Rais Magufuli, tatizo sio kuficha pesa ila utakatishaji

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
A. UTANGULIZI.
Wasalaam ndugu zangu,
Mimi siyo mfuatiliaji wa siasa lakini ni madau wa maendeleo na masuala mengi ya muhimu hapa nchini. Leo nimerudi kutoka matembezi yangu nikaingia mtandaoni na kuona alichokisema raisi juu ya watu kuficha pesa. Hili halikunistua sana lakini njia ya kulikabili tatizo ndiyo iliyonistua.

Ukweli ni kwamba tatizo la kuficha pesa lipo sana hapa nchini lakini siyo kwa kiasi kikubwa kama ambavyo raisi kalizungumzia na kulifanya liwe: Na kwa kipindi hiki nashawishika kusema kwamba lenyewe siyo chanzo cha kuzorota uchumi hapa nchini kwetu.

Huenda ndugu raisi hajaambiwa ukweli na hawa watunga sheria na wanauchumi wetu wa hapa nchini. Tatizo kubwa kwenye uchumi kwa kipindi hiki siyo kuficha pesa tu, bali suala zima la UTAKATISHAJI (Money Laundering) wa pesa. Hivyo tukiamini na kusema kwamba kuficha pesa ndiyo tatizo kuu, tutakuwa tunaufumbia mambo ukweli na kulenga shabaha sehemu ambako adui hayupo. Kwa kifupi tu ni kupoteza nguvu na rasilimali za nchi hii.

Binafsi naamini raisi kuwa una nia njema kabisa, lakini wewe siyo mtaalamu wa mambo ya uchumi na sheria. Na kwa hali ya nchi ilivyo kwa kipindi hiki sisi wananchi wako wa kawaida hatutegemei kwamba wanasheria wetu au wanauchumi wanaweza kukuambia ukweli kuhusiana na nini haswa ndiyo kansa iliyojificha kwa sasa kwenye uchumi wa Tanzania.

B. UTAKATISHAJI WA PESA
Nini maana ya UTAKATISHAJI WA PESA?
Hiki ni kitendo cha kuzichukua pesa chafu au pesa yoyete iliyotokana na uhalifu na kuifua ili ionekane safi kisha unaiingiza kwenye mzunguko wa uchumi. Mfano mzuri tu Waziri fulani anaenda kusaini mkataba na wawekezaji fulani kwenye HOTELI X.

Pindi anafanya hivyo anapewa bahasha ina cheki nono ya Bilioni kumi labda. Hali akijua kabisa kupokea ile cheki ni kitendo cha Rushwa na anweza kukamatwa baadae, waziri anaamua kuichukua ile pesa na kuipeleka kwenye mabenki ya nje au kuigawanya-gawanya kisha mtu anawekeza kwenye makampuni makubwa. (Shell Companies). Au kwa namna nyingine mtu anaweza tu akaweka kwenye akaunti ya mtu mwingine nje ya nchi na kisha pesa zinaweza kuja kama misaada.

Lakini mpaka sasa wenye uwezo wa kuficha pesa nje ya nchi ni wale tunaowaita BIG-FISH. Kwa hapa Tanzania wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa ndiyo wenye uwezo wa kusafirisha pesa kwenye mabenki ya nje (Transnational-Money Transfer).
Mheshimiwa raisi kwa hao unaofikiri pesa zimefichwa hapa nchini ni wachache sana;

Pesa chafu ipo kwenye mzunguko na inatumika kuwanunua wanasiasa na vyombo vya habari. Huu ndiyo ukweli mchungu; naamini njia yako ni njema sana kabisa lakini ingeweza kufanya kazi sana katika mazingira ya 90's na 80's.

Kwa sasa waharifu wengi wanapata pesa chafu kutokana na Rushwa, madawa ya kulevya, ujangiri, wizi , ulanguzi, kukwepa kodi na mengineyo mengi na pesa zao wanaziweka kwenye mzunguko na wala hawzifichi tena. Kadiri teknolojia na utawandawazi unakuwa na hivyo ndivyo uharifu nao unazidi kuwa wa juu (sophisticated).

Pesa hazifichwi NDANI tena, ZINAFICHWA KWENYE MZUNGUKO. Hizo pesa ndiyo zimenunua majumba na zinaendelea kujenga mengi huko MASAKI, MBEZI BEACH, UNUNIO, MSASANI, NJIRO, SAKINA etc.
Wataalamu kwa lugha ya kiingereza wanasema "INJECTING DIRTY MONEY INTO THE LEGAL ECONOMY".

Mwaka jana nilienda PCCB nikapata wasaha wa kufanya majadiliano na baadhi ya maofisa wakubwa pale. Wakanipa mifano mizuri tu kama THE TEGETA ESCROW SCANDAL na jinsi UTAKATISHAJI WA PESA ULIVYOFANYIKA. Wale wahanga wa ile skandali kama Tundu Lissu alivyosema, kweli walibeba pesa kwenye Lumbesa, magunia na sanda lakini hawakuzificha ndani, walizificha kwenye mzunguko.

Nyingi zilitumika kukupigia wewe kampeni na nyingine zikanunua Dollar, Pound na Euro na kupelekwa nje ya nchi. Na hii ni moja ya sababu kubwa kabisa Shillingi kuanguka hapa nchini. Mheshimiwa raisi ni lazima ushauriwe vizuri kabisa kwamba tatizo siyo kuficha pesa ndani, tatizo ni kutakatisha pesa na kuziingiza tena kwenye mzunguko.

IGP Mstaafu ndugu Saidi Mwema kwenye Makala yake iitwayo "CURRENT SITUATION AND COUNTERMEASURES AGAINST MONEY LAUNDERING: TANZANIA’S EXPERIENCE". Amekiri kabisa kwamba Utakatishaji wa pesa ni moja ya kosa ambalo linaumiza uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa hakuna sheria sahihi ambazo zinaweza kulishinda tatizo.

Ni kosa linalofanywa na wataalamu waliojipanga wakipata msaada kutoka kwa Wansheria na Wanauchumi wazuri kwa nchi. Mwaka juzi tena Dr Edward Hossea alisema zaidi ya asilimia 30 ya pato la taifa inapotea kwenye rushwa na utakatishaji wa pesa. Lakini mheshimiwa hili mbona hujalitaja? Huu ndiyo ufichwaji wa pesa haswaaa hawa wanaoficha ndani ni vidagaa vidogo sana ndani ya bahari kubwa.

