Rais Magufuli zingatia umri wa kustaafu kwa watumishi wa umma

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
10,392
16,039
Nimefuatilia baadhi ya teuzi za nafasi za watumishi wa uma hazizingatii sheria ya kustaafu. Mfano Ombeni Sifue na mrithi wake wote wana zaidi ya miaka sitini. Huo ni mfano tu wapo wengi wa aina hiyo.

Nashauri umri wa kustaafu uzingatiwe ili vijana wetu wasomi wapate ajira wanazostahiki
 
"Techinicall know whom" Inatakiwa techinically know why and How. Atawapata vijana wasomi, ari na hamu ya kulitumikia Taifa
 
Nimefuatilia baadhi ya teuzi za nafasi za watumishi wa uma hazizingatii sheria ya kustaafu. Mfano Ombeni Sifue na mrithi wake wote wana zaidi ya miaka sitini. Huo ni mfano tu wapo wengi wa aina hiyo. Nashauri umri wa kustaafu uzingatiwe ili vijana wetu wasomi wapate ajira wanazostahiki
Wewe una miaka mingapi?
 
Uko sahihi lakini siyo kwa CCM
 
Nimefuatilia baadhi ya teuzi za nafasi za watumishi wa uma hazizingatii sheria ya kustaafu. Mfano Ombeni Sifue na mrithi wake wote wana zaidi ya miaka sitini. Huo ni mfano tu wapo wengi wa aina hiyo. Nashauri umri wa kustaafu uzingatiwe ili vijana wetu wasomi wapate ajira wanazostahiki
Mbona hujawahi uliza why Obama anacahguwa wazee? hatuangalii umri ila kumbuka nafasi hizo ni nyeti ona vile makamba sa hizi anawaweka watu roho juu je angepata nafasi nzito kama hizi ingekuwaje, nilisha sema vijana tulieni wakati ukifika mtachaguliwa na tujifunze kutoka kwa wazee.
 
Mbona mrithi wa Sefue ana miaka 59!! Atahudumu kwa miezi kadhaa alafu anapewa ajira ya mkataba.
 
Nimefuatilia baadhi ya teuzi za nafasi za watumishi wa uma hazizingatii sheria ya kustaafu. Mfano Ombeni Sifue na mrithi wake wote wana zaidi ya miaka sitini. Huo ni mfano tu wapo wengi wa aina hiyo.

Nashauri umri wa kustaafu uzingatiwe ili vijana wetu wasomi wapate ajira wanazostahiki
Mfano unataka labda katibu kiongoZ Ambaye angechaguliwa baada ya sefue awe na umri gani Mfano!!
 
nafasi nyeti na na ni yakiutendaji zaidi nahisi umri,uzoefu ,elimu vinahusika muacheni kijazi w.j afanye kazi
 
Tunazungumzia sharia ya utumishi wa uma, akitaka apeleke mswada bungeni sheria ibadilishwe najua bunge letu litapitsha hata akitaka watu wafie kazini, kwa jinsi bunge letu lolivyo watapitisha
 
Mimi pia nimeshangaa. Kuwa kiongozi ni kuwa mfano. Huwezi kuwa rais katika nchi yenye sheria na taratibu, halafu wewe hufuati taratibu hizo, unahimiza watu wafuate sheria na taratibu.

Utaonekana mnafiki.
 
Mbona hujawahi uliza why Obama anacahguwa wazee? hatuangalii umri ila kumbuka nafasi hizo ni nyeti ona vile makamba sa hizi anawaweka watu roho juu je angepata nafasi nzito kama hizi ingekuwaje, nilisha sema vijana tulieni wakati ukifika mtachaguliwa na tujifunze kutoka kwa wazee.
Nchi haiongozwi kwa kumuangalia Obama. Sheria ndo imeweka kikomo cha miaka 60 kwenye utumishi wa umma (except for Judges na JWTZ). Sheria ifuatwe, la sivyo mfanye amendment ya sheria.
 
Mfano unataka labda katibu kiongoZ Ambaye angechaguliwa baada ya sefue awe na umri gani Mfano!!

Unafikiri hizi nafasi hupewa watoto wa miaka 21?

kuna nafasi huwezi wapa vijana .

nafasi nyeti na na ni yakiutendaji zaidi nahisi umri,uzoefu ,elimu vinahusika muacheni kijazi w.j afanye kazi
Sheria ipo wazi kwenye hili! Rais anafanya kazi nzuri, lakini anapotenda kinyume na matakwa ya kisheria ni lazima aambiwe.
 
Back
Top Bottom