliko za wastaafu wa Jumuiya. massaiboi, wakati ujanja huu unafanyika Rais wa sasa John Pombe Magufuli alikuwemo kwenye serikali ya Mkapa.
 
Zoezi hili halikuweza kufanyika mara moja kwani ilibidi kwanza mgawanyo wa mali na madeni ya jumuiya ufanyike ikisimamiwa na msuluhishi aliyekubalika kwa pande zote, Dr. Victor Umbritch.

Pamoja na kuvunjika ipo secretariat ilibaki Arusha ikiendelea kukokotoa stahili ya kila mstaafu kulingana na ngazi aliyofikia pamoja na mshahara, muda aliotumikia jumuiya, pensheni na madai yoyote yale husika kama malimbikizo ya likizo.

Mwaka 1985 msuluhishi alimaliza kazi yake na kukabidhi ripoti yake kwa sekretariat husika. Miaka miwili baadaye, 1987, Serikali ya Jamhuri ya Tanzania ilikabidhiwa fedha za pensheni za hao wastaafu wa EAC zaidi ya pauni milioni 9 za Uingereza iweze kuwafikishia walengwa ambao kimsingi walikuwa ni wale wa General Fund Services.

Ushahidi huu hapa...


Laana ya mafao nadhani ilianzia huku. Mzee Ruksa asimame Jukwaani atue huu mzigo.
 
Back
Top Bottom