C. MTAZAMO WA KISHERIA.
Nisema kabisa hata wataalamu wa sheria wanakiri kuna tatizo kubwa kwenye sheria za nchi ambazo wajanja wamezitengeneza na kuacha nafasi (gaps; lacunae) ili waendelee kupiga pesa. Naamini kabisa kwa msaada wa BOT unaweza kubadilisha noti ya elfu kumi kwasababu hilo lipo ndani ya uwezo wako lakini nakuahidi hata hizo noti mpya zitafichwa tena (HUU NDIYO UKWELI MCHUNGU).

Ukisoma Sheria ya utakatishaji wa PESA au ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na marekebisho yake ya mwaka 2012 yameorodhesha makosa mengi sana yanosababisha Utakatishaji wa Pesa. Lakini mpaka leo hii pesa inazidi kutakatishwa na kuingizwa kwenye mzunguko.

Kwa kifupi sheria za nchi ni mbovu na haziwapi mawakili wetu uwanja mpana wa kuweza kuwashughulikia ipasavyo watakatisha pesa. Hivyo hata wewe ukichapisha pesa upya bado sheria haikupi nguvu ya kufanya hivyo. Nitakupa mfano mzuri kabisa katika hili. Mwaka 1983 na 1983 Marehemu Sokoine alianza mchakato wa kuwasaka wahujumu uchumi. Naye alikuwa ana nia njema kama wewe lakini kwa bahati mbaya safari yake iliishia hapo Morogoro.

Vijana wa UVCC ndiyo walileta hamasa kubwa kwa Sokoine. Aliwashughulikia sana wahujumu uchumi, watu wengi walifungwa sana lakini mwisho wa siku ikaja gundulika kwamba wanaoguswa ni Vidagaa na wale BIG-FISH waliendelea kupeta tu mtaaani. Alipojaribu kuwagusa hata sheria za CHAMA na NCHI ziliwalinda. Inasemekana aliwataka hadi kuwafuata mawaziri wakuu wastaafu, wakubwa wengine pamoja na viongozi wa dini:Lakini ilishindikana, na kwanini kwasababu moja yeye hakuwa Raisi na mbili sheria ile ilikaa vibaya.

THE ECONOMIC SABOTEURS ACT ya 1984 ilitengeneza mahakama ya Mafisadi ya kwanza kabisa hapa nchini. Ilikaliwa na watu watatu wawili ambao ilikuwa siyo lazima wawe wanasheria. Mtu ulikuwa ukikamatwa moja kwa moja na pesa za taifa unapelekwa kwenye hiyo mahakama na unanyimwa haki ya kujitetea na wala huwi na wakili wako.

Wewe ni ndani tu: Kama ilivyo ada, BIG FISH waksema ule ni uvunjaji wa haki za binadamu hasahasa THE PRESUMPTION OF INNOCENCE and RIGHT TO LEGAL REPRESENTAION. Kweli njia za Sokoine zilivunja sana haki za binadamu lakini wengi walimpiga vitab siyo kwasababu wanajali haki za binadamu bali matumbo yao.

Ile sheria ilirekebishwa na kesi zikarudishwa Mahakama kuu na serikali ikaendlea kucheza Twisti pamoja na mafisadi. Kwa hivyo mheshimiwa raisi kjama anataka kufanya kitu kinachoeleweka ni lazima atambue kwanza tatizo ni Utakatishaji wa Pesa. (Money Laundering) kwasababu pesa ziko ndani ya mzunguko na kama kuficha wanazificha nje. Mimi naomba raisi asije akashindwa katika hili, alenge shabaha upande adui alipo.

D. NINI KIFANYIKE?
Mheshimiwa raisi ni lazima ajue kabisa kifungu kimoja cha sheria kinaweza kujenga au kubomoa nchi yetu. hadi mwaka 2000 nchi ya India ilikuwa inateswa sana na TATIZO la UTAKATISHAJI wa pesa. Walijaribu mbinu zote kama wewe lakini ikashindikana. Makanjanja walishajua kuficha hela USWIS huko. Kesi zilipopelekwa mahakamani mawakili walishindwa kuthibitisha wizi wowote ule kwasababu ushahidi walikuwa hawana. Pesa na mali zina majina mengine na huwezi kunyang'anya kwasababu ni kinyume cha sheria.

Kwenye SHERIA ZA USHAHIDI au THE LAW OF EVIDENCE, siku zote serikali ikipeleka kesi mahakamani ni lazima wao ndiyo wathibitishe kwamba mtu ni mwenye kosa. Mfano kama Mtu kaua inabidi waendesha mashitaka wathibitishe (Proof Beyond Reasonable Doubt) kwamba kweli mtu kaua hata kama alikamatwa na kisu muda huo. Ushahidi usipotosha mtu anaachiwa nje vizuri tu na hamuwezi kumgusa. Na hizi ndiyo sheria zetu hapa na duniani kote.

Kutokana na Ugumu wa kushughulikia kesi za utakatishaji wa pesa India mwaka 2000 ilipitisha sheria inayoutwa THE PREVENTION OF MONEY LAUNDERING ACT. Sheria hiyo ilikuwa ina mambo makuu mawili.

  1. Ilitengeneza mahakama maalumu ya kushughulikia utakatishaji wa pesa na rushwa.
  2. Ilibadilisha tamaduni ambayo Waingereza waliileta inayosema mwendesha mashitaka inabidi uthibithishe utakatishaji huo kwa kutoa ushahidi.
Kwenye hili la pili mtu ukikutwa na mali na ukwasi ambao hauelezeki basi mali zote na akaunti za bank zinafungwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali. Mtuhumiwa atatakiwa yeye binafsi aeleze njia zipi alizotumia kupata utajiri huo. Kama mali ni zake basi ni lazima ataweza kuthibitisha na kama akishindwa serikali inanyang'anya hizo mali kwasababu zinakuwa hazina mtu.

Sheria hii ilipigwa sana vita lakini imesaidia India kwa kiasi kikubwa na hata Waingereza na nchi nyingine wemeiga. Mwanzoni walisema inavunja haki za binadamu lakini mwishowe ukweli ukabaki kwamba: Kama Pesa ni zako basi thibitisha. Mpaka sasa India imeshughulikia kesi za iutkatishaji wa pesa zaidi ya 1500 na kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda chanya.

Tanzania yetu sheria ni mbovu na hata mawakili wetu hawajfundishwa vizuri kuhusiana na hili. Financial Intelligence Unit (F.I.U) bado wanahangaika na makesi mengi makubwa ambayo yanakaa mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili. Na ukiangalia wezi bado wanapeta na mali zao na wananendelea kuwahonga majaji na mawakili.

Mwaka 2011 kama kumbukumbu zangu zimekaaa vizuri wakati DPP ni DR MBUKI FELESHI mwanasheria mkuu kutoka Bermuda alikuja kuwafundisha waendesha mashitaka wetu kuhusiana na hizo njia. Lakini cha kushangaza mpaka sasa serikali imekaa kimya kana kwamba mambo ni mazuri kumbe kuna uozo mwingi.

Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili nchi ikabili makanjanja wanaoficha hela ndani ya mzunguko na nje ya nchi:
Badilisha sheria ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na iwe kama India na Uingereza. Mtuhumiwa atuthibitishie jinsi alivyopata pesa zake. Hata kama kuna majumba na magari huko MASAKI, NJIRO au SAKINA akishindwa kueleza jinsi gani ameyapata tunanyang'anya.

Pili,kuna sheria inaitwa MUTUAL ASSISTANCE ACT, inahisiana na nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na masuala ya utakatishaji wa pesa na uhalifu mwingine. Nadhani ukienda Uingereza na USWISI utasaidiwa kwasababu wao nao wamesaini THE UNITED NATIONS CONVENTION ON THE PREVENTION OF CORRUPTION of 2000.

Tanzania tuliipitisha tarehe 25 May 2005, Uingereza tarehe 9 February 2006 na USWISI tarehe 24 September 2009. Kisheria kama umesaini huu mkataba ni lazima nchi washirika msaidiane, mheshimiwa raisi unasubiri nini kuwafuata BIG FISH?

Tatu, PCCB na FIU wamenyimwa meno. Haiwezekani taasisi huru kama hizi wawe wahusika wakuu lakini ruhusa za kushughulikia kesi wanaenda kuomba kwa DPP. Hii haijakaa sawa hata kidogo. Tunajua DPP ni wa serikalini na kama makanjanja wakitaka kumtumia anaweza kuchelewesha au asiruhusu kesi ifike mahakamani.

Hivyo basi sheria kama THE CRIMINAL PROCEDURE ACT irekebishwe ili PCCB na Financial Intelligence Unit wawashugulikie makanjanja huko huko bila kwenda kwa DPP. Na angalizo, hizi idara inabidi ziwajibike kwa bunge na waziri husika ili kama kuna uhuni unafanyika UMMAH wa Watanzania tujue kabisa. Hapa utazuia mtafuruku uliowahi kutokea huko nyumba baina ya Dr Hossea na Feleshi ambao walitunishiana misuli huku pesa zetu zikiendelea kupigwa bila huruma.

Nne, tunaomba tume ya maadili iwe inachapisha mali za mawaziri wako kila baada ya miezi sita. Ili tujue maendeleo na mgongano wa kimaslahi ili siku waziri akikutwa na ukwasi asiseme ni vijisenti tu . Hilo sisi hatulikubali kabisa maana viongozi wa nchi hii wakistaafu wanasema mafao yao ndiyo yananua hadi maghorofa na migodi.

Hili linaleta ukakasi kabisa kwasababu hatujui kiasi cha mafao hayo yenye kuweza kununua mgodi au kununua mansion ya Billion 3 kando ya bahari halafu huyo huyo anajiita ni mtoto wa mkulima. Hapana, ni lazima tuambieane hivyo vijisenti wamevitoa wapi.

Namaliza kwa kusema hata kama Dr Edward Hossea alikuwa ni CABALIST wa PUBLIC ENEMIES. Kuna kitu kwenye kitabu chake CORRUPTION IN TANZANIA kinasema kwamba tusiegemee sana kwenye Sheria za Uingereza au COMMON LAW hasa kwenye kutoa ushahidi kwa makosa kama rushwa na utakatishaji wa pesa.

Ni lazima tubuni njia zetu sisi binafisi ambazo zitaweza kutatua matatizo yetu kama Watanzania na siyo kukimbilia sheria za wazungu ambazo zimetungwa mwaka 1947 kwa ajili ya watu wa Uingereza.

Mwaka 2012 FINANCIAL TASK FORCE (FATF) au kikosi kazi cha kupigana na rushwa na utakatishaji wa pesa cha kikundi cha nchi Tajiri saba hapa duniani au G7; kwenye mkutano wa mawaziri walitoa mapendekezo au 2012 FATF

RECOMMENDATIONS ambazo zilisema kwa uwazi kabisa njia raisi ya kushughulikia rushwa na utakatishaji wa pesa ni kumwambia mtuhumiwa athibitishe kwamba pesa zake ni za halali. Hapa nadhani utawapunguzia mzigo mawakili wetu na mwishowe wizi utapungua kwa kiasi. Wezi watanyang'anywa mali na huku wakijutia jela udhalimu waliotufanyia. Ukibadilisha sheria hatutategemea kusikia watu fulani fulani wakisema unavunja haki za binadamu wakati THIS IS JUST THE MATTER OF PROCEDURE.

Mkuu izzo unaweza kuongezea kitu hapa.

Natanguliza shukrani zangu.
Young Malcom.

CC: Bukyanagandi, herikipaji , Pascal Mayalla , MOTOCHINI , MsemajiUkweli , zitto junior, Mchambuzi, Dotworld, Red Giant , Eiyer , MSEZA MKULU, Yamakagashi, Consigliere
 
Good advice!
It may be among the causes of kuhujumu uchumi.
There is no need to include political abbreviations of the political parts in sensitive issues like this,
Why?
In order to get a wide debate of your presentation.
 
Ni kweli hii ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na marekebisho yake ya mwaka 2012 inaonekana haina nguvu sana kwa sababu haizibani benki na taasisi mbalimbali khasa maduka ya kubadilishia fedha.

Hii sheria inabidi ibadilishwe haraka ili, kama raisi atabadilisha fedha, basi yule atakaejaribu kwenda kubadili basi anachukuliwa hatua za kisheria kwa kuficha fedha nje ya mzunguko.

Sheria hii ikibadilishwa hizi benki na taasisi zitawajibika kutoa taarifa kwa PCCB au police juu ya any suspicious activity kwenye akaunti au uhamisho wa fedha usoeleweka.

Kila benki iwe na mtu maalum kwa ajili ya ku-detect kusudio au kitendo cha kutaka kutakatisha fedha au Money Laundering Reporting Officer (MLRO) na huyu pia atawajibika kwa BOT na PCCB.

Serikali kupitia wizara ya fedha na BOT wachapishe muongozo unaoelekeza cha kufanya juu ya utakatishaji fedha na kosa lake yaani Financial Crime a Guide for firms na muongozo huo usambazwe katika kila idara ya serikali, mabenki, maduka ya kubadilishia fedha na taasisi mbalimbali binafsi, au za kimataifa kulingana na the law of the land.

Pia kuwe na Steering group yaani kundi la watalaam wa forensic accounting ambalo litaitwa Joint Money Laundering steering group ambalo litatoa ushauri wake wa kitaalam kwa serikali na vyombo vya fedha na wafanya biashara na kila mhusika katika kushughulikia fedha hasa maduka ya kubadili fedha.

