Rais Mpya , Tanzania mpya, watu wapya!! Eee Mungu.

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,785
Eee Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi. Pokea heshima na utukufu, tunaliinua jina na enzi yako ya milele yote.
Asante kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania ambao umepita salama bila machafuko yoyote. Asnte kwa kutupa Rais mpya kabisa katika historia ya Tanzania. Asante kwa kutupa Slaa.

Mungu huwa unatangaza mwisho kutoka mwanzo na umesema tukiwa na Imani kama chembe ya haladali tunaweza kuamsha milima. Kwetu sisi CCM ni mlima na kwa imani tumeingusha. Umesema pia Imani ni hakika ya mambo yatarijiwayo ni bayana yasiyoonekana. Ndio maana kwa imani nimeona Slaa ni rais ni nitaishi nikiamini kuwa ni rais.

Najua uchaguzi bado kufanya, lakini katika imani mambo mawili nimekueleza kuwa utakuwa wa amani nay a kuwa Slaa ni rais. Ninakushukuru Mungu wewe ufanyaje miujiza, ufanyaye njia pasipo na njia.

Hata kama hali zote zinaonyesha CCM kupendelewana NEC, naomba ashikwe na kigugumizi mtangaza matokeo hata kama akipanga kumtangaza “Yule mtu” washindwe watangaze jina la Slaa. Mungu umefanya na unafanya miujiza kila siku. Siku ya 31 ya mwezi huu nayo umeshafanya miujiza.

Mungu mlinde Mh.Slaa katika urais wake ,mpe nguvu na hekima ya kuongoza nchi hii.Mpe uweza wa kuwatumikia watanzania kwa uwezo wake akili zake zote. Mpe afya yeye na viongozi wote wa serikali.
Linda umoja wa watanzania,linda amani , linda kila zuri la watanzania. Tupe moyo wa kukubali matokeo, wafariji CCM kwa kushindwa, wape nguvu ya kukubali na kuitoa nchi kwa Rais mpya.

Msaidie rais wa zamani Kikwete yeye na familia yake, wape umoja na amani ndani ya nyumba yao ili isivunjike kwa kutafutana wabaya. wape hekima ya kujua wabaya sio CCM ni wakati tu na mambo yake.

Ninaomba haya nikiamini
Amen.
 
Asante sana Waberoya kwa sala nzuri yenye kuleta hisia,

naongeza, 'Asante baba Mungu kwa kusikiliza sala ya watu wako watanzania tuliokulilia kama ulivyosikiliza sala ya wana wa Israeli walipokuwa jangwani kwa miaka 40. Amen, na iwe hivyo na iwe hivyo, Aaaamen'.

Naamini Mungu wetu atasikiliza sala zetu, naamini kilio chetu kimemfikia.
 
Mkuu Webby..............ulipotelea wapi Mkuu karibu tena..............
 
Habari ya siku mkuu Waberoya?

Well nimeona ni vema nisindikize post yako na kibao hiki! I believe

http://www.youtube.com/watch?v=jyDVx7cP5IE

Siku maneno hayo ya mwanzo yatakaposemwa na Dr. Slaa,........................... Mimi Dr. Wilbrod Peter Slaa...........

NB:Anywayz I have an audio for this kwa yeyote anayetaka naweza kui-upload
 
Habari ya siku mkuu Waberoya?

Well nimeona ni vema nisindikize post yako na kibao hiki! I believe

YouTube - Cameal Davis - I Believe

Siku maneno hayo ya mwanzo yatakaposemwa na Dr. Slaa,........................... Mimi Dr. Wilbrod Peter Slaa...........

NB:Anywayz I have an audio for this kwa yeyote anayetaka naweza kui-upload

Asante sana kwa kibao kitamu aisee.............I Believe!......ipo siku!
 
Amen! Tayari imekuwa!

Amen!!!

Mkuu Webby..............ulipotelea wapi Mkuu karibu tena..............

Nipo mkuu, si unajua tena dunia hii tunazunguka huku na huko, lakini mwisho wa siku tunakutania JF! nilitulia kidogo nilikuwa na imani dhaifu, lakini kumbe imani inaweza kukufanya uwe mtu mpya!

Habari ya siku mkuu Waberoya?

Well nimeona ni vema nisindikize post yako na kibao hiki! I believe

YouTube - Cameal Davis - I Believe

Siku maneno hayo ya mwanzo yatakaposemwa na Dr. Slaa,........................... Mimi Dr. Wilbrod Peter Slaa...........

NB:Anywayz I have an audio for this kwa yeyote anayetaka naweza kui-upload

za siku nzuri mwanaume! asante kwa kibao murua kinachohitajika haswaa kipindi hiki
 
Back
Top Bottom