Mhe. Rais pole sana kwa shughuli nzito ya kuliongoza taifa hili changa lenye mianya mingi ya rushwa, uzembe na upotofu wa maadili ya kiutumishi. Ninaamini kwa dhamira yako njema tutafika tu.
Katika awamu yako hii ya uongozi umeamua kuwa elimu ya msingi na sekondari (kidato cha NNE) iwe bure. Ni jambo jema sana.
Lakini ninatoa ushauri kuwa ufanyike mchujo mkali sana ktk shule za sekondari za serikali ili kuwaondoa wanafunzi wote wasio na sifa ya kuwa sekondari. Wapo wengi tu mhe. Hili likifanyika shule nyingi za sekondari tutazibadilisha matumizi na kugeuzwa kuwa vyuo vya veta ama kilimo. Serikali isibebe mzigo mzito wa kugharamia wanafunzi ambao kimsingi hawana sifa za kuwa sekondari.
Jambo hili pia lifanyike vyuo vikuu. Baada ya mtangulizi wako Jk kuamua kuwapa mikopo hata wanafunzi waliopo vyuo vikuu binafsi sifa za udahili zililegezwa ili kupata wanafunzi wengi wa kueneza vyuo vyote vya mabwenyenye na serikali. Jambo hili lilipelekea wanafunzi wasio na sifa stahiki kuingia vyuo vikuu. Madhara yake in kwamba serikali inabeba mzigo mkubwa wa kutoa mikopo kwa wanafunzi ambao tija yao baadaye ni karibu na sifuri.
Tuwaondoe wote waende wakaaome vyuo vya kati na ufundi mchundo.
Wanafunzi gani wa vyuo vikuu wako kihasara hasara tu? Hawana kitu kabisa kichwani weupee!! Kazi kuvaa headfone masikioni, suruali na sketi za kubana na kujiingiza kwenye starehe na ngono zembe. Tuwatoe wote wasiofaa. Tutaokoa fedha nyingi sana.
Nawasilisha