Mwisho, ni kuhusu offshore Accounts, ni kwamba Uswiss na nchi zingine khasa baada ya sakata la viongozi wa FIFA ambao walipokea milungula na kuificha huko Zurich, sheria zimebadilishwa sasa ambapo inabidi uthibitishe chanzo cha fedha hizo na pia benki za uswiss nazo zinawajika kutoa taarifa za watu wanaohisiwa wameficha fedha huko.

Hii pia imekolezwa na issue ya Panama Papers ambayo mpaka sasa PCCB bado wanapekua makabrasha na hawajamkamata hata mtu mmoja.

Utaalam wa kitu si tu kupiga propaganda za UKUTA au mambo ya UVICCM, bali ni pamoja na kufanya brain-storming ya masuala nyeti kama haya kwenye JF, maana inaleta tija fulani vile!
 
Fact.
Taifa linawahitaji watu kama wewe kutoa michango yenye afya kubwa.
Hongera sana, nina Imani mchango wako Utawafikia wahusika.
 
Utaalam wa kitu si tu kupiga propaganda za UKUTA au mambo ya UVICCM, bali ni pamoja na kufanya brain-storming ya masuala nyeti kama haya kwenye JF, maana inaleta tija Fulani vile!

Kudos mkuu.
 
A. UTANGULIZI.

Wasalaam ndugu zangu,
Mimi siyo mfuatiliaji wa siasa lakini ni madau wa maendeleo na masuala mengi ya muhimu hapa nchini. Leo nimerudi kutoka matembezi yangu nikaingia mtandaoni na kuona alichokisema raisi juu ya watu kuficha pesa. Hili halikunistua sana lakini njia ya kulikabili tatizo ndiyo iliyonistua. Ukweli ni kwamba tatizo la kuficha pesa lipo sana hapa nchini lakini siyo kwa kiasi kikubwa kama ambavyo raisi kalizungumzia na kulifanya liwe: Na kwa kipindi hiki nashawishika kusema kwamba lenyewe siyo chanzo cha kuzorota uchumi hapa nchini kwetu.

D. NINI KIFANYIKE?

Mheshimiwa raisi ni lazima ajue kabisa kifungu kimoja cha sheria kinaweza kujenga au kubomoa nchi yetu. hadi mwaka 2000 nchi ya India ilikuwa inateswa sana na TATIZO la UTAKATISHAJI wa pesa. Walijaribu mbinu zote kama wewe lakini ikashindikana. Makanjanja walishajua kuficha hela USWIS huko. Kesi zilipopelekwa mahakamani mawakili walishindwa kuthibitisha wizi wowote ule kwasababu ushahidi walikuwa hawana. Pesa na mali zina majina mengine na huwezi kunyang'anya kwasababu ni kinyume cha sheria.

Kwenye SHERIA ZA USHAHIDI au THE LAW OF EVIDENCE, siku zote serikali ikipeleka kesi mahakamani ni lazima wao ndiyo wathibitishe kwamba mtu ni mwenye kosa. Mfano kama Mtu kaua inabidi waendesha mashitaka wathibitishe (Proof Beyond Reasonable Doubt) kwamba kweli mtu kaua hata kama alikamatwa na kisu muda huo. Ushahidi usipotosha mtu anaachiwa nje vizuri tu na hamuwezi kumgusa. Na hizi ndiyo sheria zetu hapa na duniani kote.

Kutokana na Ugumu wa kushughulikia kesi za utakatishaji wa pesa India mwaka 2000 ilipitisha sheria inayoutwa THE PREVENTION OF MONEY LAUNDERING ACT. Sheria hiyo ilikuwa ina mambo makuu mawili.

  1. Ilitengeneza mahakama maalumu ya kushughulikia utakatishaji wa pesa na rushwa.
  2. Ilibadilisha tamaduni ambayo Waingereza waliileta inayosema mwendesha mashitaka inabidi uthibithishe utakatishaji huo kwa kutoa ushahidi.
Kwenye hili la pili mtu ukikutwa na mali na ukwasi ambao hauelezeki basi mali zote na akaunti za bank zinafungwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali. Mtuhumiwa atatakiwa yeye binafsi aeleze njia zipi alizotumia kupata utajiri huo. Kama mali ni zake basi ni lazima ataweza kuthibitisha na kama akishindwa serikali inanyang'anya hizo mali kwasababu zinakuwa hazina mtu.

Sheria hii ilipigwa sana vita lakini imesaidia India kwa kiasi kikubwa na hata Waingereza na nchi nyingine wemeiga. Mwanzoni walisema inavunja haki za binadamu lakini mwishowe ukweli ukabaki kwamba: Kama Pesa ni zako basi thibitisha. Mpaka sasa India imeshughulikia kesi za iutkatishaji wa pesa zaidi ya 1500 na kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda chanya.

Tanzania yetu sheria ni mbovu na hata mawakili wetu hawajfundishwa vizuri kuhusiana na hili. Financial Intelligence Unit (F.I.U) badfo wanahangaika na makesi mengi makubwa ambayo yanakaa mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili. Na ukiangalia wezi bado wanapeta na mali zao na wananendelea kuwahonga majaji na mawakili. Mwaka 2011 kama kumbukumbu zangu zimekaaa vizuri wakati DPP ni DR MBUKI FELESHI mwanasheria mkuu kutoka Bermuda alikuja kuwafundisha waendesha mashitaka wetu kuhusiana na hizo njia. Lakini cha kushangaza mpaka sasa serikali imekaa kimya kana kwamba mabo ni mazuri kumbe kuna uozo mwingi.

Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili nchi ikabili makanjanja wanaoficha hela ndani ya mzunguko na nje ya nchi:

Badilisha sheria ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na iwe kama India na Uingereza. Mtuhumiwa atuthibitishie jinsi alivyopata pesa zake. Hata kama kuna majumba na magari huko MASAKI, NJIRO au SAKINI akishindwa kueleza jinsi gani tunanyang'anya.

Pili,kuna sheria inaitwa MUTUAL ASSISTANCE ACT, inahisiana na nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na masuala ya utakatishaji wa pesa na uhalifu mwingine. Nadhani ukienda Uingereza na USWIS utasaidiwa kwasababu wao nao wamesaini CONVENTION ON THE PREVENTION OF CORRUPTION of 2000. Tanzania tuliipitisha ratehe 25 May, 2005, Uingereza tarehe 9 February 2006 na USWIS tarehe 24 September 2009. Kisheria kama umesaini huu mkataba ni lazima nchi washirika msaidiane, mheshimiwa raisi unasubiri nini kuwafuata BIG FISH?

Tatu, PCCB na FIU wamenyimwa meno. Haiwezekani taasisi huru kama hizi wawe wahusika wakuu lakini ruhusa za kushughulikia kesi wanaenda kuomba kwa DPP. Hii haijakaa sawa hata kidogo. Tunajua DPP ni wa serikalini na kama makanjanja wakitaka kumtumia tu anaweza aisruhusu kesi isifike mahakamani. Hivyo basi sheria kama CRIMINAL PROCEDURE ACT irekebishwe ili PCCB na Financial Intelligence Unit wawashugulikie makanjanja huko huko. Na angalizo hizi idara inabidi ziwajibike kwa bunge na waziri husika ili kama kuna uhuni unafanyika UMMA wa Watanzania tujue kabisa. Hapa utazuia mtafuruku uliowahi kutokea huko nyumba baina ya Dr Hossea na Feleshi ambao walitunishiana misuli huku pesa zetu zikiendelea kupigwa bila huruma.

Nne, tunaomba tume ya maadili iwe inachapisha mali za mawaziri wako kila baada ya miezi sita. Ili tujue maendeleo na mgongano wa kimaslahi ili siku waziri akikutwa na ukwasi asiseme ni vijisenti tu tumuulize amevitoa wapi. Hilo sisi hatulitaki kabisa maana viongozi wa nchi hii wakistaafu wanasema mafao yao ndiyo yananua hadi maghorofa na migodi. Hili linaleta ukakasi kabisa kwasababu hatujui kiasi cha mafao hayo yenye kuweza kununua mgodi au kununua mansion ya Billion 3 kando ya bahari halafu huyo ni mtoto wa mkulima.

Namaliza kwa kusema hata kam Edward Hossea alikuwa ni CABALIST wa PUBLIC ENEMIES. Kuna kitu kwenye kitabu chake CORRUPTION IN TANZANIA kinasema kwamba tusiegemee sana kwenye Sheria za Uingereza au COMMON LAW hasa kwenye kutoa ushahidi kwa makosa kama rushwa na utakatishaji wa pesa. Ni lazima tubuni njia zetu sisi binafisi ambazo zitaweza kutatua matatizo yetu kama Watanzania na siyo kukimbilia sheria za wazungu ambazo zimetungwa mwaka 1947 kwa ajili ya watu wa Uingereza.

Mwaka 2012 FINANCIAL TASK FORCE (FATF) au kikosi kazi cha kupigana na rushwa na utakatishaji wa pesa cha kikundi cha nchi Tajiri saba hapa duniani au G7; kwenye mkutano wa mawaziri walitoa mapendekezo au 2012 FATF
RECOMMENDATIONS ambazo zilisema kwa uwazi kabisa njia raisi ya kushughulikia rushwa na utakatishaji wa pesa ni kumwambia mtuhumiwa athibitishe kwamba pesa zake ni za halali. Hapa nadhani utawapunguzia mzigo mawakili wetu na mwishowe wizi utapungua kwa kiasi. Wezi watanyang'anywa mali na huku wakijutia jela udhalimu waliotufanyia. Ukibadilisha sheria hatutategemea kusikia watu fulani fulani wakisema unavunja haki za binadamu wakati THIS IS JUST THE MATTER OF PROCEDURE.

Natanguliza shukrani zangu.
Young Malcom.

CC: UncleBen , idawa , Joel , Kamu-Ubungo Msewe , FisadiKuu , Nifah , MSEZA MKULU , mchambawima1 , Mchambuzi , joka kuu , Nguruvi3 , Bukyanagandi , Masunga Maziku

Mkuu, umeongea point sana. Please continue contributing here. Tatizo Tanzania suala la viongozi au wanasiasa kufuata sheria halipo. Ni kama wimbo tu za kujitumbuiza wenyewe. Kwenye kutunga sheria ndio usiseme. We don't have MPs with the capacity to analyse most of what is brought forth. I feel it's always partisan politicking
 
Mkuu, umeongea point sana. Please continue contributing here. Tatizo Tanzania suala la viongozi au wanasiasa kufuata sheria halipo. Ni kama wimbo tu za kujitumbuiza wenyewe.

Kuna ile issue ya akaunti za watanzania kule uswiss ambalo liliibuliwa na Zitto Kabwe, lakini hadi leo kimya!
 
Wow! just wow! Sina chochote cha kuongeza hapa ndugu yangu Malcom umesema yote.

Naimani watachukua ushauri huu na kuongezea wanacho ona kinastahili.

Tutoke kwenye mkwamo huu tusonge mbele.

NB kati ya sehemu ambayo Magufuli angeweza kufika mbali ni kuliacha bunge lisimamie serikali hila la serikali kusimamia bunge sio sahihi hata kidogo.

Naamini kabisa sehemu ambayo inaweza kuleta mabadiliko ya tofauti ni bungeni peke yake ,pale ndipo sheria zote hutungwa,pale ndipo tunapata uwakilishi wa wananchi na pale ndipo panatakiwa pasimamie serikali,mikataba mingi inapita pale japo sio yote ,wabunge wakiwa wamoja wanaweza kuomba muswaada wa kupitisha mikataba yote bungeni kabla ya kuidhinishwa.

Bunge likiwa halina meno basi hizi kashfa za kina Escorow na dada yake Richmond ama cousin wao Kagoda na mtoto wa nje Lugumi tusingezisikia

Magufuli aliheshimu bunge letu tukufu badala ya hivi vioja tunavyo viona sasa hivi.
Bunge tena sio sehemu ya kusimamia serikali ,badala yake imekua sehemu ya kusimamia vyama vya siasa hili ni tatizo kubwa ,kama anaona hili ni sahihi basi muda ndio mwalimu mzuri.

Ni hayo tu ndugu yangu Malcom
 
Uchambuzi mzuri sana, lakini hawataufanyia kazi, hii nchi sijui tunakosea wapi, watu wanaonekana kabisa ni watumishi wa umma na wana utajiri wa kutupwa lakini hakuna hatua zinazochukuliwa
 
Wow! just wow! Sina chochote cha kuongeza hapa ndugu yangu Malcom umesema yote.

Naimani watachukua ushauri huu na kuongezea wanacho ona kinastahili.

Tutoke kwenye mkwamo huu tusonge mbele.

NB kati ya sehemu ambayo Magufuli angeweza kufika mbali ni kuliacha bunge lisimamie serikali hila la serikali kusimamia bunge sio sahihi hata kidogo.

