Rais Magufuli, unapoendelea kutengeneza mfumo usivisahau vyombo vya dola

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
428
250
Salamu nyingi zikufikie Rais wangu mpendwa John Joseph Pombe Magufuli, nakupongeza sana kwa namna unavyoendesha mapambano ya kiuchumi na ya kimfumo vilevile, ni miaka mingi ilipita katika bara la Africa kumpata Rais mwenye hulka na tabia kama yako, Watanzania si budi kumshukuru MUNGU kwa kutupatia Rais wa namna yako, MUNGU AZIDI KUKUWEZESHA NA KUKUPA UJASIRI ZAIDI WA KUSONGA MBELE.

Rais wangu mpendwa unapopambana na mifumo mibaya ndani ya nchi yetu nakuomba kwa moyo wa dhati na kwa unyenyekevu usivisahau vyombo vya dola, hawa ni wanao ambao wanaishi maisha ya hatari kila uchao, wanahangaika kuiweka nchi hii salama masaa 24 ndani ya mwaka mzima, angalia posho zao, angalia hali ya maisha yao, nitaanza kuelezea moja baada ya nyingine:

JESHI LA POLISI: Jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele katika kulinda raia pamoja na mali zao, nalipa heko Jeshi hili kwa kazi nzuri wanazofanya kila kukicha katika nchi yetu , nadhani hawa ndio watumishi wa umma wanaowahi kuamka mapema na wanakuwa wa mwisho pia kulala, Amiri Jeshi wangu Mkuu Joseph Magufuli, vijana hawa licha ya kuanza kuwaboroshea mazingira yao ambayo yalikuwa taaabani, bado una kazi kubwa ya kuimarisha maisha yao haswa upande wa makazi, wengi bado wanaishi kwenye nyumba ambazo ni duni kulingana na mazingira ya kazi yao wanaendelea kupata msongo wa maisha kutokana na mazingira yao, imarisha posho sana haswa ukizingatia shughuli yao ni ya masaa ishirini na nne, ni shughuli yenye kuhitaji uzalendo wa hali ya juuu na weledi usiokuwa na mipaka, ukisha yafanya haya kwa hawa vijana wako Rais wangu mpendwa mulika mfumo mzima wa Jeshi la polisi katika kupandisha vyeo na upewaji wa Promotion, kwa weledi wanagu mdogo nilionao huwa naaamini kabisa upandishwaji cheo wa kazi za medani haswa hizi za kijeshi hutegemea sana utendaji kazi wako katika ulingo wa medani hyo, pia imarisha vifaa, yakiwemo mavazi na vitendea kazi, nayaleta kwako haya Rais wangu sio kwamba we ndie mwenye kuyatendea kazi unao wasaidizi wazuri kabisa katika Jeshi hili wakipewa mwongozo wanaweza kuyasimamia kwa umakini kabisa.

JESHI LA WANANCHI TANZANIA, hawa ndio walinda mipaka yetu na nchi kwa ujumla, wnafanya kazi yao vizuri kwa sababu hadi sasa nchi yetu ipo shwari kabisa,kilio chao sio tofauti kabisa na Jeshi la polisi yale niliyosema awali hap juu yazingatiwe kabisa, lakini ningependa kushauri licha tu ya kuwa walinzi wa mipaka yetu, ningefurahi kuona Jeshi hili linaongezewa majukumu ya kufanya, isiwe tu wakati wa dharura na majanga, haswa nilifurahishwa na jambo ambalo walilofanya majuzi la kuanza kusambaza vifaa vya mahabara mashuleni, naamini kulitumia Jeshi hili Zaidi ya hapo, sababu miongoni mwao wamejaa wazalendo, nch hiii ya Tanzania tutapiga hatua Zaidi mbele.

Baaada ya kueleza kwa ufupi kuhusu majeshi hayo hapa Tanzania, kuna Jeshi la magereza, paia ambalo mahitaji yake sio tofauti sana na mahitaji ya majeshi mengine, kuna Jeshi pia ambalo ni moyo wa nchi TISS,Mhe Rais angalia upya sharia zilizounda TISS, je zinaendana na wakati tulionao? Je zinawapa nguvu hawa vijana wako kufanya kazi pasipo kuwa na shaka? nakuomba itazame sheria hiii na kwa muongozo wako naamini kabisa kuna jambo linaweza kufanyika.

Nimeandika haya yote MHE, Rais John Pombe Magufuli, sababu unapoimarisha mfumo , mfumo huu utaimarika kwa kuviiiamarisha vyombo vya dola, ambavyo ndilo jicho la nchi yetu, pia nakupongeza sana kwa ujasiri ulionao wa kuonyesha madhaifu yalioifikisha nchi hii hapa tulipo, hakika ni ujasiri wa hali ya juu.
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,383
2,000
Katika hili sina tatizo na mh. Ushauri wako ni mzuri mkuu na hasa hili jeshi la wananchi kweli ingefaa tukaendelea kuwatumia zaidi. Ujenzi wa taasisi za serikali na za kijamii iwe ni sehemu ya shughuri zao kwani wana wajuzi, vifaa na umakini mkubwa sana. Tunachaje kuwatumia wajeshi wetu kwa shughuri za kizalendo na badala yake tunawabeba wawekezaji tena Kutoka nje katika mambo madogo na ya kawaida sana?

Tulitumie jeshi letu ili litusaidie naamini na wao watajivunia kazi zao zikiwa za mifano. Na huu ndo
Uzalendo.
 

Brice85

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
828
1,000
Nchi hii sio ya majeshi tu watumishi wengine wa serikali wapo na ndio walio sahaulika bora hata ya hayo majeshi.
1. Wanapewa resheni alawansi pamoja na package kila mwezi.
2. Wana likizo ya miezi mitatu tofauti na kada nyingine za serikari.
3. Wana maduka yanayo wauzia vitu kwa bei rahisi tofauti na kada nyingine za serikali.

Na mambo mengine mengi hata sio ya kuyasema wao wanapata kama motisha na wengine hawana.
Nb.
Aboreshe maslai ya watumishi wate wa serikali bila ubaguzi tofauti na ushauri wako mtoa mada.
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
21,562
2,000
Mleta Mada Hivyo Ulivyotaja Ndiyo Vyombo Vya Ulinzi Tu?

Tiss,Pccb,Jw, Police, Immigration, Fire,Prison, Na Wananchi
 

Omuchimati

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
428
250
Mleta Mada Hivyo Ulivyotaja Ndiyo Vyombo Vya Ulinzi Tu?

Tiss,Pccb,Jw, Police, Immigration, Fire,Prison, Na Wananchi
Hapana mkuu asante kwa nyongeza......ndio maana ya kuleta uzi ili tuongezee au kuuujadili......
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom