My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,333
Kwa sababu hata wewe huwa unasema kuwa, msema kweli ni mpenzi wa Mungu, basi acha nami nikuambie ukweli tupu.
Wapinzani unaowachukia leo ndio walisababisha wewe ukawa Rais, bahati nzuri hata wewe unalijua hilo na mara nyingi umeongea kuwa uliokota embe kwenye mti wa mwarobaini.
Chama chako CCM kimeshakufa, nguvu pekee ya CCM ni Police na TISS.
CCM imebakiwa na kundi la watu wachache wanafiki ambao lengo lao ni kushibisha matumbo yao na baadhi ya illiterates wasiojua lolote.
Hao watu ni hatari na iko siku watakukana hadharani kama wanavyomkana JK leo.
Haukuwa mpango wa CCM kukupa urais, Mungu alisimama upande wako ili nawe usimame na watanzania lakini imekuwa kinyume.
Kila siku umekuwa wa kusifiwa tu, yaani hukosei, sifa anazostahili kupewa Mungu zinakuja kwako, eti hakuna kukosoa.
TBC 24/7 ina vipindi vya kusifia tu bila kukosoa, kuna serikali duniani isiyokosea?
Umetunyima haki yetu ya msingi ya kuchagua viongozi tunaowataka kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kuwa mpinzani Tanzania imekuwa uhaini, eti ni lazima CCM itawale.
Bahati mbaya kwako waliopaswa kukueleza ukweli ni viongozi wa dini kumbe nao ni ma agents wa CCM na serikali waliojificha kwenye koti la utumishi wa Mungu.
Eti kila Mtumishi wa Mungu anakusifia, ni binadamu gani wewe usiyekosea?
Hawa watu hawakusifii bali wanakusanifu ili wapate kula.
Uchaguzi wa serikali za mitaa ungeuacha ili upime juhudi zako zinavyokubalika kwa wananchi, Kitendo cha kukimbia uchaguzi mdogo kama huo ni dalili kwamba 2020 hakuna uchaguzi kabisa.
Ni kwa nini wapinzani wamekuwa adui kiasi hicho?
1. Wanazuia manunuzi ya ndege?
2. Wanakwamisha mradi wa Stiglers Gorge?
3. Wanakwamisha ujenzi wa SGR?
4. Wanakwamisha ujio wa mkoa wa Rubondo?
5. Wanashawishi wananchi waichukie serikali?
Lakini wanawezaje kushawishi wakati mikutano uliipiga marufuku na halafu tunaambiwa kuwa wananchi wanaipenda sana serikali yao.
Tunajua ya kwamba wewe ni mchapa kazi, kwa hiyo hakukuwa na sababu ya kuwafanyia hila wapinzani, utendaji wako ungeonekana kwenye sanduku la kura tu.
Sifa bila kasoro anastahili Mungu tu, zaidi ya hapo chukizo kwa Mungu.