Naamini kabisa sehemu ambayo inaweza kuleta mabadiliko ya tofauti ni bungeni peke yake ,pale ndipo sheria zote hutungwa,pale ndipo tunapata uwakilishi wa wananchi na pale ndipo panatakiwa pasimamie serikali,mikataba mingi inapita pale japo sio yote ,wabunge wakiwa wamoja wanaweza kuomba muswaada wa kupitisha mikataba yote bungeni kabla ya kuidhinishwa.

Bunge likiwa halina meno basi hizi kashfa za kina Escorow na dada yake Richmond ama cousin wao Kagoda na mtoto wa nje Lugumi tusingezisikia

Magufuli aliheshimu bunge letu tukufu badala ya hivi vioja tunavyo viona sasa hivi.
Bunge tena sio sehemu ya kusimamia serikali ,badala yake imekua sehemu ya kusimamia vyama vya siasa hili ni tatizo kubwa ,kama anaona hili ni sahihi basi muda ndio mwalimu mzuri.

Ni hayo tu ndugu yangu Malcom

Umesomeka sana Uncleben, lets hope mambo yakae vizuri.
 
A. UTANGULIZI.

Wasalaam ndugu zangu,
Mimi siyo mfuatiliaji wa siasa lakini ni madau wa maendeleo na masuala mengi ya muhimu hapa nchini. Leo nimerudi kutoka matembezi yangu nikaingia mtandaoni na kuona alichokisema raisi juu ya watu kuficha pesa. Hili halikunistua sana lakini njia ya kulikabili tatizo ndiyo iliyonistua. Ukweli ni kwamba tatizo la kuficha pesa lipo sana hapa nchini lakini siyo kwa kiasi kikubwa kama ambavyo raisi kalizungumzia na kulifanya liwe: Na kwa kipindi hiki nashawishika kusema kwamba lenyewe siyo chanzo cha kuzorota uchumi hapa nchini kwetu.

Huenda ndugu raisi hajaambiwa ukweli na hawa watunga sheria na wanauchumi wetu wa hapa nchini. Tatizo kubwa kwenye uchumi kwa kipindi hiki siyo kuficha pesa tu, bali suala zima la UTAKATISHAJI (Money Laundering) wa pesa. Hivyo tukiamini na kusema kwamba kuficha pesa ndiyo tatizo kuu, tutakuwa tunaufumbia mambo ukweli na kulenga shabaha sehemu ambako adui hayupo. Kwa kifupi tu ni kupoteza nguvu na rasilimali za nchi hii.

Binafsi naamini raisi kuwa una nia njema kabisa, lakini wewe siyo mtaalamu wa mambo ya uchumi na sheria. Na kwa hali ya nchi ilivyo kwa kipindi hiki sisi wananchi wako wa kawaida hatutegemei kwamba wanasheria wetu au wanauchumi wanaweza kukuambia ukweli kuhusiana na nini haswa ndiyo kansa iliyojificha kwa sasa kwenye uchumi wa Tanzania.

B. UTAKATISHAJI WA PESA

Nini maana ya UTAKATISHAJI WA PESA?
Hiki ni kitendo cha kuzichukua pesa chafu au pesa yoyete iliyotokana na uhalifu na kuifua ili ionekane safi kisha unaiingiza kwenye mzunguko wa uchumi. Mfano mzuri tu Waziri fulani anaenda kusaini mkataba na wawekezaji fulani kwenye HOTELI X. Pindi anafanya hivyo anapewa bahasha ina cheki nono ya Bilioni kumi labda. Hali akijua kabisa kupokea ile cheki ni kitendo cha Rushwa na anweza kukamatwa baadae, waziri anaamua kuichukua ile pesa na kuipeleka kwenye mabenki ya nje au kuigawanya-gawanya kisha mtu anawekeza kwenye makampuni makubwa. (Shell Companies). Au kwa namna nyingine mtu anaweza tu akaweka kwenye akaunti ya mtu mwingine nje ya nchi na kisha pesa zinaweza kuja kama misaada.

Lakini mpaka sasa wenye uwezo wa kuficha pesa nje ya nchi ni wale tunaowaita BIG-FISH. Kwa hapa Tanzania wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa ndiyo wenye uwezo wa kusafirisha pesa kwenye mabenki ya nje (Transnational-Money Transfer).
Mheshimiwa raisi kwa hao unaofikiri pesa zimefichwa hapa nchini ni wachache sana; pesa chafu ipo kwenye mzunguko na inatumika kuwanunua wanasiasa na vyombo vya habari. Huu ndiyo ukweli mchungu; naamini njia yako ni njema sana kabisa lakini ingeweza kufanya kazi sana katika mazingira ya 90's na 80's.

Kwa sasa waharifu wengi wanapata pesa chafu kutokana na Rushwa, madawa ya kulevya, ujangiri, wizi , ulanguzi, kukwepa kodi na mengineyo mengi na pesa zao wanaziweka kwenye mzunguko na wala hawzifichi tena. Kadiri teknolojia na utawandawazi unakuwa na hivyo ndivyo uharifu nao unazidi kuwa wa juu (sophisticated). Pesa hazifichwi NDANI tena, ZINAFICHWA KWENYE MZUNGUKO. Hizo pesa ndiyo zimenunua majumba na zinaendelea kujenga mengi huko MASAKI, MBEZI BEACH, UNUNIO, MSASANI, NJIRO, SAKINA etc.
Wataalamu kwa lugha ya kiingereza wanasema "INJECTING DIRTY MONEY INTO THE LEGAL ECONOMY".

Mwaka jana nilienda PCCB nikapata wasaha wa kufanya majadiliano na baadhi ya maofisa wakubwa pale. Wakanipa mifano mizuri tu kama THE TEGETA ESCROW SCANDAL na jinsi UTAKATISHAJI WA PESA ULIVYOFANYIKA. Wale wahanga wa ile skandali kama Tundu Lissu alivyosema, kweli walibeba pesa kwenye Lumbesa, magunia na sanda lakini hawakuzificha ndani, walizificha kwenye mzunguko. Nyingi zilitumika kukupigia wewe kampeni na nyingine zikanunua Dollar, Pound na Euro na kupelekwa nje ya nchi. Na hii ni moja ya sababu kubwa kabisa Shillingi kuanguka hapa nchini. Mheshimiwa raisi ni lazima ushauriwe vizuri kabisa kwamba tatizo siyo kuficha pesa ndani, tatizo ni kutakatisha pesa na kuziingiza tena kwenye mzunguko.

