Rais Magufuli: Watu 138 waliokuwa na kesi za uhujumu uchumi, wamelipa fedha, Wametubu na kuachiwa huru

Nadhani sasa itungwe tu sheria ya kuondoa vifungo na kuweka option ya aliyetuhumiwa kulipa pesa kwa kosa lolote analolifanya ili Serikali ijipatie pesa na kuepusha mrundikano wa wafungwa gerezani.Ukitia mwanafunzi mimba, unailipa serikali na unarudi kitaa. Ukikamatwa umeiba kuku, unailipa serikali mara 10 ya gharama ya kuku ulioiba na unarudi mtaani. Namna hiyo.
Kwani hizo faini wanazo tozwa watu unafikiri haziendi serikalini !? Umejaa nongwa mpaka una comment ujinga
 
Wazo zuri sana. Ukimpa mimba mwanafunzi, adhabu iwe faini milioni 5 na kumtunza huyo mtoto.
Sasa ukimfunga miaka 30, serikali inamhudumia huyo mtuhumiwa na mtoto anakosa matunzo ya baba, huo ni ujinga!
Kama huna mil 5, babake binti akugeuze mke !
 
Ingawa Magufuli Anavunja Sheria Kwenye Ili Swala Ila Wacha Watu Warudishe Pesa Zetu".

Kuna Kesi Watu Walikuwa Wakisababisha Hasara Kubwa Kwa Nchi Lakini Walikuwa Wakipigwa Fini Kidogo Sana, Wakati Mwiz Wa Kuku Anachomwa Moto,

Bora Yabanwe Tu Mafisadi Yarudishe Pesa Za Umma Na Tusibague Mtu Watu Wote Washugulikiwe Hasa Wanasiasa Ambao Bado Wanakenua Meno Mtaani"
Wazee wa ufipa hawakuelewi hapa Mkuu,wao wanawatetea waliotuibia pesa zetu,ambao kipindi cha Rais dhaifu(kwa maelezo yao) walishinikiza awabane warudishe pesa. Hapa ndio nashindwa kuwaelewa hawa watu.
 
Mahakama ya mafisadi haiwezi kupata mteja Tanzania kwa sababu marais ndio fisadi namba moja nakatiba inazuia kuwagusa, so wizi na ufisadi utaendelea mpaka ccm watoke madarakani.
Ccm ni ukoo wa panya kuanzia Babu mpaka kilembwe ni wezi.
Huyu ndo mlitaka kumpa nchi !?
 
alisema watazitema kupitia tundu lolote,,ha ha ha,inanikumbusha kule saudi arabia vile Bin salman alivyowakusanya wahujumu uchumi na kuwafungia kwenye hoteli la kifahari na ili kutoka lazima uteme pesa ya maana,wote walitoa pesa wakaachiwa,,hata mmiliki wa TV ya MBC ilibidi aachie tv yake iwe controlled na Bin salman,nimeamini uhujumu uchumi sio mzuri aisee
Hawajui kuwa unaweza angusha nchi. Algeria ni wahujumu ndio waliangusha nchi.
 
Nadhani sasa itungwe tu sheria ya kuondoa vifungo na kuweka option ya aliyetuhumiwa kulipa pesa kwa kosa lolote analolifanya ili Serikali ijipatie pesa na kuepusha mrundikano wa wafungwa gerezani.Ukitia mwanafunzi mimba, unailipa serikali na unarudi kitaa. Ukikamatwa umeiba kuku, unailipa serikali mara 10 ya gharama ya kuku ulioiba na unarudi mtaani. Namna hiyo.
Kwa hali ilivyo hivi sasa, huu ushauri wako ni wa busara sana.
 
Natumaini hii haitakuwa mazoea na kuzaa utamaduni. Kwamba ukirihumiwa hata kwa uzushi unaambiwa kulipa na kisha unakuwa huru na raia mwema
Ni option, unaweza kataa au kukubali. Na mwenyewe amesema hiyo ilikuwa ni 'amnesty maalum' na kuanzia siku ya mwisho wa msamaha wake, yeyote ambaye ni fresh, basi apambane na hali yake.
 
DPP alisema ni 480, leo number imebadirika?!

Sasa nimeelewa kwanini Butiku alitaka watajwe hadharani, walijua ile idadi ni ya uongo.
Wewe hiyo idadi nakusumbua nini !? Maana huwezi kututhibitishia ni uongo, ili unataka tu ionekane uongo
 
Rais Magufuli amesema hadi leo Jumamosi Watu 138 waliokuwa wakidaiwa kuwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuomba msamaha kwa DPP, wamerudisha fedha, wametubu na kuachiwa

Ametoa kauli hiyo leo akiwa Mpanda wakati akizindua safari za ndege za ATCL kutoka Dar es Salaam kwenda Mkoani Katavi na kuongeza kuwa maombi ya kukuri makosa zaidi ya 500 bado yanachambuliwa

Amesema “Walioachiwa wako huru wamekwenda kujumuika na familia zao. Huo ndiyo upendo wa pekee kwa sababu tulitoa msamaha na wao wamepokea na sisi tunashukuru. Hao sasa ni raia wema wahesabike kuwa ni raia wema katika nchi yetu.”

Aidha, ameongeza kuwa kulikuwa na watuhumiwa 700 walioomba msamaha na wataendelea kuachiwa kadri watakavyo rudisha fedha na fedha hizo zitatumika katika shughuli za maendeleo ya Watanzania
Vipi wale walipewa hela na Rugemalila nao wangerudisha maana zile fedha zimetakatishwa
 
Kwa Sheria mpya za Jiwe , Kila analowaza na kuota ndiyo Sheria.
Sheria ipo, ndio maana wanakiri mahakamani na Hakimu anapitisha hukumu. Acha kuwa mjinga kwa kuendekeza nongwa !
 
Back
Top Bottom