Rais Magufuli, Unawaza nini?

Najaribu kupata picha ya ametoka madarakani na hao anao waonyesha chuki kubwa kabisa bila kujificha wakawa madarakani atakuwa na wakati gani?
Kuwapata watu kama Mandela sio jambo rahisi ndani ya karne moja hivyo kutegemea visasi ni jambo lisilo kwepeka. Anajua hilo?
Mwinyi, Mkapa na hata JK hawakuwa wanaendesha nchi kwa chuki binafsi hivyo hata kama warithi wao wangekuwa chama tofauti bado heshima yao ingekuwepo.
Najaribu kumfananisha na kiongozi afrika mashariki na kati aliyetoka madarakani aliyekuwa na tabia hizi simpati zaidi ya Amin pekee.
 
Kwa nini unaandika "kumbe hata amerika"?

Kwani Amerika ni mbinguni?
mara zote huchukuliwa na watu wengine kama sehemu isiyo na matatizo kabisa.

mfano mtu anapotaja democrasia ataiorodhesha amerika.
 
mara zote huchukuliwa na watu wengine kama sehemu isiyo na matatizo kabisa.

mfano mtu anapotaja democrasia ataiorodhesha amerika.
Mara zote wapi?

Mbona watu wanalalamika Amerika hakuna demokrasia.

Kwa mfano, mtu anayepata kura nyingi anaweza kushindwa urais na mtu anayepata kura chache zaidi.

Hilary Clinton alimzidi Donald Trump kwa idadi ya kura, lakini Donald Trumo akawa rais.

Sasa hiyo ni demokrasia?
 
mara zote huchukuliwa na watu wengine kama sehemu isiyo na matatizo kabisa.

mfano mtu anapotaja democrasia ataiorodhesha amerika.

Sio sahihi sana lakini kwa mbali sana wana sheria zenye meno, na hizo hazina macho kuanzia kwa rais mpaka mtu wa kawaida. Mapungufu machache yako ila sio kwa kiwango cha hapa kwetu.
 
mkuu unanibishia mimi nayajua haya mambo ndivyo yalivyo .wapo watu america ni rejea yao katika mambo ya democrasia.
 
Ukisoma habari za mitandaoni, unaweza ukadhani 90% ya wabongo ni wapinzani...sasa ngoja muda wa kudemonstrate upinzani wao kwa vitendo...

Acha CCM watawale tu
 
Sio sahihi sana lakini kwa mbali sana wana sheria zenye meno, na hizo hazina macho kuanzia kwa rais mpaka mtu wa kawaida. Mapungufu machache yako ila sio kwa kiwango cha hapa kwetu.
ndio hivyo,hata wao haikutokea kwa miaka 50 au 80 wakawa walipo.

angalia matharani uhuru wameupata miaka 300 iliyopita,mengi yamepita kwa nguvu na ubabe ili kifikia ilipo leo,na wanaendelea kuboresha.

utakumbuka pia huyu mzee aliishasimamisha shughuli za kiserikali kisa wamemzingua kutoa hela zaa kujengea ukuta,na ukuta umejengwa.ndio hivyo wakuu.
 
Mbona majibu ya mawazo ya muheshimiwa yapo!!!!...just angalia yanayoendelea na hayo ndio anayo ya waza
 
Sheria na kanuni zinapotengenezwa mahsusi kwaajili ya kunufaisha kundi fulani la jamii bila kuangalia maslahi mapana ya jamii iliyostaarabika zinapoteza maana na uhalali wa kuendelea kufuatwa.

Wanasiasa wanapotumia mamlaka yao kujilimbikiza Mamlaka zaidi ili waendelee kuikandamiza jamii wanapoteza sifa ya kuwa viongozi badala yake wanageuka kuwa vibaka wa kisiasa tu.

Kundi kubwa la wanasiasa ni vibaka wa kisiasa.
 
He does not look like a person who will be there in the future. He is more of this day kind. Maybe he knows something we don't know about his health and the time he has...
 

Sioni kama kunahitajika miaka kadhaa jambo lenye kutoa haki kufanyika, labda unipe kwa uhakika inahitajika miaka mingapi jambo la kutenda haki lifanyike hapo naweza kukuelewa. Huyo aliyejenga ukuta kwa ubabe huko kwao saa hii watu wamepindua meza wanamla kichwa kutokana na nguvu ya sheria zisizo na double standard. Atajua kama ataenda kuishi kwenye huo ukuta aliuojenga kibabe au vipi hilo atajua yeye. Tunahitaji sheria za hivyo hata hapa kwetu. Huko kwao iliwachukua miaka mingi kuangalia TV ya rangi, je na sisi sasa hivi tuanzie kwenye hiyo TV ya black & white kama walivyokuwa wao, kisha ndio tume tuanze kutumia ya rangi? Acheni kutoa mifano ya kuhalalisha udictator uchwara.
 
mkuu unanibishia mimi nayajua haya mambo ndivyo yalivyo .wapo watu america ni rejea yao katika mambo ya democrasia.
Sijasema hakuna watu ambao america ni rejea yao katika mambo ya demokrasia.

Hilo si jambo ninalohoji.

Jambo ninalohoji ni, Je, Amerika ya leo yenye ubaguzi wa rangi na rais mwenye matusi asiyejali utawala wa sheria, ambaye ana wafuasi wengi tu, yenye siasa za mwenye nguvu mpishe, yenye polisi wanaoua raia kama kuku, yenye mfumo wa kura unaoweza kumpa urais mtu aliyepata kura chache, wakati aliyepata kura nyingi asipate urais, inafaa kuwa rejea katika mambo ya demokrasia?

Hapa kwenye maktaba yangu nina vitabu zaidi ya mia vinaikosoa demokrasia ya Amerika, kuanzia vya Gore Vidal, Noam Chomsky mpaka Joseph Stiglitz.

Na hawa si waandishi wa ovyo, hao ni reputable authors, big name university professors na Nobel laureate.

Ushawahi kusoma waandishi hawa?
 
basi mkuu kama tumeshindwa kuanza kuangalia tv ya rangi mbili sasa hivi sababu wao wameshavuka huko,haimaanishi kila kitu tunaweza kukibeba kama kilivyo.vingine ni lazima tupite walimopita wao.moja wapo ni huo ustaarabu.

hiyo ya kuliwa kichwa ni habari,lakini kama aliweza kusimamisha shughuli za kiserikali ili fanye jambo lake kwa mamlaka aliyopewa,usishangae wakaishia kuitisha vikao tu.
 
haifai hata kidogo.
 
Mada yako ina mawazo fikirishi lakini imeharibiwa na hisia zako za chuki dhidi ya Serikali iliyoko madarakani na kuamini kuwa matatizo ya Tanzania yatatuliwa na mataifa ya nje. Ebu jikumbushe kilichotokea Iraq na Libya.

Narejea hoja yako kuthibitisha hilo, kwamba unadai ati:
Vyama mamluki vya upinzani vilivyopandikizwa na System vijifanye eti ni vyama vya upinzani na vinashiriki Uchaguzi, mataifa makubwa yanajua ukweli wote juu ya hiyo ghiliba
 

Hata kama wataishia kwenye vikao, lakini wangalau kwa sheria zao wanaweza kumchorea mstari na kusiwe na umwagaji wa damu kama huku kwenye shit hole countries. Ingekuwa huku kitendo cha kumjadili rais tu, lazima kungezuka machafuko wapambe wake wasikose mlo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…