IGP Mstaafu ndugu Saidi Mwema kwenye Makala yake iitwayo "CURRENT SITUATION AND COUNTERMEASURES AGAINST MONEY LAUNDERING: TANZANIA’S EXPERIENCE". Amekiri kabisa kwamba Utakatishaji wa pesa ni moja ya kosa ambalo linaumiza uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa hakuna sheria sahihi ambazo zinaweza kulishinda tatizo. Ni kosa linalofanywa na wataalamu waliojipanga wakipata msaada kutoka kwa Wansheria na Wanauchumi wazuri kwa nchi. Mwaka juzi tena Dr Edward Hossea alisema zaidi ya asilimia 30 ya pato la taifa inapotea kwenye rushwa na utakatishaji wa pesa. Lakini mheshimiwa hili mbona hujalitaja? Huu ndiyo ufichwaji wa pesa haswaaa hawa wanaoficha ndani ni vidagaa vidogo sana ndani ya bahari kubwa.

C. MTAZAMO WA KISHERIA.
Nisema kabisa hata wataalamu wa sheria wanakiri kuna tatizo kubwa kwenye sheria za nchi ambazo wajanja wamezitengeneza na kuacha nafasi (gaps; lacunae) ili waendelee kupiga pesa. Naamini kabisa kwa msaada wa BOT unaweza kubadilisha noti ya elfu kumi kwasababu hilo lipo ndani ya uwezo wako lakini nakuahidi hata hizo noti mpya zitafichwa tena. (HUU NDIYO UKWELI MCHUNGU).
Ukisoma Sheria ya utakatishaji wa PESA au ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na marekebisho yake ya mwaka 2012 yameorodhesha makosa mengi sana yanosababisha Utakatishaji wa Pesa. Lakini mpaka leo hii pesa inazidi kutakatishwa na kuingizwa kwenye mzunguko.

Kwa kifupi sheria za nchi ni mbovu na haziwapi mawakili wetu uwanja mpana wa kuweza kuwashughulikia ipasavyo watakatisha pesa. Hivyo hata wewe ukichapisha pesa upya bado sheria haikupi nguvu ya kufanya hivyo. Nitakupa mfano mzuri kabisa katika hili. Mwaka 1983na 1983 Marehemu Sokoine alianza mchakato wa kuwasaka wahujumu uchumi. Naye alikuwa ana nia njema kama wewe lakini kwa bahati mbaya safari yake iliishia hapo Morogoro.

Vijana wa UVCC ndiyo walileta hamasa kubwa kwa Sokoine. Aliwashughulikia sana wahujumu uchumi, watu wengi walifungwa sana lakini mwisho wa siku ikaja gundulika kwamba wanaoguswa ni Vidagaa na wale BIG-FISH waliendelea kupeta tu mtaaani. Alipojaribu kuwagusa hata sheria za CHAMA na NCHI ziliwalinda. Inasemekana aliwataka hadi kuwafuata mawaziri wakuu wastaafu, wakubwa wengine pamoja na viongozi wa dini:Lakini ilishindikana, na kwanini kwasababu moja yeye hakuwa Raisi na mbili sheria ile ilikaa vibaya.

THE ECONOMIC SABOTEURS ACT ya 1984 ilitengeneza mahakama ya Mafisadi ya kwanza kabisa hapa nchini. Ilikaliwa na watu watatu wawili ambao ilikuwa siyo lazima wawe wanasheria. Mtu ulikuwa ukikamatwa moja kwa moja na pesa za taifa unapelekwa kwenye hiyo mahakama na unanyimwa haki ya kujitetea na wala huwi na wakili wako. Wewe ni ndani tu: Kama ilivyo ada, BIG FISH waksema ule ni uvunjaji wa haki za binadamu hasahasa THE PRESUMPTION OF INNOCENCE and RIGHT TO LEGAL REPRESENTAION. Kweli njia za Sokoine zilivunja sana haki za binadamu lakini wengi walimpiga vitab siyo kwasababu wanajali haki za binadamu bali matumbo yao.

Ile sheria ilirekebishwa na kesi zikarudishwa Mahakama kuu na serikali ikaendlea kucheza Twisti pamoja na mafisadi. Kwa hivyo mheshimiwa raisi kjama anataka kufanya kitu kinachoeleweka ni lazima atambue kwanza tatizo ni Utakatishaji wa Pesa. (Money Laundering) kwasababu pesa ziko ndani ya mzunguko na kama kuficha wanazificha nje. Mimi naomba raisi asije akashindwa katika hili, alenge shabaha upande adui alipo.

D. NINI KIFANYIKE?

Mheshimiwa raisi ni lazima ajue kabisa kifungu kimoja cha sheria kinaweza kujenga au kubomoa nchi yetu. hadi mwaka 2000 nchi ya India ilikuwa inateswa sana na TATIZO la UTAKATISHAJI wa pesa. Walijaribu mbinu zote kama wewe lakini ikashindikana. Makanjanja walishajua kuficha hela USWIS huko. Kesi zilipopelekwa mahakamani mawakili walishindwa kuthibitisha wizi wowote ule kwasababu ushahidi walikuwa hawana. Pesa na mali zina majina mengine na huwezi kunyang'anya kwasababu ni kinyume cha sheria.

Kwenye SHERIA ZA USHAHIDI au THE LAW OF EVIDENCE, siku zote serikali ikipeleka kesi mahakamani ni lazima wao ndiyo wathibitishe kwamba mtu ni mwenye kosa. Mfano kama Mtu kaua inabidi waendesha mashitaka wathibitishe (Proof Beyond Reasonable Doubt) kwamba kweli mtu kaua hata kama alikamatwa na kisu muda huo. Ushahidi usipotosha mtu anaachiwa nje vizuri tu na hamuwezi kumgusa. Na hizi ndiyo sheria zetu hapa na duniani kote.

Kutokana na Ugumu wa kushughulikia kesi za utakatishaji wa pesa India mwaka 2000 ilipitisha sheria inayoutwa THE PREVENTION OF MONEY LAUNDERING ACT. Sheria hiyo ilikuwa ina mambo makuu mawili.

  1. Ilitengeneza mahakama maalumu ya kushughulikia utakatishaji wa pesa na rushwa.
  2. Ilibadilisha tamaduni ambayo Waingereza waliileta inayosema mwendesha mashitaka inabidi uthibithishe utakatishaji huo kwa kutoa ushahidi.
Kwenye hili la pili mtu ukikutwa na mali na ukwasi ambao hauelezeki basi mali zote na akaunti za bank zinafungwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa serikali. Mtuhumiwa atatakiwa yeye binafsi aeleze njia zipi alizotumia kupata utajiri huo. Kama mali ni zake basi ni lazima ataweza kuthibitisha na kama akishindwa serikali inanyang'anya hizo mali kwasababu zinakuwa hazina mtu.

Sheria hii ilipigwa sana vita lakini imesaidia India kwa kiasi kikubwa na hata Waingereza na nchi nyingine wemeiga. Mwanzoni walisema inavunja haki za binadamu lakini mwishowe ukweli ukabaki kwamba: Kama Pesa ni zako basi thibitisha. Mpaka sasa India imeshughulikia kesi za iutkatishaji wa pesa zaidi ya 1500 na kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda chanya.

Tanzania yetu sheria ni mbovu na hata mawakili wetu hawajfundishwa vizuri kuhusiana na hili. Financial Intelligence Unit (F.I.U) bado wanahangaika na makesi mengi makubwa ambayo yanakaa mahakamani kwa zaidi ya miaka miwili. Na ukiangalia wezi bado wanapeta na mali zao na wananendelea kuwahonga majaji na mawakili. Mwaka 2011 kama kumbukumbu zangu zimekaaa vizuri wakati DPP ni DR MBUKI FELESHI mwanasheria mkuu kutoka Bermuda alikuja kuwafundisha waendesha mashitaka wetu kuhusiana na hizo njia. Lakini cha kushangaza mpaka sasa serikali imekaa kimya kana kwamba mambo ni mazuri kumbe kuna uozo mwingi.

Yafuatayo ni mambo ya kufanya ili nchi ikabili makanjanja wanaoficha hela ndani ya mzunguko na nje ya nchi:

Badilisha sheria ANTI-MONEY LAUNDERING ACT of 2006 na iwe kama India na Uingereza. Mtuhumiwa atuthibitishie jinsi alivyopata pesa zake. Hata kama kuna majumba na magari huko MASAKI, NJIRO au SAKINA akishindwa kueleza jinsi gani ameyapata tunanyang'anya.

Pili,kuna sheria inaitwa MUTUAL ASSISTANCE ACT, inahisiana na nchi mbalimbali kushirikiana kupambana na masuala ya utakatishaji wa pesa na uhalifu mwingine. Nadhani ukienda Uingereza na USWISI utasaidiwa kwasababu wao nao wamesaini THE UNITED NATIONS CONVENTION ON THE PREVENTION OF CORRUPTION of 2000. Tanzania tuliipitisha tarehe 25 May 2005, Uingereza tarehe 9 February 2006 na USWISI tarehe 24 September 2009. Kisheria kama umesaini huu mkataba ni lazima nchi washirika msaidiane, mheshimiwa raisi unasubiri nini kuwafuata BIG FISH?

Tatu, PCCB na FIU wamenyimwa meno. Haiwezekani taasisi huru kama hizi wawe wahusika wakuu lakini ruhusa za kushughulikia kesi wanaenda kuomba kwa DPP. Hii haijakaa sawa hata kidogo. Tunajua DPP ni wa serikalini na kama makanjanja wakitaka kumtumia anaweza kuchelewesha au asiruhusu kesi ifike mahakamani. Hivyo basi sheria kama THE CRIMINAL PROCEDURE ACT irekebishwe ili PCCB na Financial Intelligence Unit wawashugulikie makanjanja huko huko bila kwenda kwa DPP. Na angalizo, hizi idara inabidi ziwajibike kwa bunge na waziri husika ili kama kuna uhuni unafanyika UMMAH wa Watanzania tujue kabisa. Hapa utazuia mtafuruku uliowahi kutokea huko nyumba baina ya Dr Hossea na Feleshi ambao walitunishiana misuli huku pesa zetu zikiendelea kupigwa bila huruma.

Nne, tunaomba tume ya maadili iwe inachapisha mali za mawaziri wako kila baada ya miezi sita. Ili tujue maendeleo na mgongano wa kimaslahi ili siku waziri akikutwa na ukwasi asiseme ni vijisenti tu . Hilo sisi hatulikubali kabisa maana viongozi wa nchi hii wakistaafu wanasema mafao yao ndiyo yananua hadi maghorofa na migodi. Hili linaleta ukakasi kabisa kwasababu hatujui kiasi cha mafao hayo yenye kuweza kununua mgodi au kununua mansion ya Billion 3 kando ya bahari halafu huyo huyo anajiita ni mtoto wa mkulima. Hapana, ni lazima tuambieane hivyo vijisenti wamevitoa wapi.

Namaliza kwa kusema hata kama Dr Edward Hossea alikuwa ni CABALIST wa PUBLIC ENEMIES. Kuna kitu kwenye kitabu chake CORRUPTION IN TANZANIA kinasema kwamba tusiegemee sana kwenye Sheria za Uingereza au COMMON LAW hasa kwenye kutoa ushahidi kwa makosa kama rushwa na utakatishaji wa pesa. Ni lazima tubuni njia zetu sisi binafisi ambazo zitaweza kutatua matatizo yetu kama Watanzania na siyo kukimbilia sheria za wazungu ambazo zimetungwa mwaka 1947 kwa ajili ya watu wa Uingereza.

Mwaka 2012 FINANCIAL TASK FORCE (FATF) au kikosi kazi cha kupigana na rushwa na utakatishaji wa pesa cha kikundi cha nchi Tajiri saba hapa duniani au G7; kwenye mkutano wa mawaziri walitoa mapendekezo au 2012 FATF
RECOMMENDATIONS ambazo zilisema kwa uwazi kabisa njia raisi ya kushughulikia rushwa na utakatishaji wa pesa ni kumwambia mtuhumiwa athibitishe kwamba pesa zake ni za halali. Hapa nadhani utawapunguzia mzigo mawakili wetu na mwishowe wizi utapungua kwa kiasi. Wezi watanyang'anywa mali na huku wakijutia jela udhalimu waliotufanyia. Ukibadilisha sheria hatutategemea kusikia watu fulani fulani wakisema unavunja haki za binadamu wakati THIS IS JUST THE MATTER OF PROCEDURE.

Natanguliza shukrani zangu.
Young Malcom.

CC: UncleBen , idawa , Joel , Kamu-Ubungo Msewe , FisadiKuu , Nifah , MSEZA MKULU , mchambawima1 , Mchambuzi , joka kuu , Nguruvi3 , Bukyanagandi , Masunga Maziku , Dotworld , vyuma , Econometrician
" naamini njia yako ni
njema sana kabisa lakini ingeweza kufanya kazi
sana katika mazingira ya 90's na 80's." patam hapo
 
Nataman huu mchango ungetolewa mbele ya wabunge ,mawaziri husika au mkuu wa kaya.. Ni mchango muhimu na, wakaueleweka sana..
Naamin iwa hali ilivo hata siku moja mkuu wa kaya hawez kuwakaba hao mabig fish.. Umenikumbusha aliese mabilion ni hela ya mboga tu na yule aliyesema amepewa pole ya msiba…
 
Back
Top Bottom