Rais Magufuli una ujasiri jukwaani tu

CCM kitaendelea kuwa chama bora kabisa barani africa na duniani kote.
Ubora ktk nini ?! sema inatumia dola otherwise haina ubora wowote. Na ukipinga washauri ikubali TUME HURU YA UCHAGUZI NA KATIBA ISIYO YA KIKOLONI
 
Bila shaka huyu jamaa takuwa ni wa LUMUMBA kati ya wale wanazi..

Writer wa hii THREAD yuko deep sana zaid ya ivo VI COMMENT vyako[emoji40]
 
Huyu mwandishi huyu awe makini tena sana tusije tukasikia kwamba amepata madhara kutoka kwa watu wasiojulikana? Mwenyezimungu amlinde Amin.
Mungu mwema yupo nyuma yake[emoji120]
 
Kumbe maneno yote hayo kumbe hoja ni bunge live. Mabadiliko ya kweli ndicho raisi anachofanya na alikiahidi. Mabadiliko haya ya kweli ni pamoja na tunavyoendesha siasa zetu, likiwemo hili la bunge kuonyeshwa live 24 hours lililoanzishwa katika awamu ya nne.

Mjadala wa bunge live ulishafungwa kitambo, mtazoea tu. Ukweli ni kuwa hakuna ko kote duniani ambako bunge huonyeshwa live. Only in Tanzania ilikuwa ikifanyika hivyo. Serikali ya awamu hii inajitahidi kunyoosha nchi, wengine lazima maumivu yawapate. Tuiache ifanye hayo mabadiliko, tutaipima 2020.
 
#Bwana shemeji# kuna wakati nawaza na kujiaminisha kwamba mtukufu sana kutokana na hulka yake ya kutopenda kumsikiliza yeyote huenda hadi sasa hawajamwambia kwamba yeye ndiye mkuu wa nchi na ndiyo maana ukimtafakari kupitia matamshi yake mwenyewe utagundua kwamba anatamani kupewa mamlaka fulani)(ambayo hayajui ni yepi) ili atufikishe mahali fulani ambapo hata yeye hajui pia ni wapi!
 
..... nchi inahitaji kuwa na vijana kama wewe 200 tu ili kukua kidemokrasia
 
Masikini Magufuli, hajui anatupeleka wapi na laiti angevua hiyo miwani mieusi, pengine angeweza kuona anakotupeleka siko. Tatizo kazungukwa na wanafiki na kama kawaida wanamshangilia alivyovaa kumbe hana nguo! Kama wangegutuka wasingekosa kuiona hatari iliyo mbele yao.
 

Attachments

  • Mbele-kwa-mbele.jpg
    65.8 KB · Views: 